Utamaduni wa hovyo wa kutolipa madeni, sasa unatuletea aibu na fedheha kimataifa

Kulipwa lazima litalipwa, lakini aibu ya kutolipa madeni tayari tushavuliwa nguo!
Kama wewe ni mzalendo wa kweli kama mnavyojiita, unapaswa kulaani wote wanaosababishia taifa aibu kama hizi sio kuunga mkono hata ujinga!
ATCL kulikuwa na ufisadi mwingi miaka ya nyuma, nadhani unakumbuka kesi ya yule aliyekuwa bosi wa shirika hili, yule brother mwenye nyumba yake pale mbezi beach, enzi zile za matanuzi ya watoto wa Dar.

JPM anapambana na madudu ya kila aina, mengineyo ndiyo hayo madeni ya miaka ya nyuma.
 
Vipi na wewe umefurahia Mali yetu kushikwa kama wenzako?
Ni mjinga tu anayefurahia matatizo ya nchi, lakini aliyeyasababisha matatizo hayo ni mpumbavu.
Huwezi ingia mkataba wa huduma halafu usilipie, na unaendelea business as usual.
Awamu hii maofisa hao wanyooshwe, irresponsibility and complacency has no place in business.
 
Huyo Muzungu alidhurumiwa na Nyerere/Mwinyi kama sikosei kwa mujibu wa habari nilizosoma, sina uhakika lkn.
 
Ingawa mdaiwa siyo mwizi, ila dawa ya deni ni kulipa...

Wa kimataifa wanatumia mbinu kama hizo na mawakili wao wa kimataifa... wa humu humu ndani huruma sana...

Cc: mahondaw
 
Thsts not the point mkuu..Hujipaki kinyesi ati mto uko karibu.
Heshima ya nchi inachezewa na wachache.
Mkuu hili ni deni la muda mrefu sana, mimi na wewe tukiwa watoto wadogo. Litalipwa kama yalivyolipwa madeni mengi tu.

Unajua kuwa ile flyover ya ubungo ni deni litakalokuja kuanzishiwa uzi kama hili la huko Afrika ya Kusini?.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Wafanyabiashara wa ndani wanaidai serikali mabilioni hawalipwi, watumishi madeni kibao ya stahiki zao kila siku wanaambiwa uhakiki wengine mpaka wanastaafu au kufa bila hata senti kulipwa.
Wapo watu wameambiwa wana vyeti/majina feki pamoja na kufukuzwa kazi, ile michango yao halali waliyo weka kwenye mifuko ya jamii wamedhulumiwa huku serikali inatabasamu kwa furaha kuwa imeokoa fedha. Dhuluma baada ya dhuluma ndio sifa ya serikali yetu.
Sasa raha ya kudhulumu wanaipeleka hadi nje ya nchi na huko ndio nao watawala watakiona cha moto kwa dhuluma zao.
Vilio vya wafanyakazi na wafanyabiashara wa ndani vitaitesa sana serikali hii hadi ifike mahali ianguke kwa kuondolewa kidemokrasia au kimabavu. Yametokea kwa wengine kwa nini yasitokee hapa?
Hii comment yako inabidi waisome woote washajihishaji na wengine.
 
Kuna maafisa wengi serikalini, wanafikiri unaweza kuingia mkataba kitaifa na kimataifa, ambspo unaweza pata huduma, na kulipia hiyi huduma ni kudra ya Mwenyezi Mungu.

People dont follow on contracts.
Wakisha piga picha na tsi zso mikataba inatupwa kwenye mashelf.

Tumeona makandarasi wasiolipwa.
Kulikuwepo Fredericci na Konoike.
Hawa nasikia wamelipwa baada ya almanudura kukamatavndege zetu.

Wazawa wa ndani wengine hadi wamekufa kwa mishtuko ya kuuziwa dhamana zao, wasijue watapata wapi haki zao.

Leo tunaona masuala ya kukamatwa ndege ya ATC.

Huu utamaduni wa hovyo, kimsingi ni utapeli at Govt level, na haukuanza awamu hii.

Tujisahihishe.
Leo unamkaribisha Rais wa nje kumwomba uwekezaji, huku nyuma mwekezaji toka nchi yake anakudai hadi mahakamani.
Message gani tunaitoa nje.
Hii ni fedheha na aibu kwa nchi.
Serikali ya Tz imezoea dhuluma na utapeli, bora wale wa nje huwa wanajiongeza kwa ku'confiscate assets mpaka walipwe au hupiga mkwara wa ku'confiscate lakini wale local huwa wengi wao hawalipwi na wanaolipwa hufanya kama ni deal yaani anaye authorize ulipwe lazima mkubaliane percentage ya commission yake ndipo utaona malipo yanaidhinishwa.
 
Mkuu hili ni deni la muda mrefu sana, mimi na wewe tukiwa watoto wadogo. Litalipwa kama yalivyolipwa madeni mengi tu.

Unajua kuwa ile flyover ya ubungo ni deni litakalokuja kuanzishiwa uzi kama hili la huko Afrika ya Kusini?.
Mkuu usihalalishe udhaifu wako kihistoria, madhara yake ni wanao kuingia utumwani.

Na tofautisha madeni toka wafanyabiashara na yale ya mashirika ya kimataifa.

Yale madeni toka mashirika ya kimataifa ingalau yanazungumzika.

Yale ya wafanyabiashara/makandarasi unalipia puani.
 
ATCL kulikuwa na ufisadi mwingi miaka ya nyuma, nadhani unakumbuka kesi ya yule aliyekuwa bosi wa shirika hili, yule brother mwenye nyumba yake pale mbezi beach, enzi zile za matanuzi ya watoto wa Dar.

JPM anapambana na madudu ya kila aina, mengineyo ndiyo hayo madeni ya miaka ya nyuma.

Wale wanaotulete mateso haya wakamatwe na hata kama wamekufa wengine mali zilizobaki zifilisiwe na watu waende jela itakuwa fundisho kwa watu kufanya makosa yanayoitia hasara nchi au watu milioni 50 wakati mjinga mmoja familia yake inasoma USA na kuishi huko na wengine wakiishi humu wakitutambia na utajiri ambao baba zao wametia hasara taifa hili..Operation hii isiwe na macho ikamate kila aliyelihujumu taifa hili na kuwaghalimu masikini watanzania wanaokosa madawa na kupata huduma mbovu huku mijitu na familia zao ikiruka ughaibuni kwenye matibabu..
 
Hao wote na chain yao wakamatwe, Wengine waliishi SA na familia zao kipindi cha Alliance air mpaka hizi hasara zikapatikana kama sikosei mmoja wapo tena na mke wakaingia kwenye kesi ya EPA akahukumiwa sijui miaka 2 sidhani hata kama aliitumikia..

Mkuu moja ya tatizo la CCM ni kufumbia macho ujinga mpaka mtu akiwa adui kisiasa ndio inatumika kama fimbo ya kumchapa na akiwa ndani anaangaliwa tu huku mapambio yakiimbwa, zaidi ya 90% ya makada wa CCM wako kimaslahi kwa maana ya opportunistic, tukiweza kulisimamia hili la kutoangaliana usoni aka chama kwanza na tukajiwekea tu utaratibu makini na serious utakaodili na fraud zote kwenye mali za umma hasa kuanzia juu kabisa na watu wakawa wanakwenda jela immediately sio hizi kesi ya miaka na miaka zisizoisha kifupi mwenzi mmoja mpaka miwili hukumu tayari mtu anaanza kutumikia 20yrs to 50yrs in prison heshima itakuja na watu wataacha mizaha..
 
Mkuu hili ni deni la muda mrefu sana, mimi na wewe tukiwa watoto wadogo. Litalipwa kama yalivyolipwa madeni mengi tu.

Unajua kuwa ile flyover ya ubungo ni deni litakalokuja kuanzishiwa uzi kama hili la huko Afrika ya Kusini?.
Bukilo siyo kwamba wasiyopendezwa na tabia za kudhulumu za serikali. Eti si wazalendo. No ni wazalendo.

Tatizo linaanza na mikataba mibovu tunayowapa sirini, huku ikiwa favour wawekezaji. Na zinapotolewa mahakamani na hasa mahakama zisizoingiliwa kisiasa na maagizo ya juu. Mara moja tunashindwa kesi !!!.
Ndiyo maana watu wenye nia njema wanataka mikataba kabla ya kuingiwa iperekwe bungeni. Na asiachiwe kiongozi wa wizara, au wa kisiasa kufanya mikataba kwa niaba ya nchi bila kusimamiwa na chombo cha umma kama bunge, takukuru nk.

Wote tunaipenda nchi yetu. Japo tunaweza tukatofaotiana juu ya viongozi na tawala.

Hebu fikiri kama hapa nyumbani Mzee kakataza mali za serikali zisishikiliwe kwa amri za mahakama. Je wadeni wa ndani watapataje haki zao ?!. Tabia kama hizi mbaya . ZIKEMEWE NI UBABE.
 
Wale wanaotulete mateso haya wakamatwe na hata kama wamekufa wengine mali zilizobaki zifilisiwe na watu waende jela itakuwa fundisho kwa watu kufanya makosa yanayoitia hasara nchi au watu milioni 50 wakati mjinga mmoja familia yake inasoma USA na kuishi huko na wengine wakiishi humu wakitutambia na utajiri ambao baba zao wametia hasara taifa hili..Operation hii isiwe na macho ikamate kila aliyelihujumu taifa hili na kuwaghalimu masikini watanzania wanaokosa madawa na kupata huduma mbovu huku mijitu na familia zao ikiruka ughaibuni kwenye matibabu..
Hili naunga mkono.
Uzuri wa Magufuli haogopi mtu.

Nchi insingia fedheha na sibu kwa sabsbu kundi la watu fulani wanastarehe..
Business as usual.

Ieleweke uki i commit serikali katika madeni, aliyehusika achukuliwe hatua.
 
Mkuu usihalalishe udhaifu wako kihistoria, madhara yake ni wanao kuingia utumwani.

Na tofautisha madeni toka wafanyabiashara na yale ya mashirika ya kimataifa.

Yale madeni toka mashirika ya kimataifa ingalau yanazungumzika.

Yale ya wafanyabiashara/makandarasi unalipia puani.
Ungekuwa wewe ni wa kwanza kudaiwa hapo ingekuwa sawa. Ningeweza kukuelewa.
 
Back
Top Bottom