Utajuaje kuwa anakupenda au anakutumia tu....? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajuaje kuwa anakupenda au anakutumia tu....?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Apr 9, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu nisaidieni ni dalili zipi ambazo zitakufanya ujue mwenzio anakutumia tu (hana mapenzi ya dhati na wewe?)

  Nimeuliza hivyo kwa kuwa naanza kumhisi mtu wangu ndivyo sivyo sasa sijui ana kidosho kingine au ana sababu zake but recently nimegundua yafuatayo

  1. Simu yake ni yake na haeshi kubofya akituma sms
  2. Hununa bila sababu but atacheka na kukufurahia akisikia kuwa ninategemea kupata pesa flani toka mahali
  3. Mshahara wangu mimi ni wake anataka ajue every bit ulivyotumia
  4. Ikihappen akaona salary slip then baada ya muda akiuliza ukamwambia zimebaki kiasi flani ananuna.

  Ninahisi natumiwa au namjudge vibaya please kama kuna dalili nyingine naombeni kabla sijachukua uamuzi.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mume au boifrend MJ1?
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha huyo king'asti wake sijui wametambulishana au wanadandiana tu atatujuza tu.
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ebwana before ujatoa maoni kuhusu hiyo issue ni bora MJ utujulishishe huyo ni mwanandoa wako au bfriend tu? Nia ya mwanandoa na Bfriend hazifanani kabisa
   
 6. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Lakini pia inawezekana mwenzi wako ametambuwa kwamba kipindi hiki ni cha mtikisiko wa uchumi, so anaamua kufuatilia up to the last penny. Ndo maana akisikia inflow anashangilia coz under this economic meltdown, cash inflow ni bonge la good news MJ1!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Brooklyn,
  You have made my day maana nimecheka sana baada ya kuwa very serious the whole day.
  Sasa kama anashangilia cashflow ya MJ1 pale anaposikia king'ora cha ushindi kama kwenye kamari, na yeye je ya kwake inatoa au??
  Tusubiri Mj1 atujuze

  Samahani Mj1 usikasirike kwa vile tumetaka kujua undani zaidi ili tukupe maoni yetu.
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  swity ukimjibu WOS ndio 2tapata upanuzi wa kukujibu vizuri, hapo pengine ningekushauri ucpende kujihusisha napo sana, ndio mwanzo wa headache, kila mmoja ahucke na cm yake.
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mnahisigi mengi eeh, eti fidel?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yaani we acha tu kama huyo amesema cmu yake haiguswi ni bora abaki hivyo hivyo hata mimi nikiwa na g/f cmu yake sigusi kabisa nikupeana presha tu mi yake sigusi na yangu hagusi.
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mmoja wa wanaume wachache wenye msimamo huu.Wengi watataka kupekuwa simu za wake/wapenzi wao ila zao usiguse!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145

  Mi kwakeli siwezi pekua simu ya mtu ambaye nipo nae najua athari zake na ugomvi mwingi siku hizi kati ya watu wapenda nao ni simu.
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...anakuzingua tu, huenda anatumia calculator au anacheza games kwenye simu yake, usinune!

  ...anachekelea wewe kujiwezesha 'kiuchumi'

  ...ndio tatizo kuoana na wahasibu!

  ...ndio, karaha zao ma auditors hiyo!

  ...hapana, wala usijikondeshe. Uamuzi wa busara ni kumpa risiti zote za matumizi, muache ajiumize kichwa kubalance mapato na matumizi ya mwezi mzima na hata mwaka mzima akitaka.
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni Mtu ambaye tunatarajia kufunga ndoa rasmi July 2009. !!
   
 15. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Shoga huyo hata kama ni bf au mume HAFAI!

  1. Akibofya ya kwake na wewe chukua yako ubofyebofye
  2. Hiyo ni dalili tosha ya userengeti boy...halafu usipende sana kumhusisha mwanamme kwenye madilii yako. Heri sema umekopa pesa hata kama ni zako.
  3. Hapa no way...unless na yeye wake unaujua everbit...otherwise stop that.
  4 Salary sleep tafuta vile vibox vya chuma vya petty cash weka salary slip zako huko na uzifungia kwenye kabati lako offisini...unless na wewe unaona mshahara wako basi endelea kufunulia aendelee kununa.

  Kweli unatumiwa na inaonekana pengine umezimia mapigo ndo maana yote haya yamekutokea. It happened to me once na nilijivundisha...baada ya kufilisiwa kabisaaa...so dont end up like me. All the best
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Brook huyu ni mwenzi ambaye tuko naye kwenye serious relationship (or what seems to be as one) ninayetarajia kufunga naye ndoa katikati ya mwaka huu. Bahati mbaya tulianza kwa kuvutana tu tukajihalalishia.
   
 17. M

  Mrs Mtaba Senior Member

  #17
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 21, 2009
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa maanisha nini, fafanua sentesi zako vizuri upate msaada mzuri kwa manufaa yako.
   
 18. Violet

  Violet Member

  #18
  Apr 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamme akianza mambo ya kuomba omba hela achana naye. Wanaumme wengi sikuhizi hamna aibu tena, kuchomoa tuu wanawake, halafu anatunisha mabega juu. Kama yeye hashirikishi kwenye mambo ya hela zake, usimshirikishe kabisa kuhusu yako.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...Oooh, kumbe ni mume mtarajiwa!

  ushauri wa bure,...huenda vyote ulivyotaja ni vijitabia ambavyo huyo fiancee wako alikuwa amevifumbia macho. Kadri mnavyoelekea kwenye 'pingu za maisha', kidogo kidogo anaanza kukuonyesha nini anapendelea na nini hapendelei.

  Si kitu mbaya Yeye kukuonyesha hayo, ni bora yule anayekuonyesha anajali, kuliko yule ambaye hakuonyeshi ishara zozote halafu siku ya siku anakuja kung'aka kwa jinsi ulivyomtumiaji vibaya hela ya familia.

  Nawe kama hupendezwi na hiyo mobile fone, mwambie na mapeeeema, asije huko mbele ya safari akajakwambia, "mbona kabla sijakuoa hukulisema hilo?"

  Ndoa raha, ...ukishamjua mtu wako, mambo yake yanakuwa transparent kama chandarua vile :)
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  sijajua uko upande gani wa jinsia. mimi niko upande wa kiume. kuna mshkaji wangu kanipa stori jana eti kuna jamaa alikuwa na demu wake. sasa siku moja jamaa akachukua simu ya demu wake akajibip, la haula wa lakuwataa!! jina likatokea eti ATM! gelo frend wako anakusevu hivyo kwenye simu yake! enewei, matendo yataonyesha kama unatumiwa au mnapendana
   
Loading...