Utamtambuaje?

HILLARY MUSHI

Member
Nov 24, 2012
10
3
Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta wa kuishi nae, ila kila ninaye kutana nae na kuongea nae, mimi kwa upande wangu naona kama wanakuwa wanaigiza, sasa sijui nitamtambuaje anaye kuwa wangu wa kudumu...wadau mniambie
 
Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta wa kuishi nae ila kila ninaye kutana nae na kuongea nae, mimi kwa upande wangu naona kama wanakuwa wanaigiza sasa sijui nitamtambuaje kwamba anafaa kuwa wangu wa kudumu nae...wadau mniambie

Pole.Msubiri tu atakuja.Utamtambua kwa vigezo ulivyojiwekea.Zaidi sana endelea kuomba
 
Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta wa kuishi nae, ila kila ninaye kutana nae na kuongea nae, mimi kwa upande wangu naona kama wanakuwa wanaigiza, sasa sijui nitamtambuaje anaye kuwa wangu wa kudumu...wadau mniambie

Ngoja nikupe siri...
Siku hiizi hawa viumbe ni pesa tu ndio inawatuliza kama huna hela basi uwe na dalili zote za kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mswano yaani mchakarikaji hapo ndipo utawapata wa kutosha ushindwe mwenyewe..

Huwa wanabadilika kama vinyonga, waweza muona anaigiza kumbe anataka kujua thamani yako.

hakuna mwanamke anayependa maisha ya shida usawa huu kwanza maisha yenyewe yashakuwa mafupi.
 
nafuata imani za kale za wahenga dada yangu, kwani nimekosea kuuliza ?

Hujakosea na mimi sikukosea kumwambia aombe..Kwani wewe huwa huwaombi wahenga??? au imani yako ni legelege kwa wahenga??Kila mtu anaomba kutegemea na imani yake..
 
Ngoja nikupe siri...
Siku hiizi hawa viumbe ni pesa tu ndio inawatuliza kama huna hela basi uwe na dalili zote za kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mswano yaani mchakarikaji hapo ndipo utawapata wa kutosha ushindwe mwenyewe..

Huwa wanabadilika kama vinyonga, waweza muona anaigiza kumbe anataka kujua thamani yako.

hakuna mwanamke anayependa maisha ya shida usawa huu kwanza maisha yenyewe yashakuwa mafupi.

Believe me my dear Mtambuzi,,pesa sio kila kitu..Siku hizi kuna idadi kubwa ya wadada wamesoma,wana hela,wametulia na wanahitaji heshima tu ya jina la mrs... bhaaaas...
 
Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta wa kuishi nae, ila kila ninaye kutana nae na kuongea nae, mimi kwa upande wangu naona kama wanakuwa wanaigiza, sasa sijui nitamtambuaje anaye kuwa wangu wa kudumu...wadau mniambie

Kwa upande wangu naona kam vile wanawake unaowapata wako sababu ya kitu fulani
ambacho kinawafanya wakishakipata waamue kukuacha solemba.

Cha kufanya ni kujitahidi kuweka vigezo vyako ambavyo vitakupelekea uweze kumpata
unayemhitaji awe ako wa maisha,

Kwangu mimi vigezo nilivyoviweka kwa mwanamke nimtakae ni kama vifuatavyo:
1. Awe mpole na mwenye kauli nzuri ambazo zitatufanya tuishi kwa amani.
2. Awe mchapakazi na wala asiwe mvivu/mtegeaji kazi.
3. Awe ananisaidia ushauri pale ninapomshirikisha.
4. Awe mwenye malengo mazuri na mapenz yetu.
5. Awe mcheshi na asiyependa kukasirika mara kwa mara.
6. Sura, umbo, maalio hivyo ni nyongeza tu.
 
Pwenti
 
Uaminifu je?
 
kaka ni pesa tu ndo inafanya atulie hata hayo mambo mswano atajua tu pindi utakapokuwa umeshakuwa nazo kidogo. hebu jiulize kama kijana aliyemaliza shule yupo kwenye soko la ajira anaachwa kwa sababu hana mshiko kuna future tena hapo
 
Believe me my dear Mtambuzi,,pesa sio kila kitu..Siku hizi kuna idadi kubwa ya wadada wamesoma,wana hela,wametulia na wanahitaji heshima tu ya jina la mrs... bhaaaas...

Hapo labda mwanaume akubali kuwa HOUSE BOY......!
Wanawake wa siku hizi wanatofauti kubwa sana na wale wa zamani kama vile mbingu na ardhi, zamani mahusiano na ndoa vilishikwa na mila na desturi, kila mwanandoa nyakati hizo alikuwa anajua wajibu wake na kusimama katika nafasi yake, lakini siku hizi kuna mambo mengi yamechangia kutuvuruga,

Hili dubwana linaloitwa TV limekuja na elimu mpya, zinaitwa TAMTHILIA, vijana wa leo wamejisahau kuwa hayo ni maigizo wanataka kujaribu kila wanachokiona. wazazi nao wamshindwa kusimama katika nafasi zao, watoto wanasoma boarding tangu msingi mapaka chuo kikuu, akirudi nyumbani anafanya kile anachokiamini kwamba ni sahihi, wazee hawana nafasi tena maana kijana amekua na anajua wajibu wake.

Kaazi kweli kweli............!
 
Kipi wanachofanya ambacho kimekuwezesha kuhitimisha kwamba wanafanya maigizo?

Ni kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta wa kuishi nae, ila kila ninaye kutana nae na kuongea nae, mimi kwa upande wangu naona kama wanakuwa wanaigiza, sasa sijui nitamtambuaje anaye kuwa wangu wa kudumu...wadau mniambie
 
Kipi wanachofanya ambacho kimekuwezesha kuhitimisha kwamba wanafanya maigizo?

Hili nalo neno, maana tunazunguka tu kumbe hata hao tunaomwelekeza akaona nao wanaigiza.

Ila mapenzi ya sikuhizi kweli vijana tumepotea, yaani mara formular mara vigezo mara sijui nini......
Haya yote yanahusikaje na mapenzi mbona nayo ni maigizo tu
 
Uigizaji wao upo kwenye inshu mbali mbali mfano mtu tayari umemweleza yote kama kuishi nae lakini utakuta/nashindwa kuelewa kwamba hajiamini au ndo anajaribisha ili aone kama upo siriaz mara akutafutie rafiki yake wa kike akutege,akuzushi vitu vya ajabu ajabu ilimradi tu ukasirike so sijiu ndo nini?
 
Hivi ukiitwa 'mrs mtambuzi, au mrs tanmo, au mrs asprin ndo heshima? Yaani heshima ni kuitwa mrs naniliu?
Ndio maana watu wanakesha kwenye maombi na wengine kwa waganga...Hata Bible imedhibitisha hilo..kuwa kutakuja kipindi wanawake saba watamuendea mwanaume mmoja na kuomba angalau waitwe kwa jina lake tu na mambo mengine juu yao (nimesahau kifungu)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom