Je, niwekeze kupitia JATU Company PLC?

Priest_

Member
Jun 17, 2021
11
24
Kutokana na watu wengi kuniandikia kuniuliza kama ni salama kuwekeza pesa JATU company PLC. Nimeamua kufanya utafiti na maswali kwenye utafiti wangu yalikuwa kama ifuatavyo;-

1. Nani anaongoza JATU?
2. Je, ni biashara gani wanafanya? Pia hii biashara ni hatarishi kwa pesa yangu?
3. Je, nini maana ya shares za JATU? Pia ni salama?

Nani anaongoza Jatu?
Kawaida kabla ya kufanya uwamuzi wa kuwekeza, ni swala la msingi kujiuliza kwamba nani unampa pesa yako. Hapa unatakiwa kuangalia "managament" ya kampuni husika. Kwasababu management ndio inatoa DIRA yote ya biashara, na hii DIRA ndio itafanya wewe kupata pesa au kupoteza pesa. Unatakiwa kusoma wasifu wa management nzima na kujiuliza swali, je hawa watu kwenye management, wana uzoefu wa kutosha kuendesha aina ya hii biashara? Kanuni ni kwamba, "ukitaka kulinda pesa yako,utawekeza sehemu ambayo una uwakika kwamba mtu ambaye utampa pesa ana uzoefu wa kutosha, kama si hivyo,kuna uwezekano wa kupoteza pesa".

Ukiangalia kwa sasa, management ya JATU anaongozwa na wana sheria, ambao hakuna sehemu yeyote wameonesha uzoefu kwenye maswala ya kilimo,Viwanda na Saccos. Management hii ingefaa kama JATU ingekuwa ni kampuni ya sheria.

Biashara
Biashara kubwa ya kampuni ni uwekezaji kwenye kilimo. Kilimo ni uwekezaji ambao unategemea na msimu, rutuba ya sehemu na ubora wa mazo husika. Pia ni biashara yenye hatari kubwa. Kwasabu ya bei kushuka na kupanda.

Pia lengo lao ni kukusanya wakulima wadogo na kuwawezesha kulima kwa kisasa. Ni wazo zuri,lakini halina Tija au ni biashara mabayo haina faida. Hii ni kwasabu kimo kidogo kina gharama kubwa kuliko kilimo kikubwa. kuwekeza strategy kwenye wakulima wadogo, sio strategy endelevu kwa afya ya kampuni.

Strategies:-
a/Ili kuweza kunufaika na kilimo, kampuni inatakiwa kuja na mpango au namna ya kuhifazi mazao,ili kuweza kukabili bei ya mazo ikiwa chini na kuepuka hasara. Paka sasa, hakuna sehemu yeyote ambayo wameonesha namna ambayo watatumia kuepuka hasara ya kushuka kwa bei ya mazo.

b/Njia nyingine ya kuweza kunufaika na kilimo, ni kutumia "Viwanda".Hii ni kubadilisha mazo na kufanya bidhaa. Kwenye maelezo, wanasema wanampango wa kufungua viwanda,lakini paka sasa hawajaweza kuonesha hivyo. Pia wanasema watakuwa wananunua mazo, lakini hakuna sehemu yeyote ambayo wameonesha kwamba wanatarajia kufanya nini na ayo mazo baada ya kununua.

Shares
Shares ambazo wanatoa ni "ordinary shares". Ukiwa na hizi share, wanakuhesabu wewe kuwa ni moja ya sehemu ya kampuni. Inamaana utakuwa na uwezo wa kupanga mipango ya uwendeshaji wa kampuni. Hatari ya kuwa na shares za aina hii ni kwamba, kuna uwezekano au hatarini kupoteza 100% ya uwekezaji wako. Pia utalipwa faida tu, pale management watapo amua kuwalipa.

Hitimisho

Kuna red flags nyingi sana namna ya hii kampuni inavyo endeshwa. Wameweza kuja na wazo zuri, lakini hawajaweza kuonesha ni namna gani watafanya kufikia malego. Pia kampuni imeanzishwa toka mwaka 2016 lakini, paka sasa hawajaweza kuonesha mahesabu yao ya mwaka tangu waanze kufanya biashara. Bila shaka hiii sio safe investment.
 
Wajinga ndio waliwao, kila uchwao wajinga wanapungua na wengine wanazaliwa. Elimu Elimu elimu, kuna wenye elimu lakini haiwasaidi kutambua ukweli bora wasio na elimu
 
Watanzania tuna kasumba ya kutojua vitu na kujibu ujinga ujinga. Kama hujui kitu bora unyamaze. Kwa yeyote ambaye anaulizia kampuni ya Jatu, ni kwamb ina kila dalili ya utapeli. Wanaweza wakawa wanalima kweli lakini sio kiasi wanachokitangaza wao. Ukishawapa pesa, hutawaona tena. Inaweza kukuchukua mwaka au miaka miwili au mitatu kuwaona au kuongea na mtu. Watakukwepa kwa nguvu zote.

Management yao ina watu wana abuse sana matumizi ya pesa. Wanaweza kuwa wanatumia pesa za wawekezaji kwenye miradi mingine ambayo haina mahusiano kabisa na kilimo. Hivyo ukilima wakakwambia umevuna gunia 10, ukiwauzia hawawezi kukulipa. Utadai mpaka unakufa. Ila ukiwambia kwamba unataka hiyo pesa uirudishe kwenye kilimo, wanakubali bila shida yoyote. Sasa hii inaleta maswali;

1) Je, hawa watu wanalima kweli?
2) Wanakosaje pesa ya kukulipa kwa mazao yako na wanapataje hela hiyo hiyo kama ukikubali kuendelea kulima?

CEO wa hiyo kampuni anabadilisha simu kila siku. Ukiongea naye leo, kesho ana namba nyingine ya simu. Anakwepa watu kwa sababu watu wengi wanadai pesa na hawalipwi.

Sasa fikiria; unawezaje kulima mazao, ukaweka mbolea, mvua ikanyesha, ukavuna na kuuza tatizo tu likajitokeza kwenye malipo?? Hawa watu wana abuse pesa za watu!
 
Naongezea swali,

Tofauti ya mfumo wa biashara wa JATU na iliyokua Mr. Kuku ni ipi?
 
Sijajua kwa nini wanajiita kampuni. Wapo kama wapiga deals. Wamejaza wanasheria wengi kuliko wataalam wa kilimo. Kibaya zaidi, wanadanganya kila mkulima anayelima nao. Yaani hata wewe ukienda leo watakwambia vitu ambavyo sio kweli. Managers na CEO wanajificha kabisa. Wanatembea na ma baunsa kwenye mikutano yao. Hivi ni viashiria vya hatari sana.

Sasa hivi wapo mikoani wanawambia watu kwamba "anza na ekari moja". Wakati huo huo kuna watu wamelima nao ekari 50 lakini hawajawalipa kwa miaka mitatu na hawapokei simu zao. Sasa jiulize, huyo wa ekari moja wanataka kumfanya nini?

CEO anabadilisha namba ya simu kila siku.

Kwa ufupi wanatumia vibaya pesa ya wawekezaji. Sijui usalama wa taifa uko wapi. Hawa watu inabidi wakamatwe haraka sana kabla hawajadanganya Watanzania wengi. Usalama upo busy na mikutano ya Chadema lakini wanaohatarisha maisha ya watanzania ni hawa watu.
 
Sijajua kwa nini wanajiita kampuni. Wapo kama wapiga deals. Wamejaza wanasheria wengi kuliko wataalam wa kilimo. Kibaya zaidi, wanadanganya kila mkulima anayelima nao. Yaani hata wewe ukienda leo watakwambia vitu ambavyo sio kweli. Managers na CEO wanajificha kabisa. Wanatembea na ma baunsa kwenye mikutano yao. Hivi ni viashiria vya hatari sana.

Sasa hivi wapo mikoani wanawambia watu kwamba "anza na ekari moja". Wakati huo huo kuna watu wamelima nao ekari 50 lakini hawajawalipa kwa miaka mitatu na hawapokei simu zao. Sasa jiulize, huyo wa ekari moja wanataka kumfanya nini?

CEO anabadilisha namba ya simu kila siku.

Kwa ufupi wanatumia vibaya pesa ya wawekezaji. Sijui usalama wa taifa uko wapi. Hawa watu inabidi wakamatwe haraka sana kabla hawajadanganya watanzania wengi. Usalama upo busy na mikutano ya Chadema lakini wanaohatarisha maisha ya watanzania ni hawa watu.
Nahisi hao jamaa kweli ni wajanja wajanja maana kwa hekari wanazotaja kulima ni kama vile wanatuambia wamefikia viwango vya uwekezaji vya mabilionea wa kimagharibi, humor ndani Kuna mikono ya mafisadi vigogo wa kisiasa ndio kiisa cha kiburi hicho, huwezi kuiba hadharani mbele ya usalama wa taifa.
 
Ni wazo nzuri, ila hakuna vitabu kwenye public domain.

Utaliwa ndg yangu.

DSE suspends trading of JATU shares

The Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) has suspended agro-business JATU from trading for a period of two months.

According to the DSE, the suspension is necessary because of the ongoing Initial Public Offering (IPO) of 15,000,000 new shares.

“Following the guidance from Capital Markets and Securities Authority (CMSA), notice is hereby given on the suspension from trading of JATU shares at the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) effective from June 1 to July 28, 2021, to necessitate the synchronisation of JATU’s Corporation Actions related to split for existing listed shares and price adjustment as well as the ongoing new IPO,” reads the statement

The DSE adds that all shares following the share split for existing shares together with new shares subscribed during the IPO will be credited electronically and deposited in the Central Depository System on July 29.

JATU traded at Tsh1,200 ($0.52) per share on DSE before the suspension.

www.theeastafrican.com
 
Sijajua kwa nini wanajiita kampuni. Wapo kama wapiga deals. Wamejaza wanasheria wengi kuliko wataalam wa kilimo. Kibaya zaidi, wanadanganya kila mkulima anayelima nao. Yaani hata wewe ukienda leo watakwambia vitu ambavyo sio kweli. Managers na CEO wanajificha kabisa. Wanatembea na ma baunsa kwenye mikutano yao. Hivi ni viashiria vya hatari sana.

Sasa hivi wapo mikoani wanawambia watu kwamba "anza na ekari moja". Wakati huo huo kuna watu wamelima nao ekari 50 lakini hawajawalipa kwa miaka mitatu na hawapokei simu zao. Sasa jiulize, huyo wa ekari moja wanataka kumfanya nini?

CEO anabadilisha namba ya simu kila siku.

Kwa ufupi wanatumia vibaya pesa ya wawekezaji. Sijui usalama wa taifa uko wapi. Hawa watu inabidi wakamatwe haraka sana kabla hawajadanganya watanzania wengi. Usalama upo busy na mikutano ya Chadema lakini wanaohatarisha maisha ya watanzania ni hawa watu.
Unauliza kuhusu usalama wa taifa?? au nimekusoma vibaya kwenye paragrafu ya mwisho?
 
Mkuu,

vipi wale watu ambao walisha nunua shares kabla ya kufungiwa? Inamaana ndio "wameliwa"?

Asante
 
Sijajua kwa nini wanajiita kampuni. Wapo kama wapiga deals. Wamejaza wanasheria wengi kuliko wataalam wa kilimo. Kibaya zaidi, wanadanganya kila mkulima anayelima nao. Yaani hata wewe ukienda leo watakwambia vitu ambavyo sio kweli. Managers na CEO wanajificha kabisa. Wanatembea na ma baunsa kwenye mikutano yao. Hivi ni viashiria vya hatari sana.

Sasa hivi wapo mikoani wanawambia watu kwamba "anza na ekari moja". Wakati huo huo kuna watu wamelima nao ekari 50 lakini hawajawalipa kwa miaka mitatu na hawapokei simu zao. Sasa jiulize, huyo wa ekari moja wanataka kumfanya nini?

CEO anabadilisha namba ya simu kila siku.

Kwa ufupi wanatumia vibaya pesa ya wawekezaji. Sijui usalama wa taifa uko wapi. Hawa watu inabidi wakamatwe haraka sana kabla hawajadanganya watanzania wengi. Usalama upo busy na mikutano ya Chadema lakini wanaohatarisha maisha ya watanzania ni hawa watu.

truth speaking kiukweliii hawaeleweki
 
Back
Top Bottom