Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 360
Heroin, ambayo pia inajulikana pia kwa majina ya Brown, Smack and Skag kwa UK, ni dawa ambayo hutengenezwa kutoka kwenye mmea uitwao opium poppy. Hutumika kama kama dawa ya maumivu. Mitaani huuzwa kwenye vijipakti vidogo ikiwa katika hali ya ungaunga wa brauni.
Watumiaji wa heroin huivuta kama sigara au bangi kwa kutumia pipes au yale makaratasi ya jikoni ya silver, wengine hujidunga kwa kutumia sindano. Wengi wanaovuta huapa kwamba hawatathubutu kujidunga lakini mara nyingi nao huingia kwenye mchezo wa sindano kwa kuwa ndio njia bomba zaidi kwa kupata steam ya chapchap na yenye kukupa thamani halisi ya fedha zako.
Kwa wanaoanza kutumia heroin kwa mara ya kwanza husikia joto, hupata muwasho wa ngozi na kutapika kwa sana. Wengi husema inahitaji kutumia mara kadhaa kabla ya kuanza kuipenda na kunogewa. Kama nilivyosema hapo awali, heroin ni painkiller, it kills both physical and emotional pain.
Watumiaji husema kwamba unajiskia kama katoto kalikofunikwa kwenye ‘baby shoo' au pamba, unasahau matatizo yako yote na kujiona kama Bill Gates. Hii ndio sababu kubwa kwanini watu wengi wanaotumia heroin ni wale wenye matatizo makubwa na uhaba mkubwa wa furaha kwenye maisha yao.
Kama unatumia heroin mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa ukawa addicted au teja' kama wengi tunavyosema. Ukishakuwa teja inamaanisha utahitaji kutumia kila siku vinginevyo utakua physically ill kutokana na symptoms za kuwithdraw, na hii ndio inawafanya wengi washindwe kuacha, na pia ukizingatia kwamba watumiaji wengi hawana mengi ya kuwafanya wawe na furaha kwenye maisha yao zaidi ya kutumia huo unga.
Ukishajikuta kwenye hali hii, inakua ukiamka asubuhi unakuwa unahitaji kutumia na mawazo yako yote ni juu ya namna ambavyo utapata pesa ili uweze kununua ;unga' wa siku hiyo. Na inakuwa tabu sana kwa watumiaji sugu kwa kuwa wanahitaji kiwango kikubwa zaidi ili wapate steam, hii inamaanisha pesa zaidi na kwa kuwa wengi hawana ajira au means yoyote ya kipato, wanaishia kuingia kwenye uhalifu.
Heroin inaua kama mtumiaji atatumia kiwango kikuwa ambacho mwili wake hauwezi kukihandle, hii inaitwa Overdose na mara nyingi hutokea kama mtumiaji ata inject, na kuinject kuna ambatana na hatari za maambukizi ya magonjwa kama hep C, hep B na HIV kama watumiaji watashare sindano.
Utumiaji wa madawa ya kulevya umewasababishia watu wengi matatizo makubwa, wengine wamepoteza maisha yao kabisa, njia pekee na salama ya kuyaepuka yote haya ni simple- USITUMIE. Kama unatumia heroin, jitahidi usi inject- vuta tu, its safer na usisahau kuongea na wataalamu , kama wapo