Utamu na Faida za Tende kwenye mwili wa binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamu na Faida za Tende kwenye mwili wa binadamu

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tende mbali ya utamu wake zina faida nyingi sana mwilini
  Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana mwezi wa ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Zijue faida zake. Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee.

  Kwa leo tutazielezea baadhi ya faida za tende mwilini:

  1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

  2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

  3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

  4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

  5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

  6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

  7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

  8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

  9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

  10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
  Haya Waislam Wanaofunga wakati wa kufuturu kuleni sana Tende.
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ama kwa hakika tende ni kiboko aisee! Yaani ni mambo yoote! Mie mwezi huu ninalo boksi kabsa la kilo mbili hilo ni kutafuna tu hadi mwezi uishe na hali kadhalika ntajiwekea utamaduni wa kununua kidogo hata baada ya Mwezi Mtukufu... Akhsante sana Ndugu kwa kutukumbusha na kutufunza jambo la kheri Mola akubariki na akupe umri....
  Ramadhan Maqbuul...
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Zifuatazo Ni Baadhi Ya Faida Za Tende Mwilini:

  1. Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tuhmbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

  2. Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

  3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya mapenzi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

  4. Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

  5. Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

  6. Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

  7. Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

  8. Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

  9. Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

  10. Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Tende ina faida nyingi tena inafaa hata kwa siku za kawaida uwe unakula kila siku japo Tende punje 7 tu zatosha hicho nikiwango kidogo kwa kila siku yafaa uwe unakula hiyo Tende utaona Afya yako inakwenda vizuri. Ukila Tende kilo moja faida yake kama mtu aliye kula nyama ya Ng'ombe kilo moja.
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa taarifa hii muhimu.
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu kwa elimu hii ila kwa hapo kwenye red nayapata wapi?
   
 7. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ya kweli haya?
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  zinapatikana wapi kirahisi kwa hapa dar tuanze kuzitumia kwa wingi zaidi kwani................
   
 9. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Nina uhakika zitashusha soko la zile dawa za ndugu zangu wa kaskazini na wale waganga wa kinaigeria kwa asilimia 70
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sikujua tende kama ni dili ivi naonaga wanauza barabarani nikafikiri ni usanii tu
   
 11. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tende ni hatari kwa afya binadamu kama zitakuwa zinatumiwa mara kwa mara.tenda zinasababisha ugonjwa wa kisukari,upungufu wa nguvu za kiume na kusababisha mwili na ubongo uchovu.
   
 12. K

  Kabogo Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona inakinzana na maada ya hapo juu.Ebu acheni kutuchanganya
   
 13. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  we ni mganga wa kienyeji, au mchawi, kama si hivyo utakuwa jini. usilete uganga wako wa kienyeji hapa. tuloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi, kwani maziwa ni ya mbuzi tu...ya kondoo, ya ng'ombe, ya ngamia je? yana tofauti gani?
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  ona sasa unapewa tiba!.. angalia contents za tende scientifically sure zina virutubisho vinavyosaidia. naona ushaingilia mambo ya mashetani! ... hahaha au unataka kutoa misukule 100 NA WEWE humu JF!:becky::becky: ELIMU KWELI MUHIMU
   
 15. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Manufaa haya ni kwa Tende za Uarabuni tu ambazo zimechakatwa (Processed) au hata hizi za kwetu mbivu tu?
   
 16. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  brother nice post
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  tende ni Tende hata zikiwa ni za kibongo bora ziwe ni tende zina faida nyingi sana .
   
 18. m

  mashamsham New Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona unatutisha tumfate nani ? halafu maradhi ya kisukari si yanasababishwa na sukari ya artificial si natural mi sijuwi lakini hebu nifahamishe kwa hisani yako
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Thanx mpendwa ...
   
 20. p

  pierre JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba kama kuna daktari anayeweza kuchangia mada hii ajitokeze maana kuna wengine wakishaona kuna masharti kidogo ya kufanya anafirkiri ni mambo ya mashetani.Kweli wazungu wamefanikiwa kukupotosha,mbona ingekuwa ni kutoka ulaya usingeuliza maswali hayo?????
   
Loading...