Utandawazi (Globalization): Adui hatari wa Afrika asiyesemwa kwa undani madhara yake

MJENGA

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
884
848
Ndugu zangu poleni na majukumu. Leo nimeona tukumbushane jambo muhimu la kuliewa sote Waafrika.

Nimeona tujikumbushe ni wapi wakubwa wa dunia wanatupeleka sisi tuitwao dunia ya tatu. Ni kwamba kuanzia karne ya 14 hadi 16 huko Ulaya tayari vijitaifa (nation states) vilikuwa vimeanza kupata nguvu za kidola na kiuchumi.

Hivyo kwasababu ya ubabe, matumizi ya nguvu kujitanua kidola kuliibuka vita kubwa sana iliyopiganwa kwa takribani miaka 30 huku vita hiyo.kwa upande mwingine ikibebwa na imani ya katoliki dhidi ya waasi wake walioongozwa na Martin Luther.

Mwaka 1648 Uliitishwa mkutano wa amani uitwao Westphalia ambapo vijistate hivyo vilikubaliana mambo kadhaa ikiwemo kusitisha vita na kila mmoja kuheshimu mipaka ya mwingine na kamwe kutoingilia uhuru wa.maswala ya ndani ya nchi mwingine (sovereignty).

Baada ya hapo uchumi wao ulikua sana na kuka wa na hitaji la masoko na wafanyakazi wenye gharama nafuu wa viwandani na mashambani.

Mwaka 1884/1885 waliitana wakubwa hao chini ya Chancellor wa Ujerman Bismack wakatugawana sisi waafrika kwaajili ya kututawala na kupata malighafi za viwanda vyao na nguvu kazi isiyo na gharama.

Hapo ndipo dhana ya utandawazi (globalization ) ilipoanza. Waafrika tulinyonywa sana hadi damu wakati huo. Babu zetu walichukuliwa kwwnda kutumikishwa Ulaya na Amerika.

Kwa mchango wa nguvu kazi za babu zetu na wizi wa malighafi na rasilimali zetu waliweza kuendeleza nchi zao kwa kujenga mifumo imara ya mitaji na faida kwaajili ya maendelwo zaidi.

Ukoloni ulipokwisha miaka ya 1960 wakubwa hao walikaa tena miaka ya 1980 wakasema lazima tuurudishe ukoloni Afrika tena kutokana na kunogewa na wizi na uporaji.

Walikuja na mpango wa marekebisho ya kimfumo (Structural Adjustment Program- SAP) ukiwa ni.mpango uliolenga kuuzima mpango kababmbe wa waafrika kudai marekebisho mapya ya mfumo wa uchumi duniani (New International Economic Order) ambao uliitaka jumuiya ya kimataifa kurekebisha mifumo nyonyaji ya kibiashara kupitia WTO, IMF na WB ili waafrika nao wawe na mazingira sawa ya ushindani wa kibiashara na kiuchumi.

Hivyo SAP ililazimisha waafrika kuhurisha mifumo yao yankiuchumi (liberalozation of economy) kwa kuruhusu masoko huria (free markets) na mfumo wa siasa za vyama vingi.

Wakubwa hao walijua fika kuwa waafrika hatuna uwezo wa kufanya investments kubwa hivyo kwa uhuria huo wa.masoko ungewapa nafasi wao kutawala biashara na shughuli zingine za kiuchumi Afrika.

Aidha kupitia mifumo ya vyama vingi vya siasa walijua kuwa tutagawanyika na hivyo watatutawala kirahisi kupia vyombo vyake vyankinyonyaji vya IMF, WTO na WB. Baada ya kufanikiwa katika maeneo hayo tunashuhudia Afrika ikiwa na migogoro mingi ya kisiasa huku wao wakiendelea kuchota rasilimali zetu kilaini kabisa.

Viwanda vingi vilivyoanzishwa wakati wa mwanzo baada ya uhuru katika nchi.nyingi za Afrika vimekufa si kwasababu nyingine bali kwa mikono ya wakubwa hao kutotaka tupate mifumo imara ya kiuchumi ya kututoa huku tuliko.

Ndugu zangu utandawazi kwa maana halisi si kama watu mnavyoutafsiri kirahisirahisi, huo ni ukoloni kabisa unaotumia nyenzo na vyombo vya kimataifa kuinyonya Afrika.

Madeni makubwa ya nchi za Afrika ambayo yanadaiwa na WB yanatengenezwa kimkakati (si rahisi nikaeleweka hapa) ili nchi za Afrika ziendelee kuwa tegemezi.

