Utamu wa Maji ya Bendera: Muulize Bashe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamu wa Maji ya Bendera: Muulize Bashe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Jan 7, 2009.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Imenishangaza sana kukutana na habari moja katika gazeti la Mtanzania Daima (7 Janauari, 2009). Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho "Bashe Awashukia Wanaomtuhumu Mkapa" Hussein Bashe ambaye ni MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), anadai watu wanaomhusisha Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na ubadhirifu wamefilisika kisiasa. Hivi kweli huu ndo uhondo wa Ukada, ukereketwa au UTAJO!!Huyu mkereketwa wa SISIEMU anaendelea kudai kuwa wote wanaomuandama Mkapa ni wanasiasa wavivu wa kufikiri na wanajitafutia umaarufu wa kisiasa. Akifunga Mkutano wa Baraza Kuu la Vijana wa Chama cha SISIEMU wilayani Kinondoni kada huyo alidai nanukuu “Muacheni Mkapa apumzike, mengi ameyafanya kwa nchi hii watu wanalalamika tu kila kukicha, inashangaza kusikia kauli ya Spika kuwa atapokea hoja binafsi kuhusu Kumjadili Mkapa bungeni, hivi kuna mangapi ya msingi ya kuzumgumziwa bungeni badala ya kufikiria kumjadili Mkapa"

  Yaani kumjadili Mkapa Bungeni si muhimu kwa mujibu wa huyu Bashe. Mie siamini kama huyu Bashe sijui Basha ni mvivu wa kufikiri kama anavyodhani watanzania wako hivyo, bali MAJI ya BENDERA anayokunywa ni MATAMU kuliko taabu wanazozipata WATANZANIA kutokana na UFISADI aliofanya Mkapa na Kampuni yake.

  Sitaki kusikia wala kuambiwa kuwa Mkapa hakujua lolote jinsi Yona au Mramba walipokuwa wakitoa misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali na kupotezea Taifa mapato. Ni Rais gani hujui kuwa nchi yako inapoteza mali kiasi gani kutokana na uzembe. That means you're not a good Manager.

  Sitaki kuambiwa kuwa Mkapa alipokuwa anajizolea Kiwira alikuwa hajui kama anakiuka Katiba. CONSTITUION IS SUPREME LAW OF THE LAND. Hawezi kuachiwa afanye anavyotaka kinyume na Katiba. Alikula kiapo kuwa atailinda na kuitetea KATIBA ya JMT. Sasa iweje aachiwe wakati kaivunja katiba?

  Sitaki kuamini kuwa Bashe or Basha whatever anaweza kumpa Pressure Spika Sitta hasisikilize hoja ya kumchukulia hatua za kinidhamu Fisadi Mkapa. Haya Maji ya Bendera especially ya SISIEMU yasiwagawe watu kwenye makundi ya walio juu na chini ya sheria. Basha Bashe kumbuka kuwa uchaguzi Mkuu unakuja, na watanzania si wale wa miaka ya 1922 wa kudanganywa kwa sufuria la pilau.
  Kama wewe umeneemeka jitahidi kwa kutumia nafasi yako uneemeshe watanzania wengine ambao wanaishi kwa TAABU. Ufisadi wa Mkapa na fisadiz wenzake wamechangia kwa kiasi kikubwa Matazizo ya wananchi. Wanafunzi vyuo vikuu wanakosa udhamini, kisa serikali haina pesa, kila kitu serikali haina pesa. Lakini kwenye sherehe za kumfunda binti wa JK magari kibao ya serikali hayo Bagamoyo. Hizi pesa zinatoka wapi??

  Mkapa ni fisadi na ni busara afikishwe kwenye vyombo husika.
   
  Last edited: Jan 7, 2009
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu wangu Indume Yene, hapa tupo ukurasa mmoja hivi huyu jamaa Bashe kumbe naye ni wale wale? Ina maana huyu ni mtu wa Nchimbi/Lowassa nini?

  - Hawa watu atulie kama wananyolewa la Mkapa kutinga Kisutu halina mjadala tena it is about time, yaani uwapeleke rumande Yona, Mramba, na Mgonja bila ya Mkapa, hiyo itakua ni sheria au Ze-comedy?
   
 3. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mie siamini kama Mkapa alikuwa hajui kama anavunja sheria kujihusisha na biashara kwa njia moja au nyingine huku akiwa Ikulu. Kuna vitu vingine si lazima uende darasani ili kujua ni kosa. Mh. Prezidaa wa zamani alijua anakiuka miiko ya kiuadili kwa nini asiwajibishwe kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi? Bashe, Pilipili iliyoko shambani inakuwashia nini kama Fisadi Mkapa anafikishwa mbele ya sheria kwa makosa aliyotenda huku akijua ilikuwa makosa?
   
 4. G

  Giroy Member

  #4
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Indume heko kwa kuileta hiyo mapema kabla hakujakucha vizuri.Nataka kumkumbusha Huyo Bashe kuwa Mkapa hajapumzika aliyepumzika ni Nyerere.huyo Bwn bado tunabanana naye hapa duniani,yeye na timu wametutenda mabaya sana.inaelekea wewe bashe unatafuta umaarufu kwa hao, unafikiri watakupigia pande?kwa taarifa yako hata hao uliokuwa unawahutubia sio wote wanakuunga mkono.huo ndio mwanzo wa kupoteza hata huo umaarufu kiduchu ulionao.Inashangaza sana baadhi watu wanatafuta nafasi za kututumikia,lakini malengo yao kutuibia,badala ya kututumikia.Bashe huna mpango,kuna vitu vya maana vya kuongelea.
   
 5. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Adhaniaye amesimama aangalie hasije akaanguka.
   
 6. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo ndiyo utamu wa Maji ya Bendera ya SISIEMU. Matamshi ya Bashe sijui Basha hayatofautiana sana na Mbatia. Sioni faida ya kumtetea fisadi kwa Tanzania ya LEO. Watanzania tumeamka, sio wakati ule wa zidumu fikra za Mwenyekigoda.
   
 7. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hawezi pata fundisho toka kwa Kingunge Ngombare Mwiru. Dunia inapolizunguka jua yeye anadai jua ndo linazunguka dunia. Au pepo na mvua kali zinapokuwa zinavuma na kunyesha toka Magharibi kwenda Mashariki, yeye atadai hakuna pepo au mvua kabisa hadi aone mafuriko au miti mingi ikiwa imeng'oka. Sasa ndiyo huyo Bashe anayedai Mkapa ni msafi wakati uchafu wake uko nje nje. Hii ni kujitia AIBU mbele ya UMMA.
   
 8. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huo ni ushahidi kuwa ccm kuna jambo kati yao kwa wao kwa wao. Tusubiri tuone hatima hapahapa si mahala penginepo maaana mahakama za jf ziko tayari kurudia hukumu zake.
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mie nashukuru kijana Bashe kaonyesha rangi zake na atakuwa amesaidia sana watu wengine waliokuwa hawamfahamu, wakati wa uchaguzi ujao aombe tu na atapata majibu ya wanaichi
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Siku mkapa aklitinga mahakamani nchi itatikisika na nakuhakikishia halitakuja kutokea
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyu Bashe mimi binafsi Kitu kilichonipa wasiwasi tangu mwanzo juu ya uwezo wake na msimamo wake kisiasa ni pale alipoenguliwa kugombea uenyekiti wa UVCCM Tabora, lakini nikafikiri kwamba ni rafu tu za ccm wenyewe kwa wenyewe kwa maana wakati wa uchaguzi wa jumuiya za ccm huwa kuna rafu za hatari sana.
  Siku chache kabla ya kamati kuu ya ccm kukutana ili kupitisha majina ya wagombea nilikutana nae hoteli fulani jijini dar akiwa na wapambe wake,kwa kuwatazama tu wapambe wake miongoni mwao ni watu ambao tunafahamiana ndipo nikajua kuwa yuko kwenye kundi la ufisadi.Na ukifuatilia kwa makini utajua Bashe anawakilisha kundi gani ndani ya ccm, manake sasahivi ccm in makundi ya hatari sana, wanakulana nyama wao kwa wao!!!!!!
   
 12. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tuliwahi kudanganywa na SISIEMU kupitia watu mbalimbali pamoja na idara ya propaganda ya CCM kuwa kama Tanzania itakubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi nchi hii itageuka na kuwa kama Rwanda au Burundi. That's Bu.@&%t.
  Sasa hiyo Rwanda na Burundi iko wapi Tanzania tangu tukubali mfumo huo??????????

  Sasa naona hiyo SISIEMU imeanza kuwaadaa wananchi kupitia makada wake kuwa Fisadi Mkapa akifikishwa Mahakamani nchi italipuka. Watanzania ni waelewa sana, kuna nchi zingine wananchi wake hawana patience hata kidogo, hasira kibao. Na wameweza kuwafikisha fisadiz katika nchi zao na nchi zao hazijalipuka.
  Hakuna cha nchi kulipuka, sheria ichukuwe mkondo wake.
   
 13. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 875
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Acha ujinga wa kutisha watu, tena siyo KUTIKISIKA TU! acha ianguke kabisa, huwezi kaa kwenye nyumba imejaa nyufa, bora bomoa anza kujenga upya!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nina wasi wasi na uraia wa watu wanaomtetea mkapa?
  Manake wanaonyesha hawana ata chembe na mambo aliyoyafanya huyu mtu.
  Ivi unajua Kiwira ingekuwa properly privatised kwenye grid ya taifa tungekuwa na 100MW additional,na viwanda vyetu vya cement vingenunua mkaa wa Kiwira badala ya kuagiza nje.
  Imagine impact ya kiwila tuu kwenye uchumi ingekuwaje?Leave alone madudu mengine aliyoyafanya siwezi yachambua yote as naweza ambulia ULCERS BURE
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu TV.
  Inashangaza sana kuona watu wanatetea maovu tena hapa jamani. Hivi kweli Mkulu afanye kosa la kuvunja sheria asiwajibishwe kisa nchi itawaka moto. Acha iwake moto ili wajue kuwa hapaswi mtu kutenda upumbavu kwa sababu nchi itawaka moto. Lowassa na wengine waliwajibika ingawa hawajafikishwa kunakostahili. Siku zao haziko mbali.
  Fisadi ni fisadi tu hata kama awe Mkulu lazima sheria ichukuwe mkondo. NO ONE IS ABOVE THE LAW.
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hivi hadi leo hamjajua kuwa SISI M. imejaza watu wa aina ya Bashe?
  Kwa taarifa yenu wako wakina Bashe wengi tu! tena wako kila mahali wao wanajaribu kuona matumbo yao yanastawi kwa nguvu za wadanganyika.
  Tujaribu kuona ni kiasi gani twaweza kuwashughulikia watu wote wa aina ya Bashe maana wako wengi sana!
   
 17. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu MF nakubaliana nawe. Wako wengi tu wanaangalia upepo unaelekea wapi. Shughuli yao muhimu ni kupulizia at least matumbo yao yajae kwa migongo ya watu wengine. Watanzania tumechoka sasa, najua bado tuna safari ndefu ila tutafika tu.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,817
  Likes Received: 83,215
  Trophy Points: 280
  Bashe awashukia wanaomtuhumu Mkapa

  na Esther Mbussi
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, amesema watu wanaomhusisha Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na ubadhirifu wamefilisika kisiasa.

  Bashe alisema hayo wakati akifunga Mkutano wa Baraza kuu la vijana wa chama hicho, Wilaya ya Kinondoni, yaliko makao makuu ya umoja huo.

  Alisema Mkapa ameifanyia nchi mema mengi na kwamba hoja hizo zinazotolewa ni propaganda za wanasiasa wavivu wa kufikiri kutafuta umaarufu wa kisiasa.

  “Muacheni Mkapa apumzike, mengi ameyafanya kwa nchi hii watu wanalalamika tu kila kukicha, inashangaza kusikia kauli ya Spika kuwa atapokea hoja binafsi kuhusu Kumjadili Mkapa bungeni, hivi kuna mangapi ya msingi ya kuzumgumziwa bungeni badala ya kufikiria kumjadili Mkapa.

  Pia, Bashe alisema alikisikitikia vitendo vya wabunge kuacha kujadili hoja muhimu na zenye maslahi kwa taifa na badala yake wamebaki kutafuta nani tumshughulikie.

  Alisema atashangaa endapo bunge litamjamdili Mkapa kama ambavyo limefanya kwa miaka miwili kujadili hoja nyingi ambazo hazina maslahi ya taifa na kuongeza kuwa huo ni ushauri wa bure na si kwamba anaingilia kazi za bunge.

  Aidha, aliwataka vijana nchini kutokubali wala kushabikia sera na kauli zinazoibeza CCM kuwa haijafanya jambo lolote la maendeleo na kuwataka kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
 20. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu dogo hajatulia,anahitaji kupepewa
   
Loading...