Utani Wa Wapemba

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Kuna wakati mmoja alisafiri Mjapani, Mtanzania bara na Mzanzibari kwenye boti ndogo, mara boti yao ikaanza kuingia maji na kuzama, ilibidi watafute njia ya kujiokoa, kama[FONT=Bookman
 Old

 Style] kawaida mjapani alianza kwa kutupa vitu vyake binafsi [/FONT]kama CD player, hi-fi, radio,PC nk... ili kupunguza uzito, Mtanzania bara na Mzanzibari walimwangalia kwa mshangao sana na ku toamini.

Mjapani akawaambia 'Msijali…bado tunavyo vyingi
sana nchini kwetu hivi vitu…'.

Boti ilikuwa bado inaendelea kuzidi kuzama. Mtanzania bara bila ya kusita na yeye akaanza kutupa vitu vyake
kama vile vinyago, vitenge nk... Akawaambia wenzake 'Msijali… bado vipo vyingi sana nyumbani'.

Boti bado ilikuwa inazama. Mjapani na Mtanzania bara wakawa wanamwangalia Mzanzibari atafanya nini?! Mzanzibari akaziangalia mbata na karafuu zake na bila ya kusita na ya wasiwasi wowote alimsukuma Mtanzania bara baharini.

Maskini [FONT=Bookman Old Sty
le] Mtanzania bara
alikuwa hajui kukoga akazama. Mjapani alishtuka
[/FONT]sana. Mzanzibari akamwambia ' Usijali …wako wengi sana hawa kwetu Zanzibar,Mpaka Pemba siku hizi wanaonekana.

Nice Joke man! Naenda kulala baada ya kucheka kidogo
 
Kuna wakati mmoja alisafiri Mjapani, Mtanzania bara na Mzanzibari kwenye boti ndogo, mara boti yao ikaanza kuingia maji na kuzama, ilibidi watafute njia ya kujiokoa, kama kawaida mjapani alianza kwa kutupa vitu vyake binafsi kama CD player, hi-fi, radio,PC nk... ili kupunguza uzito, Mtanzania bara na Mzanzibari walimwangalia kwa mshangao sana na ku toamini.

Mjapani akawaambia 'Msijali…bado tunavyo vyingi
sana nchini kwetu hivi vitu…'.

Boti ilikuwa bado inaendelea kuzidi kuzama. Mtanzania bara bila ya kusita na yeye akaanza kutupa vitu vyake
kama vile vinyago, vitenge nk... Akawaambia wenzake 'Msijali… bado vipo vyingi sana nyumbani'.

Boti bado ilikuwa inazama. Mjapani na Mtanzania bara wakawa wanamwangalia Mzanzibari atafanya nini?! Mzanzibari akaziangalia mbata na karafuu zake na bila ya kusita na ya wasiwasi wowote alimsukuma Mtanzania bara baharini.

Maskini Mtanzania bara alikuwa hajui kukoga akazama. Mjapani alishtuka
sana. Mzanzibari akamwambia ' Usijali …wako wengi sana hawa kwetu Zanzibar,Mpaka Pemba siku hizi wanaonekana.

Joke yako ni chuki tupu. check hiyo read, baharini unakoga au unaogelea?
 
Pamoja na utani na nini?hivi waliowengi upande mwengine nadhani ni wapemba hasa tanga, dsm, moro, shinyanga, ila hawapo moshi kwa wachaga tuu.

Ila pia cdhani kama wapemba wana utani na kabila jengine?wadau kama mnalijua mtutonye
 
Wazenji kwa chenga tu huwa wanatupiga sana ila mwisho wa siku, sisi ndiyo tunafunga goli.

Bila sisi hamuwezi kuishi. Sasa hao Wapemba waliojaa pale Dar mbona sisi hatusemi?

Kweli Nyani haoni makalio yake.
 
PETITION: Unataka Dr. Slaa agombee URAIS mwaka 2010? Jiandikishe kwenye listi.
Dokta si kasema wampatie mshahara wake wa ubunge kwa miaka mitano atakayokosa ubunge s kama akiamua kugombea nafasi ya urais ameshaona mbali kuwa atadondokea pua..sijui kama hii petition bado ipo!!
 
Utani huo si mzuri, utani wa kujikweza kuwa wewe ni bora kuliko mwenzio hauna maana kabisa katika karne hii tulionayo, tutoe utani watu wote wafurahi, nakushauri jifunishe kujenga daraja badala ya ukuta
 
Acha kueneza chuki, kuna mamia ya wapemba wanaishi bara mbona wabara hawalalamiki au kama vipi wazuiwe wasije bara waijenge pemba.
 
Acha kueneza chuki, kuna mamia ya wapemba wanaishi bara mbona wabara hawalalamiki au kama vipi wazuiwe wasije bara waijenge pemba.
Kuna aliye lalamika..!? Nadhani upo kwenye wrong thread....!
 
What kind of a Joke is this? I do not buy it. I do not find a joke in it except asinine statements.
 
watu wako tofauti sana mbona ni utani wa kawaida sana nimecheka mpaka stress zimeisha ahsante sana kaka
Tatizo watu wanakuwa na chuki zisizo na msingi ndugu yangu...! Wanataka yale tu wanayo yapenda wao.
 
Back
Top Bottom