Utamu wa katiba mpya, Wakenya tujifunze na yanayotendeka Zimbabwe

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,517
47,756
Wadau, Afrika ya leo sio kama ya zamani tena, haya mambo ya mitandao na utandawazi yameleta mwamko mpya, imefikia hatua marais ving'ang'anizi wakaanza kupata picha. Bila kuwa na katiba mpya na nzuri, ni rahisi sana kwa nchi kuingia kwenye hali kama tunayoiona Zimbabwe.

Pale rais anajiona kama mungu mtu, kwamba atafanya chochote na lolote muda autakao na siku aitakayo, kwamba anaweza kuamka na hiki leo, kingine kesho, hatabiriki, anaweza kumpokeza madaraka hata mkewe au mwanaye na kuwakandamiza upinzani na raia, na hawezi kuhojiwa maana anahakikisha hofu imetanda nchi yote. Sasa hali kama hiyo inasababisha wanajeshi wanaanza kumchunguza kwa mbali na siku ikifika, wanafanya yao maana na wao wanapitia hali ngumu ya maisha.
Marais kama Museveni wawe makini maana shoka kama hili linaweza kuwashukia, yeye tayari yupo kwenye hatua za kubadili katiba awe rais hadi siku ataaga dunia halafu ampokeze mwanaye.

Kwa kweli ndio tunaona utamu wa katiba mpya Kenya, kuna wale tunakerwa kuona rais wetu anaburuzwa buruzwa mahakamani na chaguzi zisizoisha, haswa kama mimi ambaye huwa namuunga mkono na kumpa kura, lakini hamna jinsi. Avumilie tu maana ndio ukomavu wa demokrasia na katiba inayofanya kazi. La sivyo, angeishia kuwa dikteta na kututumbukiza kwenye machafuko.

Binafsi mimi nimesema mara nyingi huu upumbavu singeuvumilia kama ningekua rais, lakini ndio hivyo tena, katiba hii tuliipigia upatu na lazima tuvumilie sote inapofanya kazi, ni nzuri na hamna siku itafika nijutie, hata kesho ikitangazwa tufanye uchaguzi tena, nitaamka mapema na kutumbukiza kura yangu, hata kama tutarudia mara mia moja, tumetoka mbali kwa kweli.

Watu wa Zimbabwe wawe tayari kwa muamko mpya baada ya uongozi kurudishwa kwa raia, warekebishe katiba yao na hakika watapaa kama tai. Mungu ibariki Afrika.
 
Ni kweli kuna vitu vinatia kinyaa sana, Africa tuna safari ndefu bado,
I love Katiba ya Kenya, ni nzuri. Lakini ukweli ni kuwa hamuendani Nayo,
Katiba kama hiyo haiwafai taifa maskini kama Kenya, na hata Tanzania.
Wewe ni shahidi, Hapa jamvini watu hudhihirisha uelewa mdogo sana wa Mambo, na kutumia emotions sana kuliko facts, the same applies to Kenya.
Huwezi implement Katiba kama ya Marekani Kenya ikiwa watu bado wana akili za Kuiba kura kama Uhuruto, tunahitaji walau watu wenye maisha yenye nafuu na waliostaarabika, kama vile watu wa Ulaya ama pengine RSA.
Tazama sasa mnashindwa hata kulipa deni la $700mn sababu mnafanya maandamano 24/7 na mnafanya uchaguzi miaka mitatu.
Katiba mpya Tanzania natamani tuipate labda 2030,
Kwa sasa hatuhitaji katiba, tunahitaji tujitume tupate maendeleo, hasa maendeleo ya WATU, kijamii na kiuchumi.
Tena ingekuwa ni mimi hata hii haki ya kumchagua rais haikufaa kila mtu aipate, at least Mtu awe na uelewa kidogo. Wengine waishie kuchagua Madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Haiwezekani mtu hajui kusoma na kuandika, au hata ukimhoji kwa nini unamchagua Fulani hawezi kudadavua, mtu amepewa kanga na kitenge anachagua rais, (Siwadharau ila tuwe tu wakweli)

Narudia, Katiba yenu haiwafai bado, nyie ni maskini na hampo civilized,
Watu wanashindwa pata hata mlo lakini wanafikiria siasa wakati wote,

Kuna mbunge alileta mswada kwetu wa kufanya uchaguzi mkuu baada ya miaka 7, naona ana point hapa, tupunguze kufikiria siasa na tujikite kwenye shughuli za uzalishaji na pia tuokoe pesa za uchaguzi kila baada ya miaka mitano,
Africa tunahitaji kwanza maendeleo, tupunguze kufikiria politics. Siasa tuzifanye baadae watu wetu wakiacha kubeba ndoo za maji vichwani.
But I stand with you, hawa kina KIKUYU+KALENJINI, M7, CCM, PK wanatakiwa kupata somo sasa, sio wao tu ndio wameumbwa kutawala milele.
 
Aaa wapi Museveni is smarter than many of the African Presidents! As we speak most of the guys here has fought with in the Bush r either Generals or Retired Generals with plummy pension or dead by contentious circumstances for those act rebellious or r in opposition.

In Uganda once a solduer u remain a soldier all ur life meaning committed n paying allegiance to the army. It will take long for anyone to attempt that in Uganda! As those r the only people can successfully topple him! Outsiders like the Konys have tried for years n ended being crushed!

As far as the political climate n discontent in the region region are concerned a coup can happen in Kenya easier than any other place! Don't forget that ur constitution is good but so far excessively violated. And if that happens in Kenya today, there will be massive support from inside n outside Kenya as Uhuruto are unpopular. Try to read intelligence news n see potential prone zones.

A reason why Uhuruto fear sending ur army in the street to quell any resistance as they know how u r polarised in tribal allegiance! Only ur Police n Recce is allowed as in Police Kalenjin dominate while Recce squad Kikuyus while in ur KDF the process to tribalize is still ongoing.
 
Naunga mkono hoja mkuu ila hapo kwenye ukalenjin na ukikuyu sijui kama mleta uzi atakuelewa maana ni Mkikuyu huyu.
 
Mkuu umetema madini ila nmekuelewa sana hasa hapo unapozungumzia haki ya kupiga kura......huo ni ukweli mtupu huwezi ukawa hujui kureason wala kwannk unafanya uchaguzi alafu unapiga kura!!! wengi hawatakuelewa ila umeongea ukweli mtupu hapa

Big up
 
Ni kweli kuna vitu vinatia kinyaa sana, Africa tuna safari ndefu bado,
I love Katiba ya Kenya, ni nzuri. Lakini ukweli ni kuwa hamuendani Nayo,
Katiba kama hiyo haiwafai taifa maskini kama Kenya, na hata Tanzania.
Wewe ni shahidi, Hapa jamvini watu hudhihirisha uelewa mdogo sana wa Mambo, na kutumia emotions sana kuliko facts, the same applies to Kenya.
Huwezi implement Katiba kama ya Marekani Kenya ikiwa watu bado wana akili za Kuiba kura kama Uhuruto, tunahitaji walau watu wenye maisha yenye nafuu na waliostaarabika, kama vile watu wa Ulaya ama pengine RSA.
Tazama sasa mnashindwa hata kulipa deni la $700mn sababu mnafanya maandamano 24/7 na mnafanya uchaguzi miaka mitatu.
Katiba mpya Tanzania natamani tuipate labda 2030,
Kwa sasa hatuhitaji katiba, tunahitaji tujitume tupate maendeleo, hasa maendeleo ya WATU, kijamii na kiuchumi.
Tena ingekuwa ni mimi hata hii haki ya kumchagua rais haikufaa kila mtu aipate, at least Mtu awe na uelewa kidogo. Wengine waishie kuchagua Madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Haiwezekani mtu hajui kusoma na kuandika, au hata ukimhoji kwa nini unamchagua Fulani hawezi kudadavua, mtu amepewa kanga na kitenge anachagua rais, (Siwadharau ila tuwe tu wakweli)

Narudia, Katiba yenu haiwafai bado, nyie ni maskini na hampo civilized,
Watu wanashindwa pata hata mlo lakini wanafikiria siasa wakati wote,

Kuna mbunge alileta mswada kwetu wa kufanya uchaguzi mkuu baada ya miaka 7, naona ana point hapa, tupunguze kufikiria siasa na tujikite kwenye shughuli za uzalishaji na pia tuokoe pesa za uchaguzi kila baada ya miaka mitano,
Africa tunahitaji kwanza maendeleo, tupunguze kufikiria politics. Siasa tuzifanye baadae watu wetu wakiacha kubeba ndoo za maji vichwani.
But I stand with you, hawa kina KIKUYU+KALENJINI, M7, CCM, PK wanatakiwa kupata somo sasa, sio wao tu ndio wameumbwa kutawala milele.
Mbona una akili nyingi kiasi hiki?, sio rahisi katika kizazi hiki kipya kupata watu wenye uwezo wa kufikiria kama wewe, japo sijui una umri gani, ila ninaweza kuhisi ulisoma kipindi cha Nyerere japo elimu ya msingi, hongera sana mkuu.
 
Ni kweli kuna vitu vinatia kinyaa sana, Africa tuna safari ndefu bado,
I love Katiba ya Kenya, ni nzuri. Lakini ukweli ni kuwa hamuendani Nayo,
Katiba kama hiyo haiwafai taifa maskini kama Kenya, na hata Tanzania.
Wewe ni shahidi, Hapa jamvini watu hudhihirisha uelewa mdogo sana wa Mambo, na kutumia emotions sana kuliko facts, the same applies to Kenya.
Huwezi implement Katiba kama ya Marekani Kenya ikiwa watu bado wana akili za Kuiba kura kama Uhuruto, tunahitaji walau watu wenye maisha yenye nafuu na waliostaarabika, kama vile watu wa Ulaya ama pengine RSA.
Tazama sasa mnashindwa hata kulipa deni la $700mn sababu mnafanya maandamano 24/7 na mnafanya uchaguzi miaka mitatu.
Katiba mpya Tanzania natamani tuipate labda 2030,
Kwa sasa hatuhitaji katiba, tunahitaji tujitume tupate maendeleo, hasa maendeleo ya WATU, kijamii na kiuchumi.
Tena ingekuwa ni mimi hata hii haki ya kumchagua rais haikufaa kila mtu aipate, at least Mtu awe na uelewa kidogo. Wengine waishie kuchagua Madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Haiwezekani mtu hajui kusoma na kuandika, au hata ukimhoji kwa nini unamchagua Fulani hawezi kudadavua, mtu amepewa kanga na kitenge anachagua rais, (Siwadharau ila tuwe tu wakweli)

Narudia, Katiba yenu haiwafai bado, nyie ni maskini na hampo civilized,
Watu wanashindwa pata hata mlo lakini wanafikiria siasa wakati wote,

Kuna mbunge alileta mswada kwetu wa kufanya uchaguzi mkuu baada ya miaka 7, naona ana point hapa, tupunguze kufikiria siasa na tujikite kwenye shughuli za uzalishaji na pia tuokoe pesa za uchaguzi kila baada ya miaka mitano,
Africa tunahitaji kwanza maendeleo, tupunguze kufikiria politics. Siasa tuzifanye baadae watu wetu wakiacha kubeba ndoo za maji vichwani.
But I stand with you, hawa kina KIKUYU+KALENJINI, M7, CCM, PK wanatakiwa kupata somo sasa, sio wao tu ndio wameumbwa kutawala milele.
I couldn't agree more mkuu. Huwa natamani Rais awe anachaguliwa labda na wabunge au na kundi fulani la wawakilishi
 
Aaa wapi Museveni is smarter than many of the African Presidents! As we speak most of the guys here has fought with in the Bush r either Generals or Retired Generals with plummy pension or dead by contentious circumstances for those act rebellious or r in opposition.

In Uganda once a solduer u remain a soldier all ur life meaning committed n paying allegiance to the army. It will take long for anyone to attempt that in Uganda! As those r the only people can successfully topple him! Outsiders like the Konys have tried for years n ended being crushed!

As far as the political climate n discontent in the region region are concerned a coup can happen in Kenya easier than any other place! Don't forget that ur constitution is good but so far excessively violated. And if that happens in Kenya today, there will be massive support from inside n outside Kenya as Uhuruto are unpopular. Try to read intelligence news n see potential prone zones.

A reason why Uhuruto fear sending ur army in the street to quell any resistance as they know how u r polarised in tribal allegiance! Only ur Police n Recce is allowed as in Police Kalenjin dominate while Recce squad Kikuyus while in ur KDF the process to tribalize is still ongoing.
Hivi ukiondoa habari ya uchaguzi kupingwa mahakamani, wananchi wa kawaida wamefaidikaje na hiyo katiba mpya kama bado haki za msingi zinazidi kukosekana?
Police Will Not Allow NASA Supporters Into JKIA
 
Ni kweli kuna vitu vinatia kinyaa sana, Africa tuna safari ndefu bado...