Hivyo kwa picha hiyo, ni vema tuelewe malengo ya wazungu kwetu sisi waafrika kuwa siyo.mazuri. Na ni vema mkajua kuwa.wakubwa hao hawapendi.kusikia nchi masikini zinajitambua na kuanza kupambana kujikomboa.

Tanzania ilipo sasa imejitambua na hongera sana Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kuutambua ulaghai wa wakubwa hao na hivyo kuamua kwa dhati kuikomboa Tanzania.

Kelele unazopigiwa kuhusu madai ya udikteta na kujaribu kukuharibia taswira ili uchukiwe na wananchi wako ili mwishowe wao wajihalalishie kukutoa madarakani.

Ninakuomba, simama imara kwani Watanzania wenye akili kama mimi tuko wengi na tunakuunga mkono. Unapoipeleka Tanzania kila mwenye akili timamu anaona.

Kasi ya maendeleo si ya kuridhisha kama tulivyozoea kuimbiwa bali wakati huu kasi ni kubwa kiasi inawatisha wakubwa hao. Pigana Jemedari tuko nyuma yako.

Watanzania wote niwaombe tumuunge mkono Rais wetu na tusikubali kwa namna yoyote adhalilishwe na manyang'au na.majizi. Tumuombee aongoze ukombozi wa kweli.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa. Siku si nyingi Afrika itahesabiwa haki na hao wanaotutawala na kutunyonya na kututesa. Mungu amewaandalia mahali pao stahiki.
 
Naona unabariki wizi wa kura, kwa taarifa yako hatuko tayari kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kama una maslahi binafsi na cheo cha rais hiyo ni juu yako. Tunataka tume huru ya uchaguzi na hatuko tayari kuburuzwa, hiyo propaganda mfu kawapekelekee wasujudu viongozi wenzako. Tuna maendeleo gani ya kuwatisha wazungu, mpaka mlazimishe kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja?
 
Wana vyuo tu wanalilia hawajaingiziwa mikopo utawala huhu unajipambanua kuwafukuza watumishi hewa ila mwamka wa tano huu no ajira sasa hapa JPM kwa nini asilaumiwe???or tuwalaum mabeberu?
 
Naona unabariki wizi wa kura, kwa taarifa yako hatuko tayari kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kama una maslahi binafsi na cheo cha rais hiyo ni juu yako. Tunataka tume huru ya uchaguzi na hatuko tayari kuburuzwa, hiyo propaganda mfu kawapekelekee wasujudu viongozi wenzako. Tuna maendeleo gani ya kuwatisha wazungu, mpaka mlazimishe kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja?
Wizi wa kura unaingiaje hapo, hiyo ni analysis ya kisomi hutaitaki achana nayo unaikubali ifanyie kazi.
 
Wana vyuo tu wanalilia hawajaingiziwa mikopo utawala huhu unajipambanua kuwafukuza watumishi hewa ila mwamka wa tano huu no ajira sasa hapa JPM kwa nini asilaumiwe???or tuwalaum mabeberu?
Ni vigumu kuelewa, nakushauri zama shule utaelewa ninachokizungumza.
 
Wakihoji kuhusu demokrasia,uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa kuongea,haki za binadamu n.k mna waita mabeberu...

Ila wakiwapa hela za mikopo na ufadhili mbalimbali kama ujenzi wa vyoo vya shule..mnawaita wawekezaji na wadau wa maendeleo.

Akili kumkichwa.
#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Wao wanaua warabu hovyo, nani anawahoji?
 
Hoja yako nzuri. Tatizo lako hujagusia demokrasia, ndipo wengi wasemapo tunarudi nyuma,na huenda ni ukweli. Najua kumbukumbu unazo ssna mkubwa kuhusu hiyo demokrasia. Jitahidi jazia kwenye Uzi wako ushibe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ssante kwa kunikumbusha. Lakini demokrasia yenyewe brohter/sister ni ile tuliyoletewa na wazungu kama sharti la SAP (nilishalisema hata hivyo)
 
Kama serikali ya awamu ya tano haikopi kwanini deni la taifa limekua karibu kidogo kufikia mara mbili ya ya deni lililoachwa na awamu ya nne?

Nakubaliana nawe kua mambo mengine serikali ya awamu ya tano imepambana nayo vizuri. Mojawapo ni kuwatingisha WHO kua na monopoly right ya kutangaza magonjwa ya mlipuko kwa nchi yoyote! Hadithi ya ugonjwa wa ZIKA na NIMR ni mfano halisi. Hii ni sehemu ambayo mataifa makubwa yanatumia kuwapiga pesa na rasilimali mataifa madogo(ni topic inayojitegemea)

SAP ilikua ni vigumu kwa serikali ya awamu ya pili kuacha kuitekeleza kutokana na hali ya kiuchumi iliyokuwepo Tanzania hasa miaka ya mwisho ya utawala wa awamu ya kwanza, tatizo utekelezaji hasa wa sera ya ubinafsisha wa mashirika ambao ulitekelezwa hadi awamu ya tatu ulifanyika kiholela na kifisadi

Mambo ambayo yana mushkeli kwa awamu hii ni uwazi katika matumizi hasa ya utekelezaji wa miradi yote mikubwa kama ujenzi wa SGR, ujenzi wa mradi wa umeme wa Stiglers, na hata ununuzi wa ndege
Kungekua na ushirikishwaji wa wakilishi wa wananchi(Bunge) hakika ingekua ni legacy kubwa na ya kujivunia kwa Watanzania wote

Pili double standards katika kuwa treat raia na viongozi inatia doa kwenye mazuri inayofanya serikali ya awamu hii
 
Wana vyuo tu wanalilia hawajaingiziwa mikopo utawala huhu unajipambanua kuwafukuza watumishi hewa ila mwamka wa tano huu no ajira sasa hapa JPM kwa nini asilaumiwe???or tuwalaum mabeberu?
Unasoma chuo gani wewe mbona huwezi kuandika vizuri??
 
Sesten Zakazaka,
Nimekuelewa vizuri. Napenda ubishaji wa hoja kama hivi. Sasa, kama SAP ilikuwa inevitable, kwanini NIEO ambayo ilipendekezwa na nchi za Africa kuhusu mfumo rafiki wa kiuchumi ilikataliwa na badala yake ikaletwa SAP ambayo kama ulivyosema imechangia kubomoa kabisa mifumo ya uwekezaji. (Isome SAP vizuri na wala hutalaumu eti ilifanyika kiholela. Uholela ndiyo ulikuwa msingi wake ili kutuyumbisha totally). Asante.
 
Kama umepita shule na umetusua kwa ujinga huu bora nibaki na darasa la7 langu
Baki nalo likusaidie kuendelea na lawama zako kwa serikali bila kujua mfumo wa dunia unavyoziyumbisha nchi za Afrika. Kalaga baho ndugu.
 
Nakubaliana na wewe kwamba tuwe na chama kimoja.

Ila kiwe kingine hata SAU, CHAUMMA au ADC na siyo CCM.
 
mleta mada ni mbumbumbu.

huyo unaemsifia analeta maendeleo kila alichovaa na silaha zinazomlindq na gari anazotumia na ndege anazonunua kinyume na taratibu za manunuzi hadi kifaa alichotia kidole kusajili laini ya simu hadi simu anahotumia hadi kile kimota alipanda siku anazurura kwenye rubondo vyote ame-import kutoka kwa mabeberu.
 
Nchi za magharibi hazijaacha agenda yao ya.msingi ya kuendelea kuitawala Afrika ingawa awamu hii si kwa kutumia mabavu tena bali kwa kutumia mbinu ovu za kiuchumi mfano kutoa mikopo kwa Africa yenye masharti magumu, kuweka rules of the game sawa kwenye biashara za kimataifa huku wakijua tutakwama kutokana na uwezo wetu mdogo. Kutuletea liberal politics ili tugawanyike watutawale. Na pia laboratory diseases kama Ebola, HIV, SARs nk ili watengeneze fedha na kucompromise mifumo yetu ya kiafya ikiwemo utoaji kinga za magonjwa mbalimbali. Kwwnye teknolojia wametuletea gadgets ambazo zimetuenslave unakuta muda wote mtu yuko kwenyw mtandao bila tija yoyote. Kusambaa kwa silaha Africa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni matokeo ya ninachokisema. Hivi ninavyozungumza, Afrika inaendelea kumezwa na foreign military bases nyingi zikiwa za wamamrekani na mahasimu wao wa kiuchumi China. Waliofika Kaskazini mwa Afrika wanajua ninachokisema.
Hivyo baadhi yetu tusiropoke tu eti kwa sababu tunamchukia Magufuli, tuseme ukweli kuhusu bali halisi na.kile Magufuli anajaribunkupambana nacho.
 
Nakubaliana na wewe kwamba tuwe na chama kimoja.

Ila kiwe kingine hata SAU, CHAUMMA au ADC na siyo CCM.
Here we are not talking of political parties buddy, tunazungumzia adui mkubwa globalization ambaye kwa bahati.mbaya hajasemwa na kujadiliwa kisawasawa. Iwe CCM au chama chochote, kikubwa ni kujua tunapambana na nani na siyo Magufuli
 
Back
Top Bottom