Utamu na uchungu wa ndoa za mitala

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,936
2,000
Babu yangu alikuwa na wake watatu kupitia dini yetu ya asili inayoruhusu wake kulingana na uwezo wa kipesa na kingono, nikiwa mdogo nilibahatika kuwaona maisha yao, babu yangu alikuwa ana ukwasi kwa level za kijijini kila mke alimjengea mji wake na duka nje cha ajabu tuliishi kwa amani sana wajukuu tulikuwa tukiamua kulala kwa bibi mkubwa wote tunalala huko.

Mimi nilitokana na mke wa tatu ambaye babu alimpenda zaidi nadhani ila kimatumizi alikuwa hawagawi kabisa ukiacha maduka aliyoyaacha chini ya uangalizi wao alikuwa ana fiat mbili za kusomba mazao kwenda Dar akirudi na mikate, nanasi, samli, vitenge (havikuwepo mkoani kwetu) anagawa kwa usawa, aliweza kuwalea watoto kupendana wakawa wajasiliamali wazuri na 70% ni matycoon alifariki kabla ya wakeze akiacha mali bila migogoro kwani aliandika usia kila mke na mji wake na watoto wake.

Mpaka leo tunaishi kwa upendo na yeye ndo nguzo yetu, aidha wake wawili wa mwisho aliwakuta wameshazaa bila ndoa na aliwaoa na maisha yangu yote sikuwahi jua baba zangu wengine si wanae hadi namiaka 20, sasa cha ajabu wakati anafariki aliacha usia huu kwa baba zetu juu ya maisha ya ndoa:

1. Alisema katika dunia hakuna mtu muhimu kuliko mke/mumeo.
2.Hakuna zawadi unayoweza mpa mke kuzidi kuwapenda na kuwalea vyema watoto wake.
3.KAMWE USIOE MKE ZAIDI YA MMOJA, AKARUDIA KWA KILUGHA ''SIVO SIVO NDEPELILE''

Sasa wakuu huwa najiuliza kuna nini kwenye ndoa za mitara alichokiona babu?
 
mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,916
2,000
Alichokiona babu yako nafikiri hakuwa akipata mda wa kutosha wa kupumzika,angalia wiki ina siku saba na yeye ana wake watatu hivyo kama kila mke anahitaji game angalau mara mbili kwa wiki mzee alikuwa anapiga game sita takatifu kwa juma moja,mara mwezi?,mara mwaka?

Ukiwa nje huyaoni, ndio maana mzee kashauri kwa kuwa alikuwa ndani na kayaona haya.
 
Mkuuu nimerekebisha ,ila umenichekesha kuwa mzee alitaabika
 
mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,916
2,000
Mkuuu nimerekebisha ,ila umenichekesha kuwa mzee alitaabika
Nakupongeza kwa kukubali ushauri,mwingine angeshanilowesha kwa mapovu.

Mzee alikuwa anapiga hat-trik mbili kila juma,sio kazi ndogo ujue, maana ukiacha madhara yake wote tunajua.
 
kimyama nje

JF-Expert Member
May 28, 2017
361
500
USIA kama huo nami nilipewa nisioe Mke zaidi ya mmoja nakama imetokea niwe na hakika Huyo wakwanza nimemuacha Na kumpa haki yake Na wanae. Hadi Leo huwa najiuliza kunanini?
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,606
2,000
Si ajabu kila nyumba a kufika kulikuwa na mashtaka hivyo halali mpaka ayatatue
 
kimyama nje

JF-Expert Member
May 28, 2017
361
500
Nakupongeza kwa kukubali ushauri,mwingine angeshanilowesha kwa mapovu.

Mzee alikuwa anapiga hat-trik mbili kila juma,sio kazi ndogo ujue, maana ukiacha madhara yake wote tunajua.
Hao wazee wa zamani sina hakika kama walikua Na nguvu hizo. Kuna mzee huwa napiganae story anasema jando la zamani alikua anaonekana mwanaume jandoni zinafungwa Nazi mbili unasimamisha na kuzibeba kwa kichwa cha mbo### nikaona nikajalibu kubeba hata nusu sukali daaa wazee wengine waongo sana hao wanawake walikua wanavumilia pengine imechangia kifochake mapema zaidi
 
The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,936
2,000
USIA kama huo nami nilipewa nisioe Mke zaidi ya mmoja nakama imetokea niwe na hakika Huyo wakwanza nimemuacha Na kumpa haki yake Na wanae. Hadi Leo huwa najiuliza kunanini?
Inaelekea kwenye mitala kuna moto mkali sana wazee walituonea huruma
 
Gyole

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
6,919
2,000
Ni ngumu kuwaridhisha wanawake wote kwa wakati mmoja, ni ngumu kutatua matatizo yao wote kwa wakati mmoja, ni ngumu kuwapenda wote kwa wakati mmoja, na ni ngumu kuwalinda wote kwa wakati mmoja, stress stress stress kila siku yaani
 
The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,936
2,000
Nakupongeza kwa kukubali ushauri,mwingine angeshanilowesha kwa mapovu.

Mzee alikuwa anapiga hat-trik mbili kila juma,sio kazi ndogo ujue, maana ukiacha madhara yake wote tunajua.
inawezekana sababu ya kufa kwa babu yako ni idadi ya hao wake
Hhahaha sidhani alikufa na miaka 94 umri wa kuishi mwanadamu kikristo ni 85
 
The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,936
2,000
Na hiyo 9 iliyoongezeka ilikuaje? Au alihamia upande wa pili?
Biblia inasema wenye nguvu watazidi kidogo kwa majaaliwa ya mungu yaani mkristo ukifika 85 unatakiwa ufanye misa ya shukrani na useme ''sasa bwana waweza mchukua mtumishi wako ...''
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom