Utajuaje Ndoa yako imevunjika kisheria na ukaruhusiwa kuoa au kuolewa bila kwenda Mahakamani?

Don Nalimison

JF-Expert Member
Jun 26, 2020
647
1,000
MWANAMKE MPUMBAVU NA MWANAMME MJINGA ASIYEJUA SHERIA ZA NDOA YA TANZANIA.

Utajuaje kuwa Ndoa yako imeshavunjika Kisheria bila kwenda Mahakamani? Na ukawa huru kuoa au kuolewa. Nifuatilie Don Nalimison.

1. Mwanamke au MWANAMME anapobadili Dini, kisheria tayari Ndoa inakuwa imeshavunjika na Kutalakiana. Maana ule mkataba mliofanya ulikuwa wa Sheria nyingine mfano Sheria ya Kanisa au Mila au kiislam na hivyo unahitaji mkataba mpya wa Imani nyingine.

2. Mwanamke anapoolewa kwa mwingine au MWANAMME anapooa mwingine bila kufuata Sheria ya awali na mkataba wa awali, kisheria Ndoa inakuwa imeshavunjika na kutalakiana.

3. Mwanandoa mmoja anapo mtelekeza mwenzake kwa miaka mitatu bila mawasiliano, tayari kisheria inahesabika kuwa Ndoa imeshavunjika na hivyo uko huru kuoa au kuolewa.

4.Mwanandoa mmoja anapokutwa na Ugonjwa usiotibika Kama UKIMWI au TB au Kifafa au Kichaa hivyo Ndoa inahesabika kuwa imeshavunjika maana hakutawezekana kufanya tendo la Ndoa kama mmoja ana magonjwa hayo.

5. Mwanandoa mmoja anapofariki, tayari Ndoa inahesabika kuwa imeshavunjika.

6.Mwanamke akizaa nje ya Ndoa tayari Ndoa inakuwa imevunjika

7.Ndoa ni mkataba wa hiari na hivyo hiari inaweza kuvunjika. Don Nalimison nakutakia NDOA MPYA NJEMA YENYE MAFANIKIO.
 

xav bero

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
5,148
2,000
We mbulula ukioa au kuolewa una pewa vyeti viwili,kimoja cha serikalin na kingine cha dhehebu unaloabudu... Na yte haya ndoa haiwez kuvunjika mpk mmoja aridhie,,haswa mwanamke..Unadhan kuvunja ndoa ya kikristo shughuli yake ndogo tu?? Labda mmoja afe...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom