SoC02 Utambuzi wa fursa zinazokuzunguka ili kujikomboa kiuchumi

Stories of Change - 2022 Competition

KeeTZ

New Member
Aug 28, 2022
1
0
a) UTANGULIZI.

Vijana wengi wa sasa nikiwemo mimi kwa muda mrefu tumekuwa tukilalama, na pengine kuilalamikia serikali kwa uhaba wa fursa zinazoweza kufikika ili KUJIKOMBOA ki uchumi, mawazo haya yameshika hatamu vichwani mwa vijana wengi wakihisi fursa ni lazima mtu akukamate mkono na kukueleza "Fursa ni hii hapa" au "Njoo kuna mchongo huu hapa nikupe" au twende huku nikuunganishe na mtu atakaye kukusaidia"

Mtazamo huu wa maisha ulianza kupoteza nafasi taratibu katika maisha yangu binafsi miaka kama miwili iliyopita kupitia mfano hai kutoka kwa mdogo wetu wa mwisho.(Nitarudi kwake muda mfupi ujao)

Kiufupi fursa na mtu, fursa ni wewe hapo jinsi ulivyo, ukiwa bila connection, ukiwa bila laki au milioni moja mfukoni.

Fursa si hali, Fursa ni mtu na huyo mtu ni wewe binafsi, unatakiwa kufanya UTAMBUZI wa fursa zanazokuzunguka kupita wewe, unatakiwa kufanya utambuzi wa fursa kupitia changamoto zinazokukumba wewe binafsi na kutanua wigo kwa watu wengi zaidi wenye changamoto kama yako.

Utatuzi wa changamoto ndo uumbwaji wa fursa, anza kufikiri nje ya boksi kuwa ni nani na nani na kundi lipi na jamiii ipi mnaweza kwenda nao katika safari hiyo pamoja.

b) UTAMBUZI WA FURSA.

Mdogo wetu alipokuwa chuo, siku moja akaamua kutoka kwenda Karume kujitafutia raba ili naye apendeze, alifanikiwa kupata pair moja akarudi nayo chuo, kabla hata haijaanza kuitumia room mate wake akawa ameipenda akamuomba amuuzie, bila kusita akamuuzia kwa bei ya juu kidogo ya aliyonunulia na kuamua kurudi tena ILALA kupata kiatu kingine siku iliyofuata.

Akapata kiatu kama kawaida akarudi nacho chuo, kwa mara nyingine tena kuna mwanafunzi mwingine akakitaka kile kiatu na akauza tena (Hapo sasa kengere ikalia kichwani kwake na kuona kuna kitu anacho yeye binafsi ambacho anaweza kukigeuza kuwa fursa)

Akafanya UTAMBUZI wa haraka kwamba ana jicho la utambuzi bora wa bidhaa si kwa ajili yake tu bali kwa watu wengi zaidi, kwa maana kwamba amebeba radha ya watu wengine wengi.

Akaamua kuchukua hatua kuamsha kile kilicholala ndani yake na safari ya tatu anaenda kuchukua pea tano za viatu kwa mkopo, akavipanga, akavipiga picha na kufunga akaunti ya Instagram kwa mara ya kwanza akiwa na wafuasi sifuri.

Akachapicha chapisho, kila chapisho na picha yake akiwa na lengo la kunadi bidhaa alizokuwa nazo na kuzipandisha kwenye akaunti yake.(hapa alijiongeza Kidogo na kutumia mbinu za kidijitali kuwafikia raia wengi)

Viatu vile vyote viliuzika siku ile ile na watu zaidi wakiendelea kuulizia bidhaa.muonekano wa picha na machapisho aliyoyaweka yaliliza kengere nyingine kichwan, maana kuanzia siku iliyofuata walionunua bidhaa na wengine baadhi waliokosa walianza kuwa wafuasi wa ukurasa wake wa instangram, so akaendelea kurudi sokoni na safari yake ya kujifungulia milango ya KIUCHUMI ikawa umeanza rasmi.

c) PALIZI LA FURSA

Kuweza kuendelea kuihuisha fursa ulioitambua ni muhimu kuendelea kuwa mbunifu kwenye huduma au bidhaa unayotoa na kutanua wigo wa hadhira ili kuleta athari chanya. Dogo akaendelea kujiongeza kuhakikisha anapalilia alichokianzisha na kuhakikisha hakifi,wala hakidumai.

Akaanza kusoma machapisho mbali mbali na kuangalia video tofauti tofauti mitandaoni ya jinsi ya kukuza biashara yake, jinsi ya kuwafikia wateja wengi zaidi, jinsi ya kumaintain brand akanunua mpaka nakala laini za vitabu mitandaoni ki ufupi alijua nini anataka na afanye nini ili kukipata.