Tena ingekuwa ni mimi hata hii haki ya kumchagua rais haikufaa kila mtu aipate, at least Mtu awe na uelewa kidogo. Wengine waishie kuchagua Madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Haiwezekani mtu hajui kusoma na kuandika, au hata ukimhoji kwa nini unamchagua Fulani hawezi kudadavua, mtu amepewa kanga na kitenge anachagua rais, (Siwadharau ila tuwe tu wakweli)...
Congrats... Ingawa nina shaka kama wengi wanaweza kukuelewa...
 
Wadau, Afrika ya leo sio kama ya zamani tena, haya mambo ya mitandao na utandawazi yameleta mwamko mpya, imefikia hatua marais ving'ang'anizi wakaanza kupata picha. Bila kuwa na katiba mpya na nzuri, ni rahisi sana kwa nchi kuingia kwenye hali kama tunayoiona Zimbabwe.

Pale rais anajiona kama mungu mtu, kwamba atafanya chochote na lolote muda autakao na siku aitakayo, kwamba anaweza kuamka na hiki leo, kingine kesho, hatabiriki, anaweza kumpokeza madaraka hata mkewe au mwanaye na kuwakandamiza upinzani na raia, na hawezi kuhojiwa maana anahakikisha hofu imetanda nchi yote. Sasa hali kama hiyo inasababisha wanajeshi wanaanza kumchunguza kwa mbali na siku ikifika, wanafanya yao maana na wao wanapitia hali ngumu ya maisha.
Marais kama Museveni wawe makini maana shoka kama hili linaweza kuwashukia, yeye tayari yupo kwenye hatua za kubadili katiba awe rais hadi siku ataaga dunia halafu ampokeze mwanaye.

Kwa kweli ndio tunaona utamu wa katiba mpya Kenya, kuna wale tunakerwa kuona rais wetu anaburuzwa buruzwa mahakamani na chaguzi zisizoisha, haswa kama mimi ambaye huwa namuunga mkono na kumpa kura, lakini hamna jinsi. Avumilie tu maana ndio ukomavu wa demokrasia na katiba inayofanya kazi. La sivyo, angeishia kuwa dikteta na kututumbukiza kwenye machafuko.

Binafsi mimi nimesema mara nyingi huu upumbavu singeuvumilia kama ningekua rais, lakini ndio hivyo tena, katiba hii tuliipigia upatu na lazima tuvumilie sote inapofanya kazi, ni nzuri na hamna siku itafika nijutie, hata kesho ikitangazwa tufanye uchaguzi tena, nitaamka mapema na kutumbukiza kura yangu, hata kama tutarudia mara mia moja, tumetoka mbali kwa kweli.

Watu wa Zimbabwe wawe tayari kwa muamko mpya baada ya uongozi kurudishwa kwa raia, warekebishe katiba yao na hakika watapaa kama tai. Mungu ibariki Afrika.
Upanga Mkali Upanga Mkali
Katiba mpya lakini akili za watu ni zilezile primitive, hakuna la maana litakalopatikana, msikilize huyu mama ndiyo utanielewa vizuri
 
Ni kweli kuna vitu vinatia kinyaa sana, Africa tuna safari ndefu bado,
I love Katiba ya Kenya, ni nzuri. Lakini ukweli ni kuwa hamuendani Nayo,
Katiba kama hiyo haiwafai taifa maskini kama Kenya, na hata Tanzania.
Wewe ni shahidi, Hapa jamvini watu hudhihirisha uelewa mdogo sana wa Mambo, na kutumia emotions sana kuliko facts, the same applies to Kenya.
Huwezi implement Katiba kama ya Marekani Kenya ikiwa watu bado wana akili za Kuiba kura kama Uhuruto, tunahitaji walau watu wenye maisha yenye nafuu na waliostaarabika, kama vile watu wa Ulaya ama pengine RSA.
Tazama sasa mnashindwa hata kulipa deni la $700mn sababu mnafanya maandamano 24/7 na mnafanya uchaguzi miaka mitatu.
Katiba mpya Tanzania natamani tuipate labda 2030,
Kwa sasa hatuhitaji katiba, tunahitaji tujitume tupate maendeleo, hasa maendeleo ya WATU, kijamii na kiuchumi.
Tena ingekuwa ni mimi hata hii haki ya kumchagua rais haikufaa kila mtu aipate, at least Mtu awe na uelewa kidogo. Wengine waishie kuchagua Madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Haiwezekani mtu hajui kusoma na kuandika, au hata ukimhoji kwa nini unamchagua Fulani hawezi kudadavua, mtu amepewa kanga na kitenge anachagua rais, (Siwadharau ila tuwe tu wakweli)

