Utakapojenga Nyumba yako usisahau 2.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,030
50,932
UTAKAPOJENGA NYUMBA YAKO. USISAHAU 2.

Na. Robert Heriel.

Heri yule ayashikaye maneno yangu. Tena anaheri yule ayafanyaye. Basi mwanangu ukiyashika haya na kuyafanya utaishi maisha marefu yaliyojaa furaha.

Utakapojenga nyumba yako. Yenye ukubwa wa kukutosha. Wewe ni watu wa nyumbani kwako. Wewe na wageni wako. Na wanyama yako wa kufuga basi usisahau mambo haya. Tena uyashike na kuyafanya siku zote za maisha yako.

Usisahu kujenga ghala la kuhifadhia chakula. Utajenga ghala litakalohifadhi nafaka na mazao ya chakula. Ghala hilo liwe na uwezo wa kuhifadhi chakula cha zaidi ya miaka miwili. Utahifadhi Mahindi, Maharage, Mchele na aina yoyote ya chakula kwa kadiri ya upendavyo.
Ndio maana nikakuambia katika waraka ule yakuwa unapaswa ufanye kazi kwa bidii sana. Ili ujipatie akiba na chakula cha ziada kitakachokutosha wewe na watu wako. Tena upate na cha kuwapa wageni. Hakikisha uwe na shamba utakalokuwa unalima ili usinunue chakula. Kamwe usinunue chakula ikiwa Mungu wa baba yako alikupa ardhi ya kulima. Lakini kama utakiuka agizo hili ndipo utakapo pigwa na njaa mara kwa mara. Nawe utakopa kwenye maduka na majirani. Atakuja mgeni nyumbani kwako nawe utakosa kitu cha kumpa mkononi. Nawe utajiona masikini kwa kuwa ulishindwa kuwapa wageni kitu cha mkononi watakachoondoka nacho.

Mwanangu utakapo jenga nyumba. Usisahau kujenga Kisima cha maji. Utajenga kisima kwenda chini kitakachohifadhi maji. Iwe ni maji ya mvua yatakayotoka kwenyw Paa la nyumba yako au maji ya kuchimba kutoka ardhini au maji kutoka katika serikali. Hifadhi maji uwe na uwezo wa kutumia kwa miezi mitatu. Ili usije ukakaukiwa.

Ili hata majirani wakikosa maji uweze kuwapatia. Nayo nyumba yako itakuwa kama chemchem isiyokauka. Miti na bustani zitastawi mwaka mzima bila kukauka.

Mwanangu utakapojenga nyumba yako usisahau kuchimba shimo la kutupia takataka. Hilo utatupia uchafu wa nyumba yako. Hakikisha nyumba yako iwe inajitosheleza kwa kiasi kikubwa ingawa najua haitawezekana kwa asilimia mia moja. Kamwe usitupe taka taka hovyo.

Mwanangu utakapo jenga nyumba yako uweke sehemu ya kuanikia nguo zako wakati utakapozifua. Tena utenge na sehemu ya kufulia nguo zako. Ili nyumba yako ikae kwa mpangilio ukimtukuza Mungu wa Baba yako. Kwa Maana Mungu wetu ni Mungu wa Mpangilio.

Mwanangu Usichome takataka wakati wa Jioni au usiku. Bali choma taka taka wakati wa asubuhi ambapo watu wengi wameenda kazini. Lakini ukichoma wakati wa Jioni au usiku utawasumbua majirani zako kwani wengi watakuwa wamerudi nyumbani na wamepumzika. Usiwasumbue jirani zako Mwanangu. Halikadhalika na kufagia. Fagia Asubuhi tuu.

Mwanangu usiache Mifugo yako ikazurura mitaani hovyo. Ifungie kwenye mabanda. Au kama utashindwa basi ipeleke huko shambani. Mifugo inaweza kuwa kero kwa majirani zako. Hivyo ifunge kwenye mabanda yao ukiihudumie ndani kwa ndani. Ukiipa chakula na maji na mahitaji mengine ili isije kulia na kupigia watu kelele.

Mwanangu, Usije ukatumia pesa za dhuluma kujengea nyumba utakayokaa wewe. Fedha za wizi. Iwe umeiba kwa mtu au umemuibia Mungu wa Baba yako zaka na Sadaka. Usije ukanunulia chochote kile ndani ya nyumba yako. Iwe ni nondo, Au bati, au saruji, au Tofali au jambo lolote lile. Usijeiingiza hiyo fedha haramu kwenye ujenzi wa nyumba yako. Kwani ukiingiza utaiingiza nyumba yako katika Laana na mikosi.

