Utani wa wahindi

sultanwjps

Member
Jun 27, 2010
14
0
Wahindi walikua wakimtania Mhindi singa singa wakasema kua Masinga singa wote hua wendawazimu
ifikapo saa 6 kamili za Mchanana wakasisitiza kua hii sio utani bali ni kweli. singa singa mmoja akahamaki sana. ela siku iliyofuata akaenda kwa yule aliyesema hivyo kiasi saa 5 na dakika 50 ili kumhakikishia
kua maneno yake sio ya kweli . na bahati nzuri kitambo hicho hicho kila siku hua inapita gari ya muuza maziwa
na hua ananunua gilasi moja ya maziwa , hivyo alikuja na gilasi yake tayari ili ikipita gari ya maziwa atanunua.
bahati gari ya maziwa ilikuja saa 5 na dakika 58 hivyo alikimbia kwanza kununua maziwa upesi upesi
na baada ya kununua ilikua saa 6 kamili kwani alikua amevaa saa na kila mara anaangalia.
sasa huyu singa singa akaja mbio kwa yule aliyesema kua masinga singa hua wendwazimu ifikapo saa 6 za mchana ili kumhakikishia kua yeye hana wazimu. na alikua ameshika gilasi yake ya maziwa mkona wa kushoto
nae yule mhindi akamuuliza yule singa singa "Singa singa ni saa ngapi sasa " nae singa singa bila kusita
akatizama saa yake , lakini sasa alisahau kua ameshika gilasi yake ya maziwa mkono wakushoto na kwa wakati
huo alimwaga yale maziwa wakati akigeuza mkono kuangalia saa, nae yule Mhindi akamcheka sana yule singa singa na kumuambia 'jee sasa umekubali maneno yangu ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom