Utamu ndani ya CCM ..... Masilingi, DC wavaana Muleba

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Masilingi, DC wavaana Muleba

Na Muhibu Said

MVUTANO umeibuka kati ya Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi na Mkuu wa Wilaya ya Muleba (DC) hiyo, Deusdedit Mtambalike kuhusiana na michango ya ujenzi wa sekondari wilayani humo.

Hali hiyo imedhihirika baada ya Masilingi kuibuka na kumtuhumu mkuu huyo wa wilaya na kiongozi mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kwamba, wamekuwa wakimtukana kwa sababu anapinga njia haramu zinazotumiwa na baadhi ya watendaji wa kata na vijiji kukusanya michango hiyo kutoka kwa wananchi.

Masilingi anadai kuwa katika kukusanya michango hiyo, watendaji hao wamekuwa wakiwatesa, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wananchi, wakiwamo wazee, wanawake na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo, wakati Masilingi akitoa madai hayo, DC amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa Masilingi ndiye amekuwa akiwatukana viongozi wilayani humo, akiwamo yeye (Mtambalike) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, E. Basaya, kutokana na msimamo wao wa kuwahimiza wananchi kutoa michango hiyo.

Katika taarifa yake aliyoituma kwa gazeti hili jana, Masilingi alidai kuwa hivi karibuni, Mtambalike akiongozana na kiongozi huyo wa CCM, bila kuwasiliana naye kwa simu au maandishi, walikwenda katika kata ya Nshamba alikozaliwa na kuhutubia kamati ya maendeleo ya kata iliyoshirikisha viongozi mbalimbali, wakiwamo wa madhehebu ya dini na kumkashifu na kudhalilisha kiongozi mmoja wa dini aliyehudhuria mkutano huo.

"Mkuu wa wilaya aliwaambia wachange Sh 10,000 kwa kichwa na alifoka akisema mbunge Wilson Masilingi anawadanganya halafu anarudi Dar es Salaam. Hivyo, waachane na siasa za mbunge la sivyo atakuja na picha ya Rais Jakaya Kikwete na Hakimu na kuwafunga," anadai Masilingi.

Masilingi anadai kuwa katika ziara yake aliyotembelea tarafa za Kimwani, Muleba na Nshamba zilizoko jimboni mwake, alisikiliza na kushuhudia vitendo vya udhalilishaji, unyanyasaji na mateso vilivyofanywa dhidi ya wananchi ambao walimuomba awachukulie hatua za kisheria viongozi na watendaji, akiwamo mkuu wa wilaya na madiwani na watendaji wote wa kata na vijiji wanaohusika na vitendo hivyo vya jinai.

"Wananchi wanasema wamechoka kuvumilia kwamba wamemtaarifu mbunge, polisi, lakini viongozi na watendaji hao hawakamatwi na kuchukuliwa hatua za kisheria. Wananchi wameahidi kuwa wapo tayari kutoa ushahidi kwa mamlaka na mahakama wakitakiwa kufanya hivyo. Mimi naamini mamlaka za juu za utawala zinaweza kuwaondolea wananchi wa Muleba Kusini kero hizo," anadai Masilingi.

Anadai yeye binafsi, tangu mwanzoni mwa mwaku huu, amekuwa akifikisha kero hizo kwa uongozi wa wilaya wa chama na serikali na hata kushauri katika michango wake bungeni na pia Juni, mwaka huu, alitoa taarifa ya maandishi kwa uongozi wa wilaya wa chama na serikali yenye uchambuzi wa katiba, sheria na miongozo ya viongozi wa juu, akiwamo Rais Kikwete.

Kwa upande wake, Mtambalike ambaye alizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, alisema azimio la michango hiyo lilipitishwa na vikao vya halmashauri na kwamba, anashangazwa na Masilingi kuona akilalamikia pembeni wakati yeye ni mbunge na diwani ambaye alipaswa kufanya hivyo kwenye vikao vya halmashauri.

Alisema Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Muleba, ilikutana Desemba 4, mwaka huu, lakini Masilingi hakushiriki na wajumbe wakampongeza yeye (Mtambalike) pamoja na viongozi wengine wa halmashauri.

Alisema madai ya kuwakamata, kuwatesa na kuwadhalilisha wananchi na kumtukana Masilingi, ni uzushi.

"Yeye (Masilingi) ndiye anayetukana sana kila anapoendesha vikao. Anatukana viongozi wa wilaya kwamba, ni wapumbavu, anamkashifu Mwenyekiti wa Halmashauri na anapita akitamba kuwa lazima ataondoka hapa wilayani," alidai Mtambalike.

Source: Mwananchi
 
Kama Masilingi angekuwa Mbunge wa kutoka upinzani, basi CCM na serikali ungewasikia wakisema wapinzani ndo wanazuia maendeleo ya wananchi au wanawazuia wananchi wasichangie shughuli za maendeleo. Swala siyo kugoma kuchangia, swala ni njia zipi zinatumika kuwachangisha. Zama za kulazimishana zilishapitwa na wakati, hizi ni zama za ukweli na uwazi, waeleze faida na hasara na uwahakikishie kwamba michango yao itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Tatizo la sehemu nyingi ni kwamba michango inachwangwa na inaishia kwenye mifuko ya watu au kwenye ujenzi wa mahekalu ya watu badala ya kujenga shule/zahanati/barabara au kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo.

Masilingi kaa mkao wa wa kueleweka, ukilegalega 2010 utaisikia bombani unaweza kudondoshwa kwenye kura za maoni na huo ndiyo ukawa mwisho wako kisiasa. Hao wanaolazimisha michango ni wateule wa Rais na utendaji wao wa kazi unapimwa na Rais, utendaji wako (Masilingi) unapimwa na wapiga kura wako, ukicheza tu wamekuondoa maana hutakuwa na jipya once ukitaka kurudi Bungeni 2010!
 
Habari hizi nazisikia kwa wingi sana siku hizi watu kuvaana majukwaani tu. kuna hatua zozote zinazochukuliwa kufuatilia haya na kama ni ya ukweli nini kinafanyika? hakuna haja kabisa ya kupigishana kelele majukwaani watu wawaone wanafanya kazi lakini hakuna lolote wananchi tunaendelea kuumia
 
Anacho kisema Masilini ni tonoradi moja ya yale yanayo tendeka huko vijijini! Watu wanaumizwa kweli kwa kutishiwa kwa nguvu kwamba wasipotoa michango waziri mkuu atawafukuza vijijini!. yaani kuna watu hadi wanahama miji kwa ajili ya michango hii.

Imagine kila kichwa sh elfu 10! kwa maisha ya kijijini, ni hela nyingi mno, kumwambia, baba 10 alfu, mama 10 elfu, na kama kuna kijana mkubwa kwenye familia naye elfu 10!

Sipingi kwamba wasichangie lakini si kwa njia hii, na kinacho uma zaidi, wakati wananchi wananyanyaswa wachange hivi, tunashuhudia serikali inavo fuja mapesa kibao kwa ziara zisizo isha, magari ya kifahari ambayo yangetumika kufanya kazi hizi! Tunashuhudia inavo wakingia kifua wezi wote wa mapesa ya serikali kina manji na bilion, achilia mbali hayo ya Bot, na shangazi zake kina Richmonduli!

Kwa kweli inakera sana!
 
Hivi kwanza kabla ya kuwachangisha hao wanakijiji,Serikali imehakikisha imeweka mazingira gani mazuri kwa wananchi hao kujiingizia kipato kitakachowawezesha kuchangia kwa lazima hizo 10000/-?Au ndo mambo ya kujiju?
 
Huyu DC anayesema "anawahimiza" wananchi itabidi atueleze anawahimizaje?

Kodi si wanalipa? Hii michango mingine si ya hiyari? Kuhimizana gani sas huko mpaka watu wanashikana mashati?
 
Ni uonevu tu wa viongozi wa ngazi za chini na kati! Masuala haya ya kuchangishana kwa nguvu ni ujinga mtupu! Kuchanga maana yake ni hiari siyo lazima. Na kama they can't meet their target basi wajue wananchi wao hawajajengewa mazingira mazuri ya kuweza kuchanga. Mi naona haya masuala ya michango ya kujenga shule is exaggerated. Wameona huko Lake Region na Northern Zone wamejenga mashule that way sasa wanataka kulazimisha kila mkoa na wilaya wajenge mashule. Alafu tunasikia hakuna walimu! Mh!
 
Ngoma imerejea tena
Habari hizi nazisikia kwa wingi sana siku hizi watu kuvaana majukwaani tu. kuna hatua zozote zinazochukuliwa kufuatilia haya na kama ni ya ukweli nini kinafanyika? hakuna haja kabisa ya kupigishana kelele majukwaani watu wawaone wanafanya kazi lakini hakuna lolote wananchi tunaendelea kuumia
 
Back
Top Bottom