Vijana mwenzangu hakika kuna kila kitu tunachokihitaji wazi na kweupe na vikisubiria tu sisi kuanza kupiga hatua moja ya awali kufuata hizo fursa.hatua ya kwanza inaweza kuwa ngumu lakini jitihada na nia vyaweza kukupa mwanzo rahisi mno.

Huyu bwana mdogo Kipindi chote hiki alikuwa ikiniinspaya sana kwa kile alichokuwa akikifanya.aliendelea kukuza wateja lengwa wa bidhaa zake na kuendelea kufanya biashara huku Akiwa anasoma.(Tutarudi kwake tena )

d) MTAZAMO WA FURSA KIDIJITALI

Ukuaji wa Tehema na teknolojia ni fursa nyingine inayochagiza maendeleo ya kiuchumi kwa fursa zilizopo tayari. Mashirika tofauti na watu binafsi wapo kwenye nafasi kubwa ya kutumia huu ulimwengu wa kidijitali kwa kutumia teknolojia zilizopo na mifumo iliyopo kuchagiza, kufanya shughuli tofauti tofauti kukuza au kujiendeleza kiuchumi.

Watu wengi hapa nchini na ulimwenguni kwa ujumla wanafikika kirahisi kwa kutumia tecknolojia iliyopo tayari, vifaa vya ki elekroniki na mitandao ya kijamii iliyopo imekuwa media kubwa ya kubeba na kusafirisha jumbe za bidhaa au huduma kutoka kwa watoa huduma mpaka kwa walengwa kwa urahisi mkubwa. Hivyo matumizi mazuri ya teknolojia hii tulioyonayo yaweza kuchagiza na kuongeza tija kwenye fursa tulizonazonazo na kukuza uchumi.

Bwana mdogo alifanya kazi na mitandao ya kijamii usiku na mchana ili tu kuipa tija biashara yake.aliendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kila siku iitwayo leo ndani na nje ya nchi, alitumia simu janja yake vizuri, alitumia makala na elimu mtandao vizuri kuongeza ufahamu wa jinsi atakavyoendelea kukuza biashara yake.

Mbali na wateja wa hapa nchi akaanza kupata wateja nje ya mipaka ya Tanzania. Wow kufikia hii pointi ikawa dhahiri kabisa kwambia hii kitu imeanza kuwa kubwa.

Mteja wa kwanza ikitokea Africa ya kusini, ila aliendelea kupata wateja wengine kutoka Kenya, Zambia, na nchi kama tatu hivi kutoka ulaya ya mashariki.

Mapendekezo ya hadhira yamekuwa chanya kutokana na ubora wa machapisho anayoyapandisha lakini pia ubora wa bidhaa zinazowafikia wateja. Alijua mahitaji ya wateja wake na siku zote amekuwa akiwapa bidhaa ambazo ni orijino tu.

Mapendekezo chanya kwenye ukurasa wake yamezidi kumpa mwendo na amepitia hatua tofauti tofauti za ukuaji wa ukurasa wake wa Instangram kutoka wafuasi sifuri kwenda 300, kwenda 1400, kwenda 5,800, kwenda 7,000 na sasa ana +10.4k (Hii imefanikisha ufikiwaji wa wateja wengi zaidi na kumuongezea mauzo na hili imetokana na vitu vikuu vitatu alivyoweza kuvifanikisha kutokana na matumizi mazuri ya tehama na teknolojia
• Ubora wa machapisho(Ubunifu)
• Ubora wa Bidhaa
• Kujua mahitaji makususi ya wateja.

e) JUHUDI.

Tofauti baina ya ndoto zako na uhalisia ni Juhudi na kutokata tamaa

Nilikuwa nikimsikia dogo akiamka na kuanzia kuandaa kwenda kutafuta bidhaa saa 10 alfajiri hata kabla wengine haijaanza kujiandaa kwenda makazini ili awahi kurudi na kuhudhuria vipindi vinavyoanza malema chuoni.na amekuwa kufanya hivi bila kukoma kwa miaka yote mitatu mpaka kamaliza chuo.

Ki ukweli Jitihada zake zinaonekana leo maana hayupo kama alivyoanza. Kwa sasa anatengeneza pesa yake mwenyewe na hataki kabisa kusikia suala la kuajiriwa.( Katambua fursa, Katambua kuwa fursa iliyomzunguka ni yeye mwenyewe, katanya maamuzi kufanyia kazi na Imemtoa).

Mwanzoni

20220830_104326.jpg


Hivi Sasa
20220830_104138.jpg
 
Back
Top Bottom