Nawe utajenga nyumba lakini hautakaa. Utaoa mke lakini atakukosesha amani. Utazaa watoto watakupa huzuni nyingi. Nayo nyumba yako itaandamwa na magonjwa na maradhi. Itaandamwa na Majanga na Mikosi.
Nayo nyumba yako itageuka kaburi lako.

Itakuua nakuhakikishia kama Mungu aishivyo. Kama hutokufa kwa umeme, Basi utakufa kwa kuteleza kwenye sakafu. Au utakufa kwa kudondokewa na Mti au ukuta. Au jambo lolote ndani ya nyumba yako.

Naye mke
/mume wako atakugeuka. Naye ataiharibu nyumba yako. Ataleta mwanaume mwingine ndani ya nyumba yako. Tena ataiuza na kukunyang'anya kama wewe ulivyowanyang'anya wale uliowadhulumu. Mpaka utakapoangamia.

Tena wnayama utakaowafuga watakudhuru. Iwe ni mbwa, au Ng'ombe au mnyama yoyote yule. Mpaka utakapoangamia. Kwa kuwa uliasi amri ya mimi Baba yako.

Basi usifanye dhuluma ili upate ishi miaka mingi yenye furaha. Tena utaingia kaburini kwa furaha. Ukiwa na uzee mwema.

Mwanangu utakapomaliza kujenga nyumba yako. Kabla hujaingia na kukaa humo. Utafunga kwa siku saba. Lakini kama umeoa Mke wako atafunga pamoja nawe kwa siku tatu. Yeye akianza kufunga utakapofika siku ya nne ya kufunga kwako. Na ile siku ya Saba ya mfungo kwako na siku ya tatu kwa mfungo wa Mke wako. Mutamuita Mchungaji au kuhani, au shekhe au mtu yeyote yule ambaye anamcha Mungu sana. Nanyi mtaitakasa nyumba yenu. Wewe na Mke wako. Na kama mpo na watoto halikadhalika.

Mchungaji au shekhe atakayekuja mtampa zawadi kulingana na mlivyobarikiwa kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake.

Katika siku hizo saba utakazofunga naam ndizo siku tatu za mkeo atakazokuwa amefunga. Mtaombea mambo yale yanayopatikana Katika Kitabu cha Mwanzo Moja. Kila siku mtaombea kitu kimoja.

Kwa mfano siku ya kwanza. Mtaombea nyumba yenu Mungu atenge giza na nuru. Nayo nyumba yenu ijazwe nuru na giza liikimbie. Siku ya pili mtafuata hivyo hivyo kama ilivyo kwenye kitabu cha mwanzo.

Mpaka itakapofika siku ya sita ambapo mtaombea Wanyama wenu, watoto wenu, mali zenu na mtajiweka wakfu ninyi wenyewe na kuikabidhi nyumba yenu Kwa Mungu wa Baba yenu. Kama nilivyowausieni Mimi niliyebaba yenu kwa Damu.

Na siku ya Saba itakuwa siku ya ibada. Mtapumzika mkimtukuza na kumshukuru Mungu kwa kuwapa uwezo wa kujenga nyumba hiyo. Siku hiyo mtastarehe na kumsifu Mungu wa Baba yenu. Mtatoa ushuhuda wa yale Mungu aliyowafanyia kwa kipindi kizima. Kisha Mchungaji au shekhe au kuhani au mtu yeyeto ambaye anamcha Mungu ataendesha ibada na kuiweka wakfu nyumba yenu.

Kwa habari ya namna ya kula na kunywa katika siku hiyo. Mtakula kama Mungu wa Baba yenu alivyowaagiza. Muwe kama watoto wa Mungu wala msije mkahadaiwa na maneno ya Watu wengine. Kwa kuwa Mungu amewaweka hao ili apate kuwajaribu kama mtaasi sheria zake.

Katika siku hiyo mtaweka nyimbo za kumtukuza Mungu wenu. Kisha mtaweka na nyimbo nzuri za kitamaduni kulingana na utamaduni wenu. Msihofie ikiwa mtashika nililowaambia.

Kisha mtaenda kutoa sadaka kwa Watoto Yatima na Wajane. Kwa kadiri Mungu atakavyo wajalieni.

Wala Msimuogope Mungu wa Baba yenu ikiwa hamkutenda dhambi. Yeye ndiye Mungu wetu. Ndiye atakayekuwa pamoja nanyi muwapo katika mgongo wa nchi.

