Utani na Msichana ninaye fanya naye kazi unataka kunivunjia ndoa yangu

Pumb---u hizi tabia lazima tuzikomeshe!! ila nimeipenda story yako na nimekupa thanx
 
Pole sana kaka,cha msingi sitisha mazoea na huyo dada na mweleze yaliyokupa kwa sababu ya sms yake.na mkeo mweleze ukweli ukiona hakuelewi basi tafuta mzee akusaidie
 
Ma mangi ha haiwezekani chalii msichana hata ka kama mna utani kiasi gani akakutumia sms kama hiyo tena usiku na akifahamu una mke hapo kuna kitu hujatueleza,mi naona uligonga mara 1-2 na sasa ulitaka kumwacha nae kaamua kuchafua,ni mawazo yangu tuu.
 
Situation kama hizi inabidi huwe mwepesi wa kufikiri....,ungecheka saaana alafu ukasema kumbe kweli unanipenda.., yaani umeshinda mtego, tulipanga na rafiki yangu tukupime.., hivi kweli wife ningekuwa nategemea sms kama hiyo unadhani ningeacha simu chumbani.., dah kumbe mshikaji alisema kweli mi nilisema wife hawezi kukubali mtego mdogo hivi..., dah wife embu twende tukalale......
mmmh! Kuamini hii inabidi bibie awe na kichwa cha panzi.
 
Situation kama hizi inabidi huwe mwepesi wa kufikiri....,
ungecheka saaana alafu ukasema kumbe kweli unanipenda.., yaani umeshinda mtego, tulipanga na rafiki yangu tukupime.., hivi kweli wife ningekuwa nategemea sms kama hiyo unadhani ningeacha simu chumbani.., dah kumbe mshikaji alisema kweli mi nilisema wife hawezi kukubali mtego mdogo hivi..., dah wife embu twende tukalale......

Mhhhh!!! VoR, kama hujazoea kusema uongo sio rahisi kupata mawazo kama hayo! Labda awe ni mzoefu, kwahiyo lazima ajiandae kwa situatio kama hiyo! Otherwise utabaki unashangaa tu........
 
Unajua kilichonifanya mimi niondoke nyumbani ilikuwa ni kunusuru ule ugonvi usije ukaanza kukusanya watu pale nyumbani. Mkuu jitahidi sana masuala ya ndani kwako yasitoke nje. Kwa gharama yoyote ile. Suala la ugomvi ndani ya nyumba yako na mkeo likakusanya watu nyumbani kwako mpaka wanavunja mlango ni la aibu sana na halitakaa liwatoke hao majirani kichwani mwao. Na watalitumia kila mahali wakiwaona mna furaha. Utasikia "Unaowaona hawa sasa hivi wana furaha, usiku tunaweza tusilale kwa ugomvi wao". hapo mpo kwenye harusi na mamsap mnacheza "Embe dodo limelala mchangani" mmeshasahau ya nyuma, wenzenu wanatumia kama weak point. Ni vyema sana kuhakikisha ugomvi wa ndani kwako haswa na mkeo hautoki nje. Maana mara zote uwezekano wa kuelewana na mkeo na kurudi katika maisha ya kama zamani ni mkubwa. Majirani huwa wanachukulia huo ugomvi kama weak point ya kuwatangaza vibaya.
to some extent uliamua vyema kuondoka ili ugomvi usiwe wa kijiji. Rudi home atakuwa keshapoa akigomba kalete mkeka lala chini tena bila cha kujifunika,mara 2 atalainika atakufata hapo hapo chini...baba naniliuh twende kalale kitandani....hapo unatumia nafasi vizuri ktk kuleta suluhu na utani tani uachage bwana!
 
Mchukue huyo msichana muende naye nyumbani mkaombe msamaha. Mueleze mkeo ukweli mbele ya huyo msichana.
Ikiwezekana nenda na mzee. Najua mkeo ni muelewa, atakuelewa tu.
 
Nashauri uchukue mtumishi mwenzako mmoja mwenye busara ajuaye uhusiano wenu wa utani na huyo dada, chukua na huyo dada mtani wako nendeni kwa mama watoto hali halisi ielezwe na yule mwenye busara na huyo binti naye aeleze kinaga ubaga, akiri kufanya uatani na wewe, akiri kutuma meseji hiyo, akiri haikulenga mahusiano halisi ya kimapenzi na wewe na mwisho aombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza na hatimaye aahidi hatarudia tena utani wa jinsi hiyo.
 
Kuna msichana nafanya naye kazi katika kampuni moja. Sasa tumezoea kweli kutaniana na kuitana majina ya Kimahaba huku kukiwa hakuna uhusiano wowote wa Kimapenzi. Jana saa nne usiku nikiwa nafanya kazi zangu kwenye kompyuta sebuleni na simu ikiwa chumbani akanitumia ujumbe unaosomeka "Honey, its too cold today, I wish you could be beside me now, I cant Imagine how the situation could be". Aisee, mama watoto alikuwa kajipumzikia kitandani huyoo akaamka na kwenda mezani, akachukua simu na kusoma meseji. Kilichojiri hapo nilisikia mlango wa chumbani umefunguliwa, baadaye nikasikia paa, nimepigwa kofi zito la shavuni. Nilipozinduka nikamkuta analia, akaniambia haya twende chumbani ukavae uende ukampe joto huyo malaya wako. Nikasita, nikapigwa tena kofi la begani na kuambiwa nyanyukaaaa, malaya mkubwa wewe. Unataka kuniuwa niache watoto wanakula shida na malaya zako. Kwa kweli ilikuwa ni zengwe sana. na leo nimemkia hotel, baada ya kuona vurugu inataka kuanza kushirikisha majirani. Wife amekataa kabisa kunielewa, leo nimempigia simu hapokei, meseji hajibu binti nimemueleza yaliyonikuta kwa sababu ya ushenzi wake anachekacheka tu, natamani nimmeze kwa kweli. Natafakari nielekee wapi nkitoka hapa kazini.Nawasilisha kwa ushauri.

mkeo ana mapenzi ya kweli na wewe ingawa ni mkali lkn kwa watu wa aina yako huyo anakufaa sana. Unaonekana ni kiwembe wa chini chini, huyo dada kama hujammega basi ulishamtengenezea mazingira na yeye akahisi unamchelewesha. Ulikosea sana kwenda kulala hotelini, nani atathibitisha madai yako?? ungaliweza kwenda kulala kwa bestman wako au ungeenda kwa matron wake na kumuomba ampigie simu amtaarifu kwamba uko kwake, mengine mngeeongea asubuhi yake ... hili angalau lingalimpunguzia hasira na ku-keep a certain trust katika utetezi wako ... lkn kwa ulivyofanya umeshaharibu big time mtu wangu ... hakuna kitu kibaya katika ndoa kama ku-lose trust ya mkeo ... ni suala la muda tu kabla ya kumegewa, unless otherwise awe na msimamo wa ajabu sana.

rudi nyumbani mapema, tafuteni mazingira ya utulivu na mkaliongee hilo tatizo na mkeo, jitahidi uwezavyo mambo ya familia yako yaishie katika kuta kuta nne za chumba chenu!!

pole mangi!!
 
Mhh kaka kumbe na wewe umekaliwa hivyo unazabwa vibao?pole kwa yaliyokukuta wenzio tukifika home huwa tunazima simu mpaka asubuhi
 
Kuna msichana nafanya naye kazi katika kampuni moja. Sasa tumezoea kweli kutaniana na kuitana majina ya Kimahaba huku kukiwa hakuna uhusiano wowote wa Kimapenzi. Jana saa nne usiku nikiwa nafanya kazi zangu kwenye kompyuta sebuleni na simu ikiwa chumbani akanitumia ujumbe unaosomeka "Honey, its too cold today, I wish you could be beside me now, I cant Imagine how the situation could be". Aisee, mama watoto alikuwa kajipumzikia kitandani huyoo akaamka na kwenda mezani, akachukua simu na kusoma meseji. Kilichojiri hapo nilisikia mlango wa chumbani umefunguliwa, baadaye nikasikia paa, nimepigwa kofi zito la shavuni. Nilipozinduka nikamkuta analia, akaniambia haya twende chumbani ukavae uende ukampe joto huyo malaya wako. Nikasita, nikapigwa tena kofi la begani na kuambiwa nyanyukaaaa, malaya mkubwa wewe. Unataka kuniuwa niache watoto wanakula shida na malaya zako. Kwa kweli ilikuwa ni zengwe sana. na leo nimemkia hotel, baada ya kuona vurugu inataka kuanza kushirikisha majirani. Wife amekataa kabisa kunielewa, leo nimempigia simu hapokei, meseji hajibu binti nimemueleza yaliyonikuta kwa sababu ya ushenzi wake anachekacheka tu, natamani nimmeze kwa kweli. Natafakari nielekee wapi nkitoka hapa kazini.Nawasilisha kwa ushauri.

Vipi mangi umesharudi home? hebu tupe maendeleo.
 
Mama makonde yalizidi jamaa kaona bora aokoe uso wake, yaonekana huyo mama ni noma...jamaa mpaka kakimbia ULINGO...huyo atakuwa ASHA NGEDERE nini

Lol...
Magu umenivunja mbavu walah!..,.. Looo.. Kweli huyo wife ni noma bt jamaa kayataka mwenyewe...
 
Mhh kaka kumbe na wewe umekaliwa hivyo unazabwa vibao?pole kwa yaliyokukuta wenzio tukifika home huwa tunazima simu mpaka asubuhi

Khaaaa!
Wewe nae unamwona mangi kakaliwa? Mbona hata wewe umekaliwa pia? Why uzime cm kama sio unaogopa vibao? Kuzima cm ni ishara ya WOGA kwa wife, kama unajiamini acha cm on tena chumbani afu kakae sebuleni km hayajakukuta yaliyomkuta mangi.
 
Halafu wewe.........Kesi yetu tafuta wakili mzungu!
 
Pole sana kwa yaliyokukuta mkuu,
Inaonekana ulizidisha utani na huyo dada na haya sasa ni madhara yake. nakushauri tu kwa nyakati zijazo kwa mtu married kama wewe jaribu kuwa na mipaka ya utani na marafiki wako wa jinsi tofauti ili yasije kukukuta yaliyokukuta.
Kwa hili lililotokea, ni kama maji yameshamwagika , hayawezi kuzoleka ......

Pole ...
 
Mhhhh!!! VoR, kama hujazoea kusema uongo sio rahisi kupata mawazo kama hayo! Labda awe ni mzoefu, kwahiyo lazima ajiandae kwa situatio kama hiyo! Otherwise utabaki unashangaa tu........
Unajua sometimes ukweli unaonekana ni uongo kuliko ukweli.., kwahiyo hapo mtu inabidi ufanye kila kitu ili kuokoa ndoa, na hapo akili inabidi ifanye kazi..., kwahiyo angeanza kwa kucheka sana angekuwa anacheka huku akili inafanya kazi
 
God has seen you struggling with something. God says its over. A blessing is coming your way. If you believe in God send this message on, please don't ignore it, you are being tested. God is going to fix two things (BIG) tonight in your favour. If you believe in God, DROP EVERYTHING AND PASS IT ON.TOMORROW WILL BE THE BEST DAY OF YOUR LIFE. DONT BREAK THIS CHAIN. SND THIS TO 14 FRNDS IN 10MINS WEN U READ....
 
Utajuuta kumfahamu..ingekuwa mie sijui ningetumbukiza simu kwenye ndoo ya maji kwanza
Sina kusema ..imagine ndo mkeo ana utani wa hivo na mtu wewe ungefanya nini?
This is tooooooooooooooooooo much Mangi meru sijui mangi sina ...
 
Back
Top Bottom