Utakiri kwa kutokuwa mwaminifu?

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Kwa sababu yoyote ile, iwe ni kwa kuteleza au kwa uchakaramu wako,
lakini mwenzako amegundua au ana wasiwasi nawe kuwa si mwaminifu
katika mahusiano na akaamua kukuuliza kutaka ukweli. Jee:
Utakiri na kutubu? Utaongopa lakini utatubu? Utaongopa na utaendelea?
Ni mazingira gani yatakufanya uchukue uamuzi mmoja au mwengine?
 
@MAMMAMIA...........kwa hili wanawake wengi ni wahanga..... wanawake kwa kiwango cha kutosha hukiri kwamba wametoka nje ilhali hawajatoka. kuna wanaume ambao wakitilia shaka jambo hulijenge mazingira kama vile ni la kweli. wanawake kwa kutojiamini hujikuta wakikiri kwamba walitoka nje kwa lengo la kutaka yaishe, lakini ukweli ni kwamba hali huwa mbaya zaidi na inaweza kupelekea hata uhusiano ukavunjika.....
Na ikitokea tuhuma hizo zikafikishwa kwa wazazi kwa nia ya kumaliza mgogoro huo, mwanamke anaweza kusema ukweli juu ya tuhuma hizo akikanusha kuhusu kuhusika na tuhuma hizo, lakini mwanaume anaweza kuhoji ilikuwaje akiri kosa hilo wakati hakulitenda, na mke naye kwa kuhamaki anaweza kudai kwamba alilazimika kukiri ili yaishe kwa kuwa mumewe alikuwa anang'ang'ania kwamba alitoka nje wakati si kweli..................

Kwa upande wa wanaume, wao wanaweza kukiri kwamba walitoka wakati hawajatoka kama mke atakuwa anang'ang'ania juu ya tuhuma hizo, lakini kwa njia ya ubabe, na mke akizidi kuchonga sana anaweza hata kuambulia vipigo.......................
 
Nimekupata Mkuu, bila ubabe au kutaka yaishe, ikiwa ni kweli hauko mwaminifu,,bora ni lipi, kukiri au kuuchuna?
 
Kwa mwanamke itakuwa ngumu kukiri kwa sababu hatua inayofuata hapo kila mtu anaijua ni ngumu sna kwa mwanume kumsamehe mwanamke msaliti. Ila kwa mwanaume atasema tu anajua atasamehewa,
 
kukiri kunategemea na mazingira lakini mara nyingi wanaume wanaweza kukiri kutoka nje kama kufupisha kelele au ugomvi ilihali hajafanya hivyo , hasa akikutana na mwanamke muongeaji na yeye si muongeaji.. wanawake wanatengenezewa mazingira ya kipigo na inamlazimu kukiri kwamba katoka au alikaribia kutoka katikka kujinusuru kipigo
 
napita tu, ila naomba uniandikie majina ya wale wote wamekiri kua sio waaminifu. nitarudi na zawadi zao
 
Nimekupata Mkuu, bila ubabe au kutaka yaishe, ikiwa ni kweli hauko mwaminifu,,bora ni lipi, kukiri au kuuchuna?

Ni kumuacha anayekutuhumu athibitishe........... kwa mfano, LINI, WAPI,SAA NGAPI, NA NANI.......................
 
Ni kumuacha anayekutuhumu athibitishe........... kwa mfano, LINI, WAPI,SAA NGAPI, NA NANI.......................

ni nadra sana kuwa na vitu hivyo wengi hutengeneza mazingira ya kulazimisha
 
Bora kuuchuna na kujirekebisha na kuacha kabisa, haya mambo ya kukiri kiri hovyo yanaweza leta balaa bure ikala kwangu.
 
Dah mimi mwenzeni kila nikitaka kuakupiga kazi za nje wife ananishtukia dah, mpaka najionaga **** .... nimeamua kutulia NGURUWE PITA SINA MKUKI MIYE!!!!!
 
Kwa mwanamke itakuwa ngumu kukiri kwa sababu hatua inayofuata hapo kila mtu anaijua ni ngumu sna kwa mwanume kumsamehe mwanamke msaliti. Ila kwa mwanaume atasema tu anajua atasamehewa,
Ninakubaliana nawe lakini si wanawake wote wanaokubali kusamehe. Ile akisikia tu harufu ya usaliti anakunja virago na hakuna kumrejesha nyuma. Pia si wanaume wote wasiosamehe wake zao; kuna wengine sijui kama ni kupenda kupindukia, ufahamu kuwa binadamu tunakosea au vipi, lakini wapo wanaosamehe.

kuuchuna na kurekebisha tabia yangu[/QUOTE] Hii inakubalika kwa kuepusha mifarakano zaidi katika mahusiano.

kukiri kunategemea na mazingira lakini mara nyingi wanaume wanaweza kukiri kutoka nje kama kufupisha kelele au ugomvi ilihali hajafanya hivyo , hasa akikutana na mwanamke muongeaji na yeye si muongeaji.. wanawake wanatengenezewa mazingira ya kipigo na inamlazimu kukiri kwamba katoka au alikaribia kutoka katikka kujinusuru kipigo
Hapo red! Inaonesha kama mtu hakukamatwa kwenye mlo, anaweza kuzua lolote ili asikubali kosa lake. Tatizo kwa kutumia hoja ya nguvu wanaume ni rahisi kukwepa na wanawake kuingia mtegoni. Mwanamke akikiri anatafuta kipigo na talaka, asipokiri kisago mpka atajuta. Wanaume wengine kama polisi wa mahabusu.

It wasnt me....
Boss mbona umeruka?

Ni kumuacha anayekutuhumu athibitishe........... kwa mfano, LINI, WAPI,SAA NGAPI, NA NANI.......................
Hii ndio hiyo kutafuta hoja ya nguvu - hakuna ushahidi, hakuna kosa, hata kama umekosa.

Bora kuuchuna na kujirekebisha na kuacha kabisa, haya mambo ya kukiri kiri hovyo yanaweza leta balaa bure ikala kwangu.[/QUOTE]. Hapo red: Bora nusu ya shari kuliko shari kamili, ingawaje kiustaarabu bora kukiri, hatari zake ni kupunguza mapenzi usiaminike tena.
 
Back
Top Bottom