Narudia, Katiba yenu haiwafai bado, nyie ni maskini na hampo civilized,
Watu wanashindwa pata hata mlo lakini wanafikiria siasa wakati wote,

Kuna mbunge alileta mswada kwetu wa kufanya uchaguzi mkuu baada ya miaka 7, naona ana point hapa, tupunguze kufikiria siasa na tujikite kwenye shughuli za uzalishaji na pia tuokoe pesa za uchaguzi kila baada ya miaka mitano,
Africa tunahitaji kwanza maendeleo, tupunguze kufikiria politics. Siasa tuzifanye baadae watu wetu wakiacha kubeba ndoo za maji vichwani.
But I stand with you, hawa kina KIKUYU+KALENJINI, M7, CCM, PK wanatakiwa kupata somo sasa, sio wao tu ndio wameumbwa kutawala milele.

Naheshimu maoni yako na naomba ukubali kutokukubiliana, mara nyingi huwa sijadili na wewe chochote maana nimekuzoea kama mzee wa kubeza beza asiyeandika chochote cha msingi. Leo nafurahi umejitutumua na kuandika aya kadhaa, ina maana upo tayari kujadili mada, tatizo nilibanwa na kazi sana leo.

Mchango wako huu wa leo naona umekua wimbo mtamu sana kwa makada wa CCM maana wao kila wakiskia katiba mpya huishia kuweweseka.

Waliobuni mifumo ya katiba dunia hii walikua na akili sana, maana kuna baadhi ya jamii bila kuendeshwa kikatiba wanaishia kuzunguka mbuyu. Husasan jamii zetu za Kiafrika, ni kweli tumeiga wenzetu kwa kila kitu ikiwemo jinsi tunakula na hata tunavyochamba lakini kwa kuiga katiba ndio kitu kizuri tulichofanya maana Mwafrika bila sheria huwa kama mnyama.

Kwa kifupi, katiba yetu mpya imetufaidi sana, nchi yetu tunaona maendeleo yakifika pembe zote za nchi, gatuzi na mikoa yote ikijiamulia vipau mbele vyao bila kupangiwa na Nairobi kama tunavyoona kwenu uwanja mkubwa wa ndege usiokua na maana unajengwa Chato wakati watu wa hapo Chato vipau mbele vyao ni tofauti sana na huo uwanja, pia tunashuhudia jinsi dola yetu inavydhibitiwa na kukwepa uongozi wa kiimla ambao tunauona kwenye nchi zote zilizotuzunguka.

Hayo ya kusema kwamba watu wanapiga kura bila kujua maana yake, sio sababu tosha yakutufanya tutelekeze mfumo huu wa katiba unaotutoa kwa kasi. Taratibu wananchi wanaendelea kupata elimu na kuanza kuhisi umuhimu wa kura zao, hamna kitu kizuri kama kutikisa dola, kuweka rais kwenye mkao wa kuogopa kutupwa nje muda wowote, anaishia kutenda na kufanya kazi kwa bidii, sio kama marais ambao wana uhakika wa kuwa madarakani hadi kifo chao.
Suala la watu kupiga kura bila kuzingatia vigezo vyenye tija ni jambo la kawaida hata kwenye nchi zilizokomaa kidemokrasia kama Marekani, kule unakuta kuna mamilioni ya Wamarekani ambao huegemea kwenye milengo yao na huwambii kitu, kama yeye Democrat hajali hata kama mtateua nguruwe igombee urais kwa tikiti ya chama hicho, na taswira ndio hiyo hiyo kwa Republicans.
 
MK254 Nakubaliana na wewe kwa hili. Ila kuna mambo kama mawili naomba nikusahihishe ili hii hoja yako ikae sawa.

Mosi ni kuhusu hii unayoiita KATIBA MPYA. Ni dhahili kuwa kitu kizuri zaidi kwenye katiba yenu sio UPYA wake bali ni UBORA wake. Kama katiba yenu isingekuwa na ubora mnaoutaka hata kama ingekuwa mpya kila siku, bado isingeweza kutatua changamoto zenu. Lakini pale katiba inapokuwa bora, hata iishe miaka mingapi bado itaendelea kuwafaa na kusaidia kutatua changamoto. Katiba yenu imekamilika tangu 2010 kama sikosei, huo upya ushaisha. Hivyo kwenye katiba yenu, kizuri ni Katiba bora na sio katiba mpya.

Suala la pili ni hili ulilosema kuwa linawakera kuona rais wenu akiburuzwa mahakamani kila baada ya uchaguzi, hasa ninyi mafuasi wake. Labda nikukumbushe kuwa, Uhuru anaburuzwa mahakamani kama mgombea wa urais na si kama rais. Mamlaka yake kama rais hayajaguswa, ila kwa sababu anazo kofia zote mbili kwa wakati mmoja basi hana budi kutekeleza wajibu wake. Na hata akiwa huko mahakamani anaitwa mgombea sio rais.

Kuweni tu wapole wakati demokrasia inachukua nafasi yake, huenda hii ikawapandisha mwakani kwenye democracy index.
 
Asante kwa mchango wako chanya usiokua na ule ushabiki wa kawaida.
Katiba yetu bado tunaiona mpya maana humo kuna vinpengele ambavyo havijakamilika kwenye utekelezaji wake, fahamu utekelezaji wa katiba ni hatua za taratibu ambazo huchukua miaka maana ni kitu kinabadilisha mfumo wa maisha, kinabadilisha mazoea yote, rais anaishia kushangaa jinsi mikwara na matamko yake yasiyokua na tija yanavyopingwa na kukataliwa kisheria.

Hatukutengeza katiba ilmradi ionekane tu mpya, bali ulikua mchakato mzima, kumbuka tulipiga chini kura ya maoni ya mwanzo pale ambapo dola ilikua imethubutu kubadilisha vinpengele fulani vya rasimu ya katiba iliyopendekezwa mwanzo, na kuchakachua, tukaishia kuboresha na kuhakikisha imetulia na hatimaye kuipitisha kama nchi.

Binafsi kama binadamu mwenye hisia ninakerwa na huku kumburuza rais wangu mahakamani, sio jambo geni kwa shabiki yeyote kukerwa pale anapoona ushindi wao ukiishia mahakamani. Lakini pia nikiangalia shilingi kwa upande wa pili, napata afueni kwamba wenye mashaka na uchaguzi wameishia mahakamani badala ya maamuzi ya mtutu wa bunduki au mikimbio ya kila siku yenye umwagikaji wa damu. Hapo ndio utamu wa katiba mpya na bora unadhihirika, nchi inabaki imesimama wima, wataalam wa sheria wanaingia ulingoni kutoana jasho humo hadi kieleweke.

Tungekua tunategemea katiba ya zamani, nina uhakika kufikia sasa lazima nchi ingekua imeingia kwenye machafuko makubwa, watu kuuana na kuharibiana majengo na mali. Kiasi kwamba hata jeshi lingekua limeingilia na kuchukua usukani, bora hivi tulivyo ambapo mambo yanaishia uraiani na kuwekana sawa.

Changamoto zipo, sio kwamba nasema katiba mpya ndio suluhu kwa kila kitu maana mwisho wa siku katiba ipo kwajili ya binadamu na sio kinyume, hivyo safari ni ndefu lakini tunakokwenda tutafika tu. Leo hii mimi binafsi sina hofu hata nani awe rais maana nina uhakika hatutaongozwa kiimla, katiba hairuhusu nguvu zote kuwa kwa mtu mmoja, ila taasisi huru ndio zinashirikiana katika shughuli za kila siku.
 
Naheshimu maoni yako na naomba ukubali kutokukubiliana, mara nyingi huwa sijadili na wewe chochote maana nimekuzoea kama mzee wa kubeza beza asiyeandika chochote cha msingi. Leo nafurahi umejitutumua na kuandika aya kadhaa, ina maana upo tayari kujadili mada, tatizo nilibanwa na kazi sana leo.

Mchango wako huu wa leo naona umekua wimbo mtamu sana kwa makada wa CCM maana wao kila wakiskia katiba mpya huishia kuweweseka.

Waliobuni mifumo ya katiba dunia hii walikua na akili sana, maana kuna baadhi ya jamii bila kuendeshwa kikatiba wanaishia kuzunguka mbuyu. Husasan jamii zetu za Kiafrika, ni kweli tumeiga wenzetu kwa kila kitu ikiwemo jinsi tunakula na hata tunavyochamba lakini kwa kuiga katiba ndio kitu kizuri tulichofanya maana Mwafrika bila sheria huwa kama mnyama.

Kwa kifupi, katiba yetu mpya imetufaidi sana, nchi yetu tunaona maendeleo yakifika pembe zote za nchi, gatuzi na mikoa yote ikijiamulia vipau mbele vyao bila kupangiwa na Nairobi kama tunavyoona kwenu uwanja mkubwa wa ndege usiokua na maana unajengwa Chato wakati watu wa hapo Chato vipau mbele vyao ni tofauti sana na huo uwanja, pia tunashuhudia jinsi dola yetu inavydhibitiwa na kukwepa uongozi wa kiimla ambao tunauona kwenye nchi zote zilizotuzunguka.

Hayo ya kusema kwamba watu wanapiga kura bila kujua maana yake, sio sababu tosha yakutufanya tutelekeze mfumo huu wa katiba unaotutoa kwa kasi. Taratibu wananchi wanaendelea kupata elimu na kuanza kuhisi umuhimu wa kura zao, hamna kitu kizuri kama kutikisa dola, kuweka rais kwenye mkao wa kuogopa kutupwa nje muda wowote, anaishia kutenda na kufanya kazi kwa bidii, sio kama marais ambao wana uhakika wa kuwa madarakani hadi kifo chao.
Suala la watu kupiga kura bila kuzingatia vigezo vyenye tija ni jambo la kawaida hata kwenye nchi zilizokomaa kidemokrasia kama Marekani, kule unakuta kuna mamilioni ya Wamarekani ambao huegemea kwenye milengo yao na huwambii kitu, kama yeye Democrat hajali hata kama mtateua nguruwe igombee urais kwa tikiti ya chama hicho, na taswira ndio hiyo hiyo kwa Republicans.
Umejitahidi kuandika vizuri, ila ninamaswali machache
1)paragraph ya mwisho umezungumzia kuhusu suala la watu kupiga kura bila kuangalia vigezo, umesema hilo ni jambo la kawaida kwasababu hata USA watu wamegawanyika hivyo, wale ambao ni wapenzi wa Republican, kamwe hawawezi kuchagua Democrat na kinyume chake, kwanini hilo likitendeka USA unaona ni sawa ni jambo la kawaida, lakini likifanyika Afrika hasa hasa Tanzania unahisi sio sawa na kusema watu wananunuliwa?
2)Kwanini wakenya kila kitu lazima mtolee mfano wa USA, mbona hamuwaigi USA kuachana na rushwa na ukabila?
3)Mbona wewe unaandika maelezo marefu mno(insha), ila wakiandika wengine unapiga kelele?
 
Hehehe!! Leo umevaa fulana tofauti, baada ya kutiririka humu na bandiko kadhaa ambazo hata sijui zinahusiana vipi na mada husika, hizo links zako huwa unarusha rusha kwenye kila mada hamna mtu huziafuata maana humu tunajadili na kuwekana sawa sio ushabiki wa kurusha rusha links.

Sababu za mimi kutaja kwamba Marekani kuna mamilioni ya watu hupiga kura bila kujali vigezo wala nini ilmradi mgombea ni wa chama chao, ilikua kumjibu yule game over alipodai kwamba katiba yetu haitufai kwasababu wengi wetu hatuzingatii vigezo wala kudadavua sababu za kuwapigia kura viongozi, na eti katiba kama hii inawafaa hao wa Ulaya, ndio ikabidi nimkumbushie kwamba na huko Ulaya binguni anaowahusudu wana hulka kama hizo pia, kuna mamilioni wenye 'ukabila' wa kiaina likija suala la upigaji kura.

Huwa hawajali mgombea anayo mapungufu gani, ilmradi anagombea kwa kutumia chama chao, hata kama mropokwaji asiyetumia akili na mwenye matusi, hata kama haongei sera wala nini, wanampa kura tu, tena wanaamka mapema na kupanga foleni kutwa ili wampigie kura kisa ni wa chama chao. Sikusema ni jambo nzuri, ila nimesema ni jambo la kawaida na linatokea katika kila nchi duniani, hata huko kwa mabwana zetu, na lipo hata Tanzania, kwanza huko kwenu ndio usipime.

Nchi zetu zote hizi tumeiga mabwana zetu kwa asilimia 98%, yaani kila kitu, hapo ulipo nina uhakika kila kilichokuzunguka umeiga na sio cha asili ya Kiafrika. Huo unafiki wa kujiona nyie ndio hamjaiga chochote na kuelekeza kidole Kenya ndio hunichosha na kuwapuuza.

La kuandiika insha, fahamu kwamba mimi ni msomaji sana, tena nasoma vitabu vingi na aina ya taaluma yangu inahusu kusoma na kutafiti kila siku, na mara nyingi ukiandika insha zako humu, kuna zile zenye tija huwa nazisoma hadi mwisho, lakini nikiona unaandika upupu wa kupindisha pindisha kinafiki, huwa hata sisomi zaidi ya aya moja, napita kimya maana humu kila mmoja wetu yupo huru kuchagua nini cha kusoma au kipi cha kupuuza, nina uhakika sio kila mtu husoma ninachoandika.
 
Jambo moja ninaloliona na ninadhani ni sababu kubwa ya Kenya kutokuwa na amani, umoja na utengemano wa kitaifa ni tabia ya wakenya wengi ukiwemo wewe kujiona wanajua kila kitu na kutotaka au kutoweza kukubali pale anapokosolewa, kubali ama ukatae, hii ndiyo tabia inayowasumbua wakenya karibu wote, kila mmoja kujiona yupo correct na kutotaka kusikuliza mawazo ya mtu mwengine, wewe hili tatizo linakusumbua sana.

Katika kumjibu kwako gameover ulishaanza kwa kusema, ulipanga kutomjibu hoja zake, lakini kwa kuona watu wamempongeza ukaona ujibu ili kuonyesha kwamba alichosema sio sawa, kama kawaida yenu mlivyo.

Kuhusu kuchagua watu kiushabiki, ulitolea mfano USA, na kuandika neno kwamba ni hali ya kawaida kwasababu hata USA wanafanya hivyo, lengo ni kuonyesha kwamba hilo sio tatizo, ungeona ni tatizo usingetumia neno ni kawaida, badala yake ungesema ni tatizo linalokumba nchi nyingi hata hizo zilizoendelea, usijaribu kupindisha maneno baada ya kujikuta umebanwa, kama kawaida ya wakenya hampendi kukubali pale mnapofanya makosa, nchi inasambaratika kwa sababu ya kila mtu kujiona ni mtimilifu

Kuhusu kuandika insha, tatizo ni lile lile la wakenya, kitu kikifanywa na mtu mwengine utakikashifu na kukisema vibaya, ila mkikifanya ninyi, mtakipaka lipsticks na wanja ili kipendeze, insha ni insha, haijalishi umeandika wewe au ameandika mtu mwengine, mnatabia hiyo sana, ikiwezekana anzeni kubadilika otherwise nchi yenu itakatika vipande vipande, then muanze kuwalaumu Raila na Uhuru kumbe ninyi wenyewe tabia zenu ni hovyo
Umejitahidi kuandika vizuri, ila ninamaswali machache
1)paragraph ya mwisho umezungumzia kuhusu suala la watu kupiga kura bila kuangalia vigezo, umesema hilo ni jambo la kawaida kwasababu hata USA watu wamegawanyika hivyo, wale ambao ni wapenzi wa Republican, kamwe hawawezi kuchagua Democrat na kinyume chake, kwanini hilo likitendeka USA unaona ni sawa ni jambo la kawaida, lakini likifanyika Afrika hasa hasa Tanzania unahisi sio sawa na kusema watu wananunuliwa?
2)Kwanini wakenya kila kitu lazima mtolee mfano wa USA, mbona hamuwaigi USA kuachana na rushwa na ukabila?
3)Mbona wewe unaandika maelezo marefu mno(insha), ila wakiandika wengine unapiga kelele?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom