Utamtambuaje Mchumba Wako Anayesoma Chuo Anakupenda Kwa Dhati na Mwenye Malengo Ya Maisha na Wewe?!

Nitajulikana

JF-Expert Member
Sep 20, 2017
328
355
Ndugu zangu,kwanza nawasalimia nyote nikiwa na matumaini yangu kwamba mu wazima wa afya.

Nimekuja na mada hii nikiomba msaada kwenu.Mimi sijaoa na nimekuwa nikitafta mwanamke wa kuoa kwa mda mrefu.
Nashindwa kuiita bahati nzuri au mbaya kwani kila mwanamke ambaye nimekuwa nikiweka malengo naye nimekuwa nikikuta ni mwanachuo tena chuo kikuu.

Nimeisha kutana na wanawake watatu na nimeshindwa kudumu nao kwani siwaamini wanawake wanachuo katika kupenda,kulinda,kutunza kuvumilia mapenzi na hasa (long distance love)

Kilichonisukuma kuomba elimu na ushauri huu ni miezi miwili iliyopita nilikutana na binti.Kama kawaida tulianzisha urafiki na urafiki huu ulidumu bila kila mtu kumwambia mwenzake anajishughulisha na mini.

Jana jioni ndio tukaamua kufungukiana kuhusu maisha yetu ya kila siku na shughuli zetu.Katika hali isiyokuwa ya kawaida yule binti akaniambia ni Mwanachuo mwaka wa pili!! Nilistuka sana na nikaona km akili yangu inaendelea kuvurugwa.

Sasa ndugu zangu naomba elimu na ushauri kwa hili nifanyeje? Niendelee kuwa nae? Ananipenda kweli? Hataniharibia feature yangu njiani?!!.
Msaada wenu jaman mwenzenu hili jambo linanisumbua sana maana hii too much!!!!
 
Wana kuja walio bobea... nacho jua kwa haraka haraka na chuo alipo ana boyfriend anae mpiga show. Wewe utasaidia kumpa hela yakula boyfriend wa chuo atakusaidia kumridhisha si uko mbali bwana mpaka muonane ni hadi chuo kifungwe au uingie gharama zaku msafirisha kutoka chuo kukufata kila unapo miss mchezo, wakati mwingine itakubidi wewe ue unamfata chuoni kwa kusafiri...
 
Ushauri wangu hapo ni kuwa mstahimilivu kuwa nae,Punguza wivu katika kumfuatilia hasahasa simu
 
Kumbe mpaka awe chuo!!

Hamna kipimo cha upendo,huwa tunahisi tuu . Moyo wa mtu kichaka
 
Samahan kwa kutoka nje ya mada wakuu

hv ilikua ukishapiga kura ile 2010 tunachanganya kwenye boks moja au ni tofauti, mana nahsi nilikosea boksi. Si kwa vyuma hv.
 
Ndugu zangu,kwanza nawasalimia nyote nikiwa na matumaini yangu kwamba mu wazima wa afya.
Nimekuja na mada hii nikiomba msaada kwenu.Mimi sijaoa na nimekuwa nikitafta mwanamke wa kuoa kwa mda mrefu.
Nashindwa kuiita bahati nzuri au mbaya kwani kila mwanamke ambaye nimekuwa nikiweka malengo naye nimekuwa nikikuta ni mwanachuo tena chuo kikuu.
Nimeisha kutana na wanawake watatu na nimeshindwa kudumu nao kwani siwaamini wanawake wanachuo katika kupenda,kulinda,kutunza kuvumilia mapenzi na hasa (long distance love)
Kilichonisukuma kuomba elimu na ushauri huu ni miezi miwili iliyopita nilikutana na binti.Kama kawaida tulianzisha urafiki na urafiki huu ulidumu bila kila mtu kumwambia mwenzake anajishughulisha na mini.
Jana jioni ndio tukaamua kufungukiana kuhusu maisha yetu ya kila siku na shughuli zetu.Katika hali isiyokuwa ya kawaida yule binti akaniambia ni Mwanachuo mwaka wa pili!!
Nilistuka sana na nikaona km akili yangu inaendelea kuvurugwa.
Sasa ndugu zangu naomba elimu na ushauri kwa hili nifanyeje? Niendelee kuwa nae? Ananipenda kweli? Hataniharibia feature yangu njiani?!!.
Msaada wenu jaman mwenzenu hili jambo linanisumbua sana maana hii too much!!!!
Kuna kipimo kinaitwa pesa...kitumie utajua tu hata kama udhati hautoonekana komaa tu maana muhimu ni mapenzi hiyo dhati ni nyongeza!
 
Hamna kipimo. Asikudanganye mtu.

Anaweza akaonekana deep sana, na mkakaa zaidi ya miaka miwili, ila when all hell break loose, trust me, you wont see it coming.

Wenye kuweza haya mambo ni waliozoea kubet tu.
 
Samahan kwa kutoka nje ya mada wakuu

hv ilikua ukishapiga kura ile 2010 tunachanganya kwenye boks moja au ni tofauti, mana nahsi nilikosea boksi. Si kwa vyuma hv.
Siku nyingine utakumbuka tu.wacha vyuma vikazw
 
Samahan kwa kutoka nje ya mada wakuu

hv ilikua ukishapiga kura ile 2010 tunachanganya kwenye boks moja au ni tofauti, mana nahsi nilikosea boksi. Si kwa vyuma hv.
ndio unaamka Saa hizi na bado
 
ni bora usichunguze hivyo vya kama wapendwa kweli kwanza miezi miwili ni muda mdogo jaribu kuenjoy the moment kama anakupenda na ilipangwa mfikie ndoa mtafika tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom