Utamchukia Zitto Kabwe lakini akiongea anamwaga sumu tupu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Donald Trump ni mwanasiasa anayefanana sana na dunia ya sasa ya vitu vinavyopatikana haraka haraka. Trump ni mwanasiasa asiyetabirika, muda wowote ule anaharibu hali ya hewa kwa uropokaji wake. Ni mjanja mwenye kujua kuwa watu wa kizazi cha kisasa hawataki sana mambo ya takwimu, hawataki sana kusikia sera mbalimbali na jinsi zitakavyoweza kutekelezeka.

Hillary Clinton ni tofauti kabisa, yeye ni kama alivyo mumewe (Bill Clinton), yupo tayari kumwaga sera kwa kuongea kwa muda mrefu bila ya kujali kama wanaomsikiliza wameanza kusinzia au kupiga miayo.

Zitto Kabwe ni aina ya Hillary na Bill Clinton. Haendani sana na kizazi chake, ambacho siku zote kinataka mambo ya haraka haraka, kinataka kusikia jinsi gani leo inavyoweza kuwa bora zaidi.

Unaweza kumchukia Zitto Kabwe labda kwa sababu ya ile intellectual Superiority Complex lakini jamaa kila akifungua mdomo bungeni anamwaga sumu nzito. Tena anazidi kukomaa katika ule utulivu wa kuchukua muda anaopewa kwa ajili ya kujenga hoja.

Katika dunia ambayo Hillary na Bill Clinton wanaingia kwenye miaka ya sabini, wanaibuka wanasiasa vijana wenye kusimamia katika mantiki (substance) badala ya mihemko ya muda mfupi.

Zitto Kabwe asichoke kusoma vitabu vingi kutoka kwa watu walioelimika, tabia hiyo inamsaidia katika kujenga hoja nzito.

Donald Trump anawafaa hawa waliozaliwa miaka ya karibuni wenye kupenda vituko na vichekesho lakini mantiki ikiwa zero.

Keep it up Zitto Kabwe.
 
Hata Elton John waweza kumchukia lakini akisimama jukwaani utamkubali tu. Ndivyo walivyo watu wa sura mbili....hear him sing

 
Yote uliyosema ni kweli sana, lakini hoja yako ni nini hasa?

Hoja yangu ni kuwafikishia ujumbe wanasiasa, kwamba wajitahidi muda mwingi waongee vitu vyenye mantiki.

Mipasho, kejeli na matusi sio silaha za kutegemewa na mwanasiasa mwenye kutaka kuacha legacy.

Mwalimu JKN anakumbukwa kwa sababu ya uwezo wa kujenga hoja. Zitto anazidi kukomaa katika uwezo wa kujieleza akaeleweka.
 
Hoja yangu ni kuwafikishia ujumbe wanasiasa, kwamba wajitahidi muda mwingi waongee vitu vyenye mantiki. Mipasho, kejeli na matusi sio silaha za kutegemewa na mwanasiasa mwenye kutaka kuacha legacy.
Mwalimu JKN anakumbukwa kwa sababu ya uwezo wa kujenga hoja. Zitto anazidi kukomaa katika uwezo wa kujieleza akaeleweka.
Kwahiyo Zitto ameacha legacy wapi sasa? ACT WAZALENDO? Halafu mbona husomeki, mara Clinton, mara Trump, mara Nyerere!
 
Back
Top Bottom