Utamaduni wa Magharibi wa Demokrasia kushindwa kutia nanga kwenye nchi nyingi ni fumbo kubwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,557
46,104
Historia inaonyesha Demokrasia kitovu chake ni Ugiriki ambapo karne ya 5 binadamu wa huko waliibuka taratibu na wazo la maamuzi ya serikali na uongozi unaotokana na ridhaa ya watu wengi badala ya uimla.

Mifumo ya kidemokrasia ilitumika kiasi fulani kwa tawala kama himaya za Roma ya kale, karne ya 14 mabwanyenye wa Waingereza walimlazimisha mfalame wao kusaini mkataba wa Magna Carta ambao uliweka rasmi mfalme na Serikali ya kifalme hauko juu ya sheria, ulianzisha bunge na kuweka sheria za kulinda haki na mali binafsi za watu. Karne ya 18 yakaja mapinduzi na uhuru wa makolini ya Marekani dhidhi ya utawala wa kifalme wa Uingereza, yakaja na mfumo wa Urais na demokrasia kutumika kwa upana zaidi.

Tangu wakati huo demokrasia ikasambaa duniani na mataifa mengi Ulaya na nje ya Ulaya yakaiga hiyo mifumo ya utawala wa UK na US.Baadhi kama Ufaransa yakauondoa kabisa utawala wa kifalme na kusimika jamuhuri mengi yakazidhibiti nguvu za tawala zao za kifalme.

Demokrasia kama mojawapo ya utamaduni wa ulimwengu wa magharibi umeendelea kusambaa au kusambazwa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu lakini tofauti na tamaduni nyingine kama Dini, lugha na mavazi demokrasia imepata upinzani mkali sana na sababu nyingi kutolewa kwa nini demokrasia sio sahihi kwa sehemu zote za dunia, chache zina mashiko nyingi hazina mashiko.

Wapo wanaoamini demokrasia inashindwa kwenye baadhi ya nchi kwa sababu inachelewesha maendeleo, wengine wanaamini demokrasia kuzipa umuhimu haki za mtu mmoja mmoja zaidi kuliko jamii kwa ujumla kutaharibu jamii zao, wengine wanaona demokrasia inaenda kinyume na mambo mengi katika dini zao n.k

Yote kwa yote uimla unazidi kuwa imara na kuna kila dalili kwamba demokrasia haitashika mizizi kwenye nchi nyingi ambazo demokrasia haijashika mizizi mpaka sasa. Pia hata nchi nyingi ambazo demokrasia ilkuwa imeshika mizizi imara zinapitia changamoto kubwa zinazotishia uhai wa demokrasia zao kuendelea ku "survive".

Lakini kama ilivyo kawaida ya maisha ya binadamu kuwa katika muendelezo wa mapambano na kutafuta kilicho bora muda wote, muda utazungumza iwapo kuna upande utaibuka mshindi kabisa na kuuzima upande mwingine katika mapambano haya.
 
Back
Top Bottom