Utamu: Nadharia ya mapenzi na suala zima la upendo

Msonjo

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
1,308
2,224
Habari zenu wadau.

Unajua katika mapenzi na sualazima la upendo, kuna tofauti kubwa sana jinsi mtu anavyo mpenda mtu mmoja ukilinganisha na anavyo mpenda mwingine.

Unaweza ukamwambia mama yako nakupenda sana.
Na ukwambia mkeo/mpenzi wako pia nakupenda sana.

Lakini upendo wako kwa mama yako sio sawa na upendo wako kwa mkeo/mpenzi wako, na vilevile upendo wako kwa kaka/dada yako sio sawa na upendo wako kwa rafiki yako

Sasa katika nadharia ambazo nimewahi kukutananazo ni nadaharia ya kuufananisha "upendo ni kama utamu katika vitu".

Asali tamu, tende tamu, embe tamu, tikiti tamu, nanasi tamu, chungwa tamu, parachichi tamu na tango tamu n.k.

Lakini utamu wa asali sio sawa na utamu wa tende. Embe pia tamu lakini utamu wake sio sawa na utamu nanasi. Chungwa nalo tamu lakini utamu wake sio sawa na utamu tikiti. Parachichi na lenyewe tamu lakini utamu wake sio sawa na utamu wa tango.

Na hivyo hivyo katika suala la mapenzi(upendo) baina ya watu.

Hebu tueleze upendo wako kwa nani ni kama utamu katika nini?

Binafsi upendo wangu kwa mama yangu ni kama utamu katika asali.

Funguka.
 
Binafsi kila kitu kizuri kipo ndani ya upendo, hakuna cha kulinganisha/kufananisha na upendo.
Mkuu sijalinganisha upendo na utamu, Ila namna watu tunavyo pendana huwa sio sawa.

Ni kama utamu wa vitu haufanani ingawa tunasema vyote vitamu.

Au wewe upendo wako kwa watu ni sawa? ukizingatia na nafasi zao kwako.
 
mm nafikiri kuna upendo wa Mama ni kama chumvi unaponya kila kitu matumizi yake hayafananishwi na chochote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom