Utamkumbuka huyu kwa wimbo wake upo hasa?

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,053
653
Leo ilikuwa siku ya huzuni kwa kumuaga mwanamziki aliyekuwa kipenzi cha wengi hasa katika nyimbo zake zenye ujumbe mzito! hakika Mungu amlaze mahali pema peponi Amen!

je wewe kama Mpenzi wa mziki bila kujali umri wako unaweza kusema ni wimbo gani ambao ukiusikia utamkumbuka daima Remmy Ongala?

Katka nyombo zake ambazo mimi sitaweza kumsahau ni kama ule wa Kifo hakina huruma,Ndumila kuwili na nyingine nyingi.

Wewe je unaweza tupa ni wimbo gani na sababu za kupenda nyimbo hizo?
 
Kati ya nyimbo zake ni hizi hapa
1. kifo hakina huruma
2.Bibi wa mwenzio
3.Musiki
4.sauti ya mnyonge
5.siku ya kufa
6.Mnyonge hana haki
7.harusi ya mwanza
8.Nalilia mtoto
9.Ndumilia kuwili
10.Tanzania
11.Tembea ujionee
12.Mariam wangu
13.Kalola
14.Kipendacho roho

Kati ya hizo hapo utakubaliana na mimi nyimbo zake zilikuwa nzuri!
 
Wiki jana, room mate wangu wa shuleni, wakati nikiwa Mazengo amefariki dunia. Hizi habari nilizipata juzi. Jamaa alikuwa ni member wa JF pia ila jina lake la hapa nitaliweka kapuni.

Ningelipenda Remmy Ongalla na kijana wangu Herman Emanuel Nzowa niombe kwa Mungu awape mapumziko mema, Amen.

Wimbo wangu kwao wote ni:

Wimbo wangu niupendao: Ndumila kuwili
http://www.youtube.com/watch?v=-wggnVn2RWk
 
Last edited by a moderator:
Kuna ule mwingine mashairi yake yanaimbwa Nasikitiika eeeh dunia imani imekwisha watu wameota mapembe, kula kwa tabu, kulala kwa tabu kuvaa kwa tabu kila kitu kwa shida. Kauimba miaka ya themanini na sita na saba wakati huo akiwa na mtindo wa BONGO BEATS
 
Sikonge naungana na wewe kumtakia pumziko la milele marehemu Nzowa na DR REMMY
 
Kibao 'Machozi ya samaki' huwa sichoki kukisikiliza.
Pia ule wimbo wa 'Mambo kwa sox' nao sitousahau.
 
Wiki jana, room mate wangu wa shuleni, wakati nikiwa Mazengo amefariki dunia. Hizi habari nilizipata juzi. Jamaa alikuwa ni member wa JF pia ila jina lake la hapa nitaliweka kapuni.

Ningelipenda Remmy Ongalla na kijana wangu Herman Emanuel Nzowa niombe kwa Mungu awape mapumziko mema, Amen.

Wimbo wangu kwao wote ni:

Wimbo wangu niupendao: Ndumila kuwili
YouTube - Remmy Ongala & Orchestra Super Matimila ~ Ndumila Kuwili

sikonge samahani kama ntakukwaza... hivi mwana JF akishafariki nivibaya ku-reveal ID yake?
 
Last edited by a moderator:
Sifahamu kama ni vibaya. Ila maadamu mwenyewe wakati akiwa hai hakutaka kufanya hivyo, ni bora kuacha kama ilivyo.

Unajua wakati mwingine unaweza kuwa unaandika UPUUZI kwenye majukwaa ya Wapwa.

Sasa wakija kufahamu watoto wako/Wajukuu na ndugu kwa ujumla jina lako, inakuwa Kasheshe.

Ndiyo maana ni bora jina likaendelezwa kufichwa. Ya JF na yabaki JF. Kama aliandika cha maana basi watu wataendelea ku-copy au ku-quote maneno yake Marehemu.

Labda kuna haja watu wawe wanaandika STATEMENT kuwa, wakifariki basi Jina lake halisi litangazwe.

roja that mkuu, ila kule kwa wapwa ni sawa na sehemu yoyote ya rika, huo uppuzi upo tu, hata jeshini, hostel, bar, mikutanoni nk... kwahiyo usiwe mnyonge wala kutia shaka ya huko kwani kama ulisoma boarding basi waijua beto

i hope he was a great JF contributor mkuu
 
kumbe Acid we ni mwanajeshi??!
Upo kambi gani?
 
Acid,

Huwa natokea huko kwa Wapwa mara moja moja. Ila siyo member mzuri sana hasa sasa hivi nilivyo na mawazo mengi sana. Ila nikiwa nimetulia au kuchoka, basi huwa naingia kwa Wapwa kuburudika.

Wengine hata ninawasiliana nao kwa simu. Hivyo si kuwa siwapendi au kuwaonea aibu ila huko ni kama JKT. Yaliyotokea JKT wengi wetu hawatataka ndugu zao wayafahamu. Mie nilikuwa MWIZI mzuri sana wa chakula. Sasa hii si sifa ya kujivunia na mengine mengi.

Tupo pamoja sana kwa Wapwa ingawa huwa nachangia kwa nadra sana.

YES: Kama unavyoona hapo juu, Mazengo Sec enzi hizo ilikuwa shule ya WANAUME tu.
Mkitaka totoz basi nendeni Msalato, hapo mnafanya Chagulaga na Bihawana Sec.
roja that mkuu, ila kule kwa wapwa ni sawa na sehemu yoyote ya rika, huo uppuzi upo tu, hata jeshini, hostel, bar, mikutanoni nk... kwahiyo usiwe mnyonge wala kutia shaka ya huko kwani kama ulisoma boarding basi waijua beto

i hope he was a great JF contributor mkuu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom