Utalii wa ndani

Isack Elia

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
331
474
Je ushawahi kufanya utaliiwa ndani kwa kutembelea hifadhi yoyote nchini? Kama hapana nini kinakukwamisha na kama ndiyo tutajie ulipotembelea
5b11aac874c04e908136eddf565d369b.jpg
 
Je ushawahi kufanya utaliiwa ndani kwa kutembelea hifadhi yoyote nchini? Kama hapana nini kinakukwamisha na kama ndiyo tutajie ulipotembelea
5b11aac874c04e908136eddf565d369b.jpg

Hapo nilishafika kwenye ziwa la viboko, ngorongoro kama sipo basi patakuwa pamefanania, tena nilipiga picha kwenye huo mti hapo kulia.
Utalii wa ndani nilishaufanya kama group ambapo tulienda mbugani siku hiyohiyo na kuondoka sijawahi kulala huko kwa kuogopa kuliwa usiku hasa pale park guards wakiwa wameondok kwenda kulala.

Mleta mada labda nizungumzie gharama za hoteli zilizoko kwenye mbuga zetu, ziko aghali sana. Halafu sijui kama huwa wanamsimu wa kushusha bei ili kuvutia watu kuja kulala huko kwa wingi na kufika mbugani kuangalia
wanyama. Kiufupi gharama ya kwenda kuangalia wanyama ni ndogo ila ya kulala hoelini ndo kubwa mnoo kana kwamba wengi wakijiwaza wanaghairi.

Ila wenzetu wakenya wanawezaje? Mbona huwa wanatoa ofa sana za watu kwenda kulala hoteli za mbugani kwa bei za ofa karibu na bure? huku kwetu tumelogwa na nini?
Au wanaogopa wanyama wenyewe hakuna wameshawindwa na wawindaji haramu na wengine kuuzwa nje?

Mleta mada pia labda ungeongeza picha za utalii kuvutia wachangiaji.

Mie nilitembelea Mikumi na Ngorongoro, natarajia kwenda Maasai Mara, Sekenai Camp in Nairobi mwezi wa 12, kuna bonge la ofa.
 
Kupata gari lakukupeleka mbugani ndiyo ghali. Wala si Hotels. Kwa mfano Ngorongoro ipo hostel nzuri tu yeyote anaweza akalala pale. Pia huitaji kulala mbugani.....maeneo ya Karatu kuna lodges and Hotels nzuri mno chaguo lako tu.

Sasa hivi yamefanyika maboresho unalipia Bank kila kitu ukifika getini unaonyesha pay in slip unapita. Hii imesaidia sana kupunguza muda wa kusubiri getini maana asubuhi magari yanakuwa mengi especially high season.

Ukiwa na gari binafsi utafurahia tour yako gharama inapungua sana.

Well, nimetembelea hifadhi nyingi tu Tz hasahasa kaskazini maana ndipo naishi. Ngorongoro, Manyara, the Serengeti, Tarangire, Mt Kilimanjaro pia bila kusahau Hadzabe community na sehemu nyingine ndogondogo za utalii kama Ngorongoro Endoro (Elephant cave).
 
Kilimanjaro,ruaha,ngorongoro zote tayr natamani sana kwenda Serengeti
 
Back
Top Bottom