UTAMU wa nyama ya mtu umemponza mzee wa Mpanda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
UTAMU wa nyama ya mtu umemponza mzee wa Mpanda anadai ni tamu lakini polisi hawakukubaliana naye wakaamua kumtia mbaroni. Eti alifundishwa na babu yake kwamba akiona polisi wanaenda kumkamata ameze uume ili asionekane.

Dawa hiyo washikaji kama unafanya dili chafu na hutaki polisi wakukamate wewe tafuta uume wa mwanamume umeze. Sasa kazi kwako kama utataka kumuua hilo utajua mwenyewe au utameza akiwa hai hiyo kazi kwako.

Maswali sitaki kwani mwenye majibu anashikiliwa na polisi wa Mpanda yeye ndiye yuko kwenye nafasi ya kujibu maswali yako yote. Watu wakasoma habari hiyo ilitikisa katikati ya wiki, wakashangaa kwamba kweli dunia inaelekea mwisho. Nani atakuja kuinusuru na majanga haya? Kila mtu ana jibu lake wengine watadai Yesu Kristo wengine wanasema mwisho ni siku ya kufa kwako.

Sasa ukishangaa hayo je, yaliyotokea huko Tanga, mwanadada Eshe alivyokuwa anamshughulikia mtoto wa kike hadi anamlegeza. Polisi nao wanashangaa iweje mwanamke mwenzake amlegeze mwanamke mwenzake kiasi hicho.

Hayo ndio mambo ya dunia yetu ambayo wahenga walitwambia ukishangaa ya Musa utaona ya firauni. Hivyo wadau mambo mengine kama hayo ukiyasikia wewe nyamaza tu maana hatujui kesho kutakuwa na kituko gani.

Hebu tuachane na hayo twende kwenye maonesho ya Nanenane, maana wiki hii macho na masikio yetu yako kwenye viwanja vikubwa ambako bidhaa za wakulima zinaoneshwa. Mambo yako Arusha, Morogoro, Dodoma na huko Mbeya. Mdau mmoja akaniandikia kwamba ukienda kwenye viwanja hivyo hakuna cha mazao yanayooneshwa zaidi ya nyama choma na bia ndizo zimechukua nafasi za maonesho.

Akanipa umbeya tena kuwa kule Arusha na Dodoma wanaotamba ni wachomanyama na wengi zaidi wanaozichangamkia nyama hizo sio wakulima bali ni maofisa wa halmashauri ambao ndio wameteka maonesho hayo kwa kisingizio kuwa wanaonesha mazao yao.

Jamani lini halmashauri zikalima? Nikahoji tena iweje wakulima wasijitokeze wakati kuna kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, mdau hakuwa mchoyo akanisisitizia kuwa tatizo kiingilio cha kushiriki kikubwa na wakulima wengi ni walalahoi ndio maana wakayakacha maonesho ya mwaka huu.

Akanidokeza sababu ya pili kuwa mwaka huu ulioisha mazao hakuna, kaya nyingi zinahemea chakula na hazina hata mazao ya kwenda kuonesha. Wengi wanaiomba serikali iwapelekee chakula hicho, cha kwenda kuonesha Nanenane watakitoa wapi? Lakini ni kweli! Basi nami nimebaki tu kushangaa habari za mbuzi beberu linalotoa maziwa ya ajabu.

Tena beberu lenyewe limetokea Bagamoyo. Sasa unashangaa nini hujui tena mambo ya Mlingotini ambako watu wanapatia vyeo na utajiri? Safari hii wameamua kuvunja ukimya wamewapelekea mbuzi wa ajabu, beberu lakini anakamuliwa maziwa.

Ajabu mbuzi huyo anakamuliwa kila siku lakini hapo hapo ana uwezo wa kupanda majike na kuyazalisha. Mbuzi wa faida kweli kweli! Sikiliza anatoa maziwa robo lita kila siku, lakini usidhani ni shoga, sio shoga kama unabisha peleka mbuzi jike wako uone.

Lakini kinachosisimua zaidi ni kwamba maziwa yake ni murua hasa kwa vijana ambao wanapenda kutumia dawa za Wamasai kuongeza nguvu. Kijana kazi kwako kama nguvu zako una wasiwasi nazo, nenda Bagamoyo ukanywe maziwa ya beberu.

Ukitoka huko mambo yako yatakuwa murua na mama Ngina atafurahia kazi utakavyoifanya. Kila la kheri vijana wenzangu mtakaofunga safari kwenda Mlingotini kumwona kaka Abdallah Jumanne mkazi wa Kijiji cha Kilomo.

Chanzo: HabariLeo | Maziwa ya beberu na nguvu za kiume
 
Back
Top Bottom