Utajisikiaje upoambiwa?

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,597
Kwa wale ambao wako kwenye ndoa au mahusiano, kuna wakati mwenzi wako anakusimulia kuwa mtu fulani (ama unamfahamu au la) amemchokoza kwa kutaka wawe na mahusiano ya kimapenzi (amemtongoza). Kuna watu wanadhani kwamba kuambiwa kitu cha namna hiyo inaonesha kuwa mwenzi wako ni mwaminifu na kutoambiwa ni kinyume chake. Binafsi sipendi kuambiwa ila kuna wakati natamani (kama binadamu) kujua kama hayo yanamkuta mwenzangu na akina nani wanamtokea, ingawa kiukweli najua yanatokea. Je wewe unapenda kuambiwa?
 
sijui kama napenda kuambiwa au sipendi but ol I knw ni kwamba kumwambia mpz wako kuwa kuna jamaakakutongoza ni kwamba huyo jamaa hukumpenda na wala huna interest nae but ungekuwa unampenda n una interest wala husingesema.
 
Huo ndo wasi wasi wangu mkubwa kwamba kuambiwa ni kanyaboya, akimpenda hatakaa akwambie. Ndo maana mimi nachunga mzigo wangu. Nikiona danger signs au moyo wangu ukinambia kitu nashughulika mwenyewe. Kusubiri akwambie lazima utapewa news za kichina tu! Hata hivyo wanaume wengi huwa hawasemi hayo mambo kwa sababu wengi wetu ndo tunawatokea wanawake. Waliowahi kutokewa mara nyingi watatuelimisha. Binafsi sitokewagi au kama natokewa sijui!
 
Woga tu ndugu kwani ww nawe culimtongoza ndo ukampata? kama kweli analipa atatongozwa daily na akikwambia kila akitongozwa utamfungia na kazi utamwachisha ww vumilia tu........kama ni mwaminifu shukuru.......lol?
 
Halafu wanawake kwa jinsi walivyo, hata kama kaolewa asipotongozwa tongozwa mara kwa mara hajisikii vizuri.
 
Mie sipendi kuambiwa ingawa najua hivi vitu vinaweza kuwepo
Issue ni kwamba akitongozwa/akitongoza kiukweli na akakubali kwani atakuja kuniambia ??
 
Akitongozwa ki ukweli naye akavutiwa hawezi kuja kukwambia, watamalizana tu huko huko! Ndio maana mambo mengine huwa tuna ''assume'' kwamba uko peke yako na hakuna mwingine! Ili maisha yawe rahisi na yasiyo na pressure!
 
na wanaume walicvyo hata kama wameoa, wasipotongoza tongoza marara kwa mara wala hata hawasikii raha.
 
wanajickia kama malaria malaria vile? we masaki...

icon10.gif
Jamani laaziz si kweli lakini? Maana hiyo nimeipata toka kwa wanawake wenyewe!

Kuna dada mmoja alikuwa analalamika kwamba mimba imemfanya awe na sura mbaya na kukosa mvuto kiasi kwamba hatongozwi kabisa. Yaani eti kipindi chote alichokuwa na mimba aliwahi kutongozwa na mwanaume mmoja tu, tena mwanaume mwenyewe alikuwa kalewa!
icon10.gif
 
sijui kama napenda kuambiwa au sipendi but ol I knw ni kwamba kumwambia mpz wako kuwa kuna jamaakakutongoza ni kwamba huyo jamaa hukumpenda na wala huna interest nae but ungekuwa unampenda n una interest wala husingesema.

Hivi Peal umeolewa??? maana nakugongea thanks lakini wewe daaa!!!!
 
Akitongozwa ki ukweli naye akavutiwa hawezi kuja kukwambia, watamalizana tu huko huko! Ndio maana mambo mengine huwa tuna ''assume'' kwamba uko peke yako na hakuna mwingine! Ili maisha yawe rahisi na yasiyo na pressure!

You assume everything is at standard temperature and pressure na maisha yanaendelea au vipi mkuu.Na ukigundua signs of changes,kama alivyosema mkuu DC you work out to resume the ideal condition.
 
Hivi mtu unaweza kusubiri kusimuliwa kama jua litachomoza au litazama? tangu mtoto wa kike anaanza kukimbia kimbia anaanza kuambiwa maneno ya kutongozwa (hey mchumba..!) na anapoanza kuota manyonyo ndio kabisa, na akianza kupata balehe ndiyo inakuwa ugomvi.. haijalishi msichana anakuambia au hakuambii ukweli ni kuwa atatongozwa akienda sokoni, akienda kanisani, akikaa darasani, akipita ofisini n.k

Mtoto wa kiume hivyo hivyo naye atatongoza hata migomba alimradi imekaa kimapenzi mapenzi..

so that given; mwisho wa siku ni uamuzi wa mtu kukataa au kukubali. Mwanamke utatongozwa kila wakati na kila mahali hata ujifanye mkali kama simba; lakini unayo nguvu yakukubali au kukataa. Ukikubali au ukikataa yote yanakuhusu wewe zaidi lakini yana gharama kubwa kwa mwenzio; na mwanamme vile vile.. unaweza ukaamua kumtongoza fulani au kutomtongoza au kukubali kutongozwa na mtu au kutokutongozwa lakini uamuzi wowote una gharama kwako na kwa mwenzio.

Mwisho wa siku (sijui kama ni siku ile ile!) tafuta na upate mtu atakayekupenda na ambaye kwake wanaume/wanawake wengine wote hawafui dafu. Kama unaye ambaye anazidiwa na mtu mwingine basi utajiunga katika ile clabu ya "wale"..
 
kweli kabisa....ni uamuzi wa mtu mwenyewe..haina mjadala hii
 
mimi naweka wazi

hahaha mie naona kama utoto Original Pastor

Na imagine nimetoka sokoni /church or saloon namketisha kitako mwenzangu ooh swetie za muda tena ...mmh mwenzio nikwambie leo kuna jamaa kanitongoza ,,kanambia nakupenda vile ulivyo hata kama uko double or single ...
moyo wangu umezaliwa kwa ajili yako dada FL1

hehehe nadhani hata yeye atajiuliza huyu kawaje leo ??
 
Halafu wanawake kwa jinsi walivyo, hata kama kaolewa asipotongozwa tongozwa mara kwa mara hajisikii vizuri.

Kutongozwa tongozwa hiyo inawezekana kwa sababu watogozaji ni sisi wanaume. Ila hiyo ya kujisikia vizuri au la sina hakika nayo. Nadhani ni suala la mtu binafsi labda wenyewe waseme!

Mie sipendi kuambiwa ingawa najua hivi vitu vinaweza kuwepo
Issue ni kwamba akitongozwa/akitongoza kiukweli na akakubali kwani atakuja kuniambia ??

Hapo kwenye red, kitu kama hicho kitakurusha roho sana. Imagine unaambiwa anayemtokea mtu wako rafiki yako kipenzi. Usingizi utapatikana kweli?
Hapo kwenye blue; moyo siyo transparent, kwa hiyo kila mtu abebe msalaba wake kwenye hilo ingawa mengine tunaweza kusaidiana.

Akitongozwa ki ukweli naye akavutiwa hawezi kuja kukwambia, watamalizana tu huko huko! Ndio maana mambo mengine huwa tuna ''assume'' kwamba uko peke yako na hakuna mwingine! Ili maisha yawe rahisi na yasiyo na pressure!

Hiyo ndiyo naita "kanuni ya imani". Huna sababu ya kuhisi kuwa mwenzio anakuhujumu hadi upate uthibitisho pasi na shaka. Usilolijua halikunyimi usingizi, ingawa unaweza kuwa unaibiwa.

na wanaume walicvyo hata kama wameoa, wasipotongoza tongoza marara kwa mara wala hata hawasikii raha.

Siyo wote. Wengine tunatamani lakini tunarudisha sime kwenye mikoba yake na kusonga mbele. Kwa hiyo huwezi ku-generalize.
 
sijui kama napenda kuambiwa au sipendi but ol I knw ni kwamba kumwambia mpz wako kuwa kuna jamaakakutongoza ni kwamba huyo jamaa hukumpenda na wala huna interest nae but ungekuwa unampenda n una interest wala husingesema.

HAYO MANENO YA KWELI PEARL. Aakimkubalia hawezi kusema
 
Halafu wanawake kwa jinsi walivyo, hata kama kaolewa asipotongozwa tongozwa mara kwa mara hajisikii vizuri.

kumbe kutongozwa kuna raha yake eeeh!!!! (nahisi kama ilivyo kwenye kutongoza)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom