Utakiona cha mtema kuni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utakiona cha mtema kuni!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzizi wa Mbuyu, Jun 12, 2009.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nalitumia, kusikia sana msemo huu "CHAMTEMA KUNI" kwa muda mrefu sasa katika maisha yangu ya kila siku. Najua kuna maneno yanatumika kwa maana hiyo hiyo kama vile; kilichomtoa kanga manyoya ya shingo, kijinga cha moto, kilicho mfanya chura ashinde mtoni n.k haya maelezo yake yako wazi.

  Ila ukweli ndugu zanguni nimejaribu kuulizia chanzo cha matumizi ya neno hili, nimeishawahi kusikia kuwa ni msemo wa wahenga tu..., wengine wanasema ni hadithi ya kimapokeo, wengine wanasema ni hadithi ya kwenye kitabu. Lakinipamoja na yoote hayo sina uhakia hasa nini chanzo cha neno.
  Please, naomba ufafanuzi, kwa yeyote anaejua msemo huu "CHAMTEMA KUNI" ulitokana na nini. Cha mtema kuni! kipi! kiatu?, kisa?! ,kiuno?! nk kilifanya nini hadi kiogopwe namna hii??!!

  Kama ni hadithi , ilikuwa kwenye kitabu gani? Mtunzi alikuwa nani...na mengineyo....

  Maoni ya watu mbalimbali kutokana na swali hili...

   
 2. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Lugha ninayojua ni "akifanya hivyo atakiona cha mtemakuni". Ninaelewa ni kama tishio au onyo: akifanya kitu kisicho halali ataona matokeo yake yaani atapata adhabu.

  Mtemakuni (pia: mtema-kuni au mtema kuni) ni mtu anayepasua miti kuwa kuni. Kwa hiyo ana kazi nzitonzito pia ni watu wenye nguvu ya kimwili. Maana neno "kutema" hupatikana kwa maana mawili moja ni "kutema mate" mengine ni "kupasua kitu" kama ubao, miwa n.k.

  Sina uhakika juu ya asili ya usemi lakini nimeielewa hivyo:

  Hawa watemakuni ni watu wenye nguvu wanajua kuadhibu. Ukitaka kuiba kwao utaona jinsi gani wanavyoweza kujitetea. -
  au labda pia: Watemakuni ni watu wanaoishi katika mazingira magumu msituni wakifanya kazi hii nzito heri usijaribu kucheza nao...

  Sijui wenzangu wanaonaje?
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana ndugu yangu, si haba, iatabidi niende BAKITA pia kujiridhisha.
  Hapa inaoneka wengi wetu huwa tuna tumia misemo tusiyojua asili yake!
   
 4. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  BAKITA unataka kuuliza namna gani? Je wanao ukurasa mtandaoni unapoandika maswali?
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Ntakwenda mzimamzima ofisini kwao, ninashida sana na hii kitu ndugu yangu nina kazi nayo. Sidhani kama watakosa ufafanuzi juu ya msemo huu. Kama unakingine cha kunisaidia, sema ndugu yangu.
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mzizi wa Mbuyu nimekupata mkuu ngoja nichangie kidogo; Mimi hili nilipata simulizi toka kwa jamaa mmoja wa Kenya ambae anasema kuna mwalimu aliwasimulia shule ya msingi juu ya kisa cha mtema kuni. Hiyo hadithi inasema hivi:

  Siku moja jamaa mtema (mkata) kuni alienda porini kukata kuni. Sasa akakuta mti mkubwa umeanguka na umekauka vizuri, ambao wenyeji wanaupenda sana kwa kutumia kwa vile kuni zake hazitoi moshi n.k. Sasa huyo mtema kuni akaanza kukata kuni na kurundika mzigo mkubwa tu.

  Jua lilipozidi kuwa kali jamaa akavua nguo akabaki uchi (hakutarajia mtu kutokea maeneo hayo kwa vile ni mbali na makazi ya watu) huku akiendelea na kupasua kuni toka kwenye lile gogo. Ikatokea jamaa akawa amechoka na pia jua kali, kwa hivyo akaamua kukaa juu ya lile gogo kupumzika.

  Sasa lile gogo lilikuwa lina ufa (kutokana na kutanuka kwa jua kali), kwa hivyo nyanya zikawa zimening'inia kwenye huo ufa. Baada ya kitambo kirefu kupita, jua nalo likawa linazama; kwa hivyo jamaa akaamua kunyanyuka ili ajitayarishe kuondoka. Sasa kumbe lile gogo lilikuwa limeshaanza ku-contract (kusinyaa); kwa hiyo nyanya zikashindwa kutoka.

  Jamaa wakati anakukuruka, huku contraction ya gogo inaendelea taratibu; jamaa akajikuta immediate options zimekauka kwa vile hakuweza kujinasua na shoka lilikuwa mbali hivyo hawezi kuzikata nyanya ili atoke. So, jamaa ndio akafia pale juu ya gogo baada ya mateso ya muda mrefu, kwani hata kelele alizopiga hazikuweza kusikika kijijini ambako palikuwa mbali. Kwa hivyo, ndugu, jamaa na marafiki walipomtafuta ndio wakamkuta jamaa amejifia juu ya gogo na nyanya zimenasa ndani ya gogo....! Kwa hivyo ikaonekana ni mateso makubwa mno mtu anayoweza kuyapata, so watu wakawa wanafanya reference kwamba ukifanya jambo baya/ukaidi n.k then utakiona cha mtema kuni

  Poa mkuu nipe thanks....
   
  Last edited: Jun 17, 2009
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mtemakuni hakika ni mpasuaji au mkataji wa kuni kama wengine walivyosema. Hadithi ya mkatakuni wengine wanasema wakati akikata kuni alikosea mahesabu (umakini)shoka likatua kwenye mguu likampasua na kumjeruhi sana. Kwa hiyo, kukiona cha mtemakuni ina maana ya kujiingiza kwenye shida ya kujitakia, ni kukosa umakini katika kutenda jambo ambapo baadaye mtu anakuja kujuta kutokana na shida atakayoipata. Kumbe, ni msemo wa onyo, wa kumtaka mtu awe mwangalifu ili mabaya yasimkute. Ni msemo unaotaka seriousness ya mtu katika kutenda ili kujiepusha na matokeo mabaya.
   
 8. k

  kela72 Senior Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bonge la elimu hii, tumeelimika wengi!
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Mkuu, thanks umepata ila duh! kama ni kweli ilikuwa hivyo, mtema kuni aliteseka sanaa!! Yaani nanihii.. yake ilibanwa kwenye gogo!!
  Poa, lakini kweli pia ntakwenda BAKITA, nikipata muda kuchunguza jambo hili.
   
 10. Madam Koku

  Madam Koku Senior Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mi huwa nafahamu simulizi tofauti kuhusu ''kukiona cha mtemakuni'', sikuwahi kusikia pia hizo zilipoelezwa hapo juu.
  Niliambiwa kuwa mtema kuni ni mtu anaekata kuni na alieenda kukata kuni porini na alipokuwa anataka kuzifunga kuni pamoja akawa anatafuta kamba, na bila kujua akamgusa nyoka akidhani ni kamba ili afungie kuni, loooo! kilichofuata ni mapambano... kwa hiyo hicho ndo kilikuwa ''cha mtemakuni'' nilichokifahamu.
  It is so intresting kuwa kuna simulizi tofauti tofauti kuhusiana na msemo uleule. Na nafikiri mambo kama haya yangehifadhiwa vizuri (yangekuwa well documented) ingesaidia kwa vizazi vijavyo hasa ukizingatia kiswahili kinakua sana sasa hivi ktk nch nyingi za Afrika.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii methali inatokana na hadithi au simulizi ya mkata kuni (Mtema kuni... Hiki ni kiswahili cha zamani). Kwa ufupi inasimuliwa kwamba mkata kuni alikwenda porini kwa nia ya kutema kuni (kukata kuni) kutokana na sababu anazo zijuwa yeye au kwa kuzidiwa na mawazo alipofika porini akapitiwa na usingizi (kama bado nakumbuka vizuri) ndio kwanza ulikuwa muda wa Mawio yaani jua linachomoza).

  Alipokurupuka... kuangaza huku na huku shoka halioni, na hali anakumbuka vizuri kulichukuwa...

  Yeye hakahisi labda limedondoka mahali... akaanza kulitafuta kuanzia Mawio mpaka Machweo (Kuzama kwa jua Wakati wa Magharibi) Mwisowe akajikuta amechoka na shoka halionekani.

  Akaamua kukaa chini ya mti ili apumzishe akili na kutafakari upya wapi alipolidondosha shoka lake. Wakati anajiandaa kukaa chini kuangalia begani kwake analiona shoka lake... kumbe alikuwa amesahau kuwa shoka lilikuwa amelining'iniza begani kwake...

