MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,752
- 48,345
Wadau, Afrika ya leo sio kama ya zamani tena, haya mambo ya mitandao na utandawazi yameleta mwamko mpya, imefikia hatua marais ving'ang'anizi wakaanza kupata picha. Bila kuwa na katiba mpya na nzuri, ni rahisi sana kwa nchi kuingia kwenye hali kama tunayoiona Zimbabwe.
Pale rais anajiona kama mungu mtu, kwamba atafanya chochote na lolote muda autakao na siku aitakayo, kwamba anaweza kuamka na hiki leo, kingine kesho, hatabiriki, anaweza kumpokeza madaraka hata mkewe au mwanaye na kuwakandamiza upinzani na raia, na hawezi kuhojiwa maana anahakikisha hofu imetanda nchi yote. Sasa hali kama hiyo inasababisha wanajeshi wanaanza kumchunguza kwa mbali na siku ikifika, wanafanya yao maana na wao wanapitia hali ngumu ya maisha.
Marais kama Museveni wawe makini maana shoka kama hili linaweza kuwashukia, yeye tayari yupo kwenye hatua za kubadili katiba awe rais hadi siku ataaga dunia halafu ampokeze mwanaye.
Kwa kweli ndio tunaona utamu wa katiba mpya Kenya, kuna wale tunakerwa kuona rais wetu anaburuzwa buruzwa mahakamani na chaguzi zisizoisha, haswa kama mimi ambaye huwa namuunga mkono na kumpa kura, lakini hamna jinsi. Avumilie tu maana ndio ukomavu wa demokrasia na katiba inayofanya kazi. La sivyo, angeishia kuwa dikteta na kututumbukiza kwenye machafuko.
Binafsi mimi nimesema mara nyingi huu upumbavu singeuvumilia kama ningekua rais, lakini ndio hivyo tena, katiba hii tuliipigia upatu na lazima tuvumilie sote inapofanya kazi, ni nzuri na hamna siku itafika nijutie, hata kesho ikitangazwa tufanye uchaguzi tena, nitaamka mapema na kutumbukiza kura yangu, hata kama tutarudia mara mia moja, tumetoka mbali kwa kweli.
Watu wa Zimbabwe wawe tayari kwa muamko mpya baada ya uongozi kurudishwa kwa raia, warekebishe katiba yao na hakika watapaa kama tai. Mungu ibariki Afrika.