Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,178
Mataifa yanayofanya vizuri na kuongoza katika utalii duniani ni pamoja na; Ufaransa, Hispania, Marekani, China, Italia, Uturuki, Mexico, Ujerumani, Uingereza. Kwa Africa ni South Africa, Misri, Morocco, Algeria, Zimbabwe, Mozambique, Ivory Coast, Kenya na Botswana.
Ukiyatazama mataifa haya kwa undani utagundua kila moja lina yote au baadhi ya mambo yafuatayo:
1. Historia kubwa, za muda mrefu na maarufu duniani kote. Ukiizungumzia hispania ni taaifa lililohusika kwa kiasi kikubwa kuwafanya binadamu wafike sehemu nyingine za dunia, US ni taifa la kwanza katika Ulimwengu wa kisasa kuanzisha Demokrasia, Misri ina historia maarufu ya mafarao na Piramidi n.k
2. Siasa zenye ushawishi mkubwa kwa mataifa mengine. Hapo utaiona Marekani, China, Uingereza, Misri, n.k
3. Muingiliano mkubwa na wa muda mrefu na Mataifa mengine. Kuna mataifa ambayo yako wazi sana kutembelewa na raia kutoka nchi nyingine na kuna mataifa ambayo ni yaliyojifungia "wanapenda kufanya mambo yao kama kisiwa cha kipekee"
4. Biashara na uchumi wa soko hurua ni kigezo kikubwa katika kupata watu wengi wanaoitembelea nchi yako. Botswana ni mzalishaji namba moja wa Almasi Africa, Kenya imekuwa taifa la kibepari tangu kuanzishwa kwake.
5. Miondombinu bora. Watalii wanapenda watembelee maeneo yenye barabara nzuri za lami, hospitali bora, miji misafi n.k
Kama tunataka kuwa na sekta kubwa ya utalii kuliko wengine barani Africa tuzingatie hayo. Kuwa na vile "tunavyofikiri" ni vivutio vingi na kuvitangaza kwa nguvu sana ni tone dogo tu katika bahari ya utalii.