  Hapo ndipo palipo patikana huo msemo wa "Utakiona cha mtema kuni... Kutafuta shoka wakati lipo begani."

  Hii kidogo inataka kufanana ule msemo wa "Utakiona kilicho vunja shoka mpini ukabaki... msemo huu umetokana na simulizi za Sir H. Rider Haggard kwenye moja ya simulizi zake zinazo elezea visa vya mwindaji Tembo hodari Bwana Allan Quatermain (Makumazan or Macumazahn)... Na msaidizi wake Msolopaganzi (Umslopogaas) na shoka lake Nkosi kazi (Inkosi-kaas)... Bwana Henry Curtis, na rafikie Kapiteni Good, (Bwana Mzuri).

  Kwenye liwaya hii ndipo pia lilipo patikana jina Gagula... Kibibi kilichokuwa kichwawi (Kigagula)

  Vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu ambavyo vinaonyesha au kusimulia ujasiri wa hali ya juu sana... Pia kwenye ile riwaya ya Machimbo ya Mfalme Suleiman na nchi ya Wakukuana... Na vile vingine ambavyo havikuwahi kutafsiriwa kwa kiswahili kama vile SHE & Ayesha (Tibet)

  Wale walio wahi kusoma watamkumbuka sana Bwana Msolopaganzi (Umslopogaas) na majigambo yake a.k.a Mikwara mizito aliyokuwa akiwatishia maadui zake...

  Nakumbua mwisho wa riwaya Umsolopaganzi alipomaliza kazi ya kulinda ngazi kuu... Alikuwa amepata majeraha mengi mwilini... akajua kuwa mwisho wa uhai wake umekaribia ndipo alipoamua kufa na shoka lake (Bibi msemi).... alilizungusha shoka lake kiasi ya kuonekana kama mwali wa moto... kisha kwa pigo moja... pigo lililo takatifu... Pigo lililo nyooka... akalishusha shoka lake kwa kasi ya ajabu na kulipasuwa jiwe lile na huku shoka lake likitawanyika vipande vipande na kubakia akiwa ameshikilia mpini wa shoka ukiwa mzima.... Mzee wa kizuru akaanguka chini akakata roho...

  Soma baadhi ya vipande toka Riwaya ya Allan Quatermain...

  Soma majigambo (Mikwara ya mzee wa Kizuru)
   
 12. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 80
  Tangu nikiwa shuleni nimekua nikiusikia huu usemi,hivi ni nini hasa mtema kuni alikiona mpaka iwe hivyo..
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Happy Valentine wana jf. Naomba kujua kisa kilichompata "Mtema Kuni" hadi huu msemo kuwa maarufu, hasa pale mtu anapoonywa asitende jambo fulani.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kutema ni kukata kwa kibantu
  kuni hapa jiongeze, kuni kuu ulimwenguni

  zamani wanamme ndo walihesabiwa peke yao. Sasa Mzee X aliiba mke wa mfalme. Akatemwa kuni.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kunielewesha Kongosho, japo sijakupata vizuri hebu fafanua tena kwa lugha "rahisi"
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nilivamia hii Thread , nikidhani unaulizia "Ukuni" ! Kumbe "Mtema kuni"
  Hii siifahamu, niwaachie watu wa Mrima, naimani watakutosheleza.
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  huyu mzee ukuni ulikatwa akabaki mwanamme shati.
  Haku-qualify hata kuwa mwanamme suruali.

  Ndo maana ukionywa halafu husikii wanakuambia utakiona cha mtema kuni. Huyu mzee alionywa ila hakusikia.

  Nachoka kuandika kirefu.

   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kaka mara zote nikiona nyuzi zako nashawishika kuzisoma
  na mara zote nakosa chakuchangia ktk nyuzi zako...
  duh!
  ila kwa hili niliwahi kuckia japo akili imefuta, kuwa Mtema kuni ina maana ya mkata kuni. ...
  Moja ya simulizi za Mtema kuni nilizosimuliwa utotoni ni pale aliporudi nyumbani bila kuni
  lakini na jeraha la kuchomwa na mwiba mkali. .... and blah blah blah
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  nimekupata sasa Kongosho, lakini mbona hawasemi "ukuni" bali wanasema kuni?
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Kwa nini huwa unakosa cha kuchangia?? Asante kwa mchango wako.
   
Loading...