Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 45
Nimeshika Gazeti la Uhuru la leo, mbele yangu yapo pia magazeti mengine ya hapa nyumbani ikiwemo gazeti la serikali la habari leo. Ndani ya gazeti la CCM la uhuru kuna matangazo matano ya serikali ya wizara, idara, wakala na halmashauri tofauti tofauti. Kwa mahesabu ya haraka jumla ya matangazo haya ni kati ya milioni 3 na 4 za kodi za watanzania wote bila kujali itikadi. Ndani ya gazeti la habari leo, gazeti la serikali- ukiondoa hotuba ya waziri. Hakuna hata tangazo moja la ukurasa mzima kati ya yale ambayo yametolewa na serikali katika gazeti la CCM. Huu si ufujaji wa kodi zetu? Kwanini gazeti lenye kufikia wasomaji wasiofikia elfu tano lipewe matangazo yote haya wakati magazeti yanayofikia wasomaji zaidi ya elfu 20 ikiwemo gazeti la serikali kuachwa? Je, huu si mpango kabisa wa kuendesha CCM na taasisi zake kwa kutumia fedha za walipa kodi wa itikadi mbalimbali na wasio na chama? Kuna maana gani kwa serikali kutoa matangazo katika chombo ambacho hakifikii umma wa walio wengi? Ruzuku ya takribani bilioni mbili ambayo CCM inapata kila mwezi inatumika kufanya nini kama bado wanaiba kodi zetu kwa upande wa nyuma kuendesha chama chao halafu wanaendelea kututangazia kuwa serikali haina fedha za kuwasaidia wanawake?