Mwanangu utakapojenga nyumba yako na kuishi na Mke wako. Msiue kiumbe chochote kile ndani ya nyumba yenu. Ikiwa mliona Panya tafuteni Paka. Ikiwa mliona mbu basi tafuteni popo au viumbe wowote walao mbu. Kamwe usiue kiumbe chochote kwa Maana hivyo viliumbwa kwa ajili yako ili vikusaidie.

Ikiwa utaona shida katika hili basi Muombe Mungu akuongoze lakini Baba yako nakuusia usiue kiumbe yoyote yule hata kama ni hatari. hata kama ni Nyoka au Nge au tandu. Nao hawatakudhuru.

Mwanangu utakapojenga hakikisha mnaishi kama Watoto wa Mungu aliyemkuu. Kuweni watu wenye kuonyesha ukuu wa Mungu popote pale mlipo.

Kwa habari ya Rangi ya Nyumba. Mwanangu utachagua rangi ipendezayo lakini iendanayo na hali ya hewa ya eneo husika. Ili usijeingia gharama kila mara. Zingatia ukali wa jua upakapo rangi ya nyumba yako na wingi wa mvua. Halikadhalika na Muelekeo wa madirisha kulingana na kuchomoza na kuzama kwa jua. Na muelekeo wa Upepo.

Mwanangu utakapojenga Nyumba. Usiingilie mambo ya mke wako. Mpe amri mkeo atakazozitekeleza. Mke wako ndiye awe Mratibu wa Mavazi ya hapo nyumbani kwa watoto na wewe mwenyewe. Wewe uwe kama muangalizi ikiwa anaenda vile Mungu wa Baba yako anataka. Yeye asimamie masuala ya ratiba za chakula katika nyumba yako. Usafi na kuwa kama mkaguzi wa mali za nyumba yako. Yeye ndiye atakuwa anafuatilia ubadhirifu wa mali na pesa. Japokuwa wewe ndiye utakuwa msemaji wa mwisho.

Mwanangu utakapojenga nyumba yako. Usikae nyumba moja wewe na mama yako au Baba yako kwa zaidi ya mwaka mmoja. Tena Mwambie mke wako wazazi wako wasikae nyumbani kwako zaidi ya mwaka mmoja. Labda iwe kwa sababu maalumu kama maradhi tena iwe umethibitisha hilo.

Mwanangu utakapojenga nyumba yako. Kamwe usimpokee mwanamke aliyekimbia ndoa yake. Iwe ni Dada yako au Dada wa mke wako. Iwe ni mama yako au mama ya Mke wako. Iwe shangazi yako au shangazi wa mke wako. Asikae hapo nyumbani zaidi ya siku mbili. Utamuambia aondoke. Wala moyo wako usiingie huruma fanya kama Baba yako nilivyokuamuru.

Mwanangu ikiwa ulizaliwa kama mtoto wa nje. Ukafanikiwa ukajenga nyumba. Na mama yako anataka kumkimbia Baba yako wa kambo ili aje kuishi kwako. Usikubali. Mwambie akae huko huko na Baba yako wa kambo. Aje kukusalimia lakini sio kumkimbia mume wake huyo. Kwani yuamkimbia Baba yako wa kambo kwa sababu yako. Kwa kuwa wewe unauwezo. Usiwe sababu ya kuvunja ndoa ya Mama yako. Tena Moyo wako usijeingia hila ukamshauri Mama yako amuache Baba yako wa kambo kwa kuwa sio baba yako. Hilo ni kosa na kama Mungu aishivyo.

Kamwe usichoke kusoma mausia ya Baba yako.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
 
Mkuu nakushauri andika kitabu baada ya fasihi yako kufika tamati
 
"Mwanangu, Usije ukatumia pesa za dhuluma kujengea nyumba utakayokaa wewe. Fedha za wizi. Iwe umeiba kwa mtu au umemuibia Mungu wa Baba yako zaka na Sadaka. Usije ukanunulia chochote kile ndani ya nyumba yako. Iwe ni nondo, Au bati, au saruji, au Tofali au jambo lolote lile. Usijeiingiza hiyo fedha haramu kwenye ujenzi wa nyumba yako. Kwani ukiingiza utaiingiza nyumba yako katika Laana na mikosi."

Baadhi ya maneno mazito sana toka kwenye andiko lako mkuu. Mwenye masikio na asikie
 
Imekaa vzr mkuu
Yes imebidi niisome yote, maana kadri nilivyizidi kuisoma ndo nilitamani kujua kinachoendelea mbele ya fasihi simulizi.

Lete nyingine tena haswa kuhusu vijana kuacha njia na kuiga maisha ya wasanii wa filamu na muziki. Huku wakidhani mile wanachoona kwa wasanii hao ni maisha halisi.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom