Utalii na madhara ya mabomu Tanzania

waltham

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,522
1,045
[h=2]Kenya, Tanzania attacks blow to tourism industry[/h] Kenya and Tanzania were targeted in separate attacks in key tourist sites, police said.

ni mapema kusema kutakuwa na hadhari zozote kutokana na mabomu huko arusha lakini wengine hapa JF wamekuwa wakisherekea mabomu kenya sasa basi yaja nyumbani tz, siwasikii sauti zao tena. kuwaza tu..............
 
Ni kweli kwamba mashambilio haya ya mabomu kwenye miji muhimu kwa utalii yanaathiri uchumi. Serikali iwe makini,uwezekano upo kuwa baadhi ya Watanzani hata viongozi wasio waaminifu wanahusika/wanashirikiana na wahalifu. Turejee bomu lililolipuliwa kwenye mkutano wa Chadema Arusha,mheshimiwa mmoja alisema kabla kuwa kutakuwa na mauaji kwenye mkutano Chadema kufunga kampeni ya uchaguzi mdogo,kweli mauaji yakatokea,alijuaje? Lini alianza kutabiri majanga? Kwa nini serikali ilikataa kuunda tume ya kimahakama kuchunguza? Haiwezekani haya mauaji yatokee,wahusika wasipatikane,bila uhusika wa mtu mkubwa/kiongozi. Ingefaa uchunguzi uende mbali sana.
 
Mimi nadhani huenda haya mabomu siyo CCM Vs CHADEMA/Upinzani. Tujiulize kwanini yatokee Arusha? Naweza ku-speculate kuwa yeyote anayefanya hivi lengo lake ni kuhujumu utalii. Swali jingine ni kuwa nani anaweza kuwa nyuma ya kuhujumu utalii? Serikali isiliangalie kwa muono wa Siasa au Udini peke yake. Kuna mtu au kikundi cha watu kinataka mambo yawe draw au ni njia nyingine ya kuifanya Tanzania ijiingize kwenye vita Somalia. Tanzania ikifanya hivyo itakuwa ina-commit a grave mistake. Ah! nawaza kwa sauti tu.
 
Hata mimi nina mashaka na nchi jirani...why Arusha na Zanzibar????

Tena nchi jirani hiyo yaweza isiwe direct competitor ila ni yenye chuki tu na Tz....

Kwa nini si DSM?????

vile vile tusidharau hawa wanasiasa...they are capable of anything kwa kuwa ni most selfish human beings....

Kikubwa serikali iweke ulinzi mkali na isambaze wana usalama nchini...tumezungukwa na maadui kila kona...kuna wanaoonea gere amani yetu; kuna wenye hasira ya kichapo; kuna wenye hasira ya ardhi yetu, wenye hasira ya kunyang'anya watalii wao; kuna wanaodhani sisi ni sababu ya wao kutokuwa maarufu anymore...and the list goes....

Wewe angalia humu watu wanasema watanzania tuna wivu; like serious???? Tuna wivu gani wakati tulishajizoelea kuwa wa mwisho katika kila kitu isipokuwa amani...kati yetu na wao (number one) nani anayeweza kuwa na wivu na mwenzie? Nani anayeingiwa na woga wa maendeleo ya mwenzie...sie tulishazoea kuachwa kiuchumi ...wao ndio wnaweweseka

Ingekuwa enzi za mwalimu...ambapo ilikuwa ngumu hata kuiteta serikali (1/4 ya wananchi walikuwa mashushu) hawa wote wangekuwa mbaroni...naona usalama wa Taifa kwa sasa huko very weak....

Mugo"The Great";10012570 said:

Kenya, Tanzania attacks blow to tourism industry

Kenya and Tanzania were targeted in separate attacks in key tourist sites, police said.

ni mapema kusema kutakuwa na hadhari zozote kutokana na mabomu huko arusha lakini wengine hapa JF wamekuwa wakisherekea mabomu kenya sasa basi yaja nyumbani tz, siwasikii sauti zao tena. kuwaza tu..............

unknown.gif
 
Hata mimi nina mashaka na nchi jirani...why Arusha na Zanzibar????

Tena nchi jirani hiyo yaweza isiwe direct competitor ila ni yenye chuki tu na Tz....

Kwa nini si DSM?????

vile vile tusidharau hawa wanasiasa...they are capable of anything kwa kuwa ni most selfish human beings....

Kikubwa serikali iweke ulinzi mkali na isambaze wana usalama nchini...tumezungukwa na maadui kila kona...kuna wanaoonea gere amani yetu; kuna wenye hasira ya kichapo; kuna wenye hasira ya ardhi yetu, wenye hasira ya kunyang'anya watalii wao; kuna wanaodhani sisi ni sababu ya wao kutokuwa maarufu anymore...and the list goes....

Wewe angalia humu watu wanasema watanzania tuna wivu; like serious???? Tuna wivu gani wakati tulishajizoelea kuwa wa mwisho katika kila kitu isipokuwa amani...kati yetu na wao (number one) nani anayeweza kuwa na wivu na mwenzie? Nani anayeingiwa na woga wa maendeleo ya mwenzie...sie tulishazoea kuachwa kiuchumi ...wao ndio wnaweweseka

Ingekuwa enzi za mwalimu...ambapo ilikuwa ngumu hata kuiteta serikali (1/4 ya wananchi walikuwa mashushu) hawa wote wangekuwa mbaroni...naona usalama wa Taifa kwa sasa huko very weak....

Mbona muna uoga wa kutututaja Kenya, haja gani uzungushe maneno ovyo na kiusanii. Mnalipuana kijinga halafu kwa uoga mnakimbilia kutulaumu. Wakenya hatuna muda na mahangaiko yenu. Visa vya kiajabu tumezoea kuvisikia tokea Bongo, mara kulipuana kwa mabomu mikutano ya siasa na kuwamwagilia tindi kali Wakristo na watalii, mabomu ovyo. Chuki zenu wenyewe za kidini na pumba.

Ifahamike sisi hatuna gere na uchumi wa Tanzania na kadiri unavyokua ndivyo hata sisi tunanufaika maana Wakenya ndio wa pili katika uwekezaji Bongo baada Waingereza.
Zaidi, kustawi kwa utalii Tanzania pia kuna Wakenya wengi wananufaika kwa kufanya deals na makampuni ya kitalii ya Bongo na kuwaleta Watalii.

Gesi ya Mtwara itawanufaisha Wakenya pakubwa pia, maana ninyi hamna viwanda vya kutosha kuitumia yote.

Hivyo, tumieni inteligensia yenu kubaini nini chanzo cha mabomu haya, haswa mnapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Muache kutapatapa ovyo.
 
Ushakunywa chang'aa yako unaongea kama umewekewa mota yakuongeza maneno mdomoni. Kawatulize al shababu huko kwenu, kwetu yanakuhusu nini? acha ubwe-ge
 
Back
Top Bottom