Utamaduni wa kuomba radhi kwa makosa ya kiutendaji

PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
335
496
Wadau tumeshuhudia baadhi Ma- Rais wastaafu wakiwaomba radhi watanzania, kwa makosa ya kiutendaji waliyofanya wakuwa madarakani.

Alianza Hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere, kwenye hotuba yake ya kuwaaga wantazania kabla ya kustaafu,alikili kuwa alifanya makosa ya kiutendaji akaomba radhi na akatoa sababu kuwa pamoja na mambo mengine, nchi ilipata Uhuru ikiwa na wasomi wachache sana,kwa hiyo watendaji wengi hawakuwa na ujuzi wala uzoefu wa masuaka ya kiutawala na kuendesha nchi.

Akaja Rais awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi( Mzee Ruksa).Baada ya miaka kumi ya utawala wake, akiwaaga wantazania,aliomba radhi kwa makosa ya kiutendaji,ambapo nchi likaribia kufilsika na kushindwa kukopesheka. Japo alijitetea kuwa alikuwa na nia nzuri, kufungua milango ya kuuchumi ikaishia kuingiza wema na wabaya. Alitia mfano kuwa unaweza kufungua dirisha la nyumba yako kwa ajili ya kuingiza hewa safi, lakini mbu, inzi na mbung'o nao wakajipenyeza kuingia na kuleta madhara makubwa.

Juzi kati Rais wa awamu ya tatu Mzee wetu Benjamini Mkapa akizidua kitabu cha maisha yake.(MY LIFE,MY DESTINY) alisikika akiwaomba radhi watanzani kwa makosa kadha wa kadha ya kiutendaji wakati wa utawala wake wa kipindi cha miaka kumi 1995-2005. Moja kati ya makosa aliyomba radhi ni pamoja na kashfa ta EPA ambapo amewatupia lawama waandamizi wake wa Karibu kwa kumshauri vibaya.

Hatujamsikia Rais wa awamu ya NNE, Mzee wetu Jakaya Mrisho Kikwete; pengine nae atakuwa jambo la kusema kuhusiana na kashfa ya Tegeta Escro, yetu macho na maskio.

Ni dhahiri sasa imezoeleka na kuwa utamaduni wa kila Rais anaestaafu kuomba radhi kwa makosa ya kiutendaji. Ingawa ni ustaarabu na uungwana kuomba radhi, pengine tuangalie namna nyingine nzuri ya kuweza kuubadirisha utamaduni huu kwa maslahi mapana ya nchi, ili tusiwe na viongozi wanaoshia kuomba radhi kwa makosa ya kiutendaji baada ya kustaafu.

Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madaraka yanalevya! Hivyo makosa na madudu yote hukumbukwa mara tu baada ya kurudi mtaani.
 
Back
Top Bottom