Utajisikiaje ukiwa na mdogo wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajisikiaje ukiwa na mdogo wako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Afrika Furaha, Dec 17, 2010.

 1. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utajisikiaje ukiwa umeongozana na mdogo wako uliyemzidi miaka kama 8 hivi, mnaenda sehem mnakutana na watu tofauti lakin cha ajabu wakimuona dogo lako wanamwamkia SHIKAMOO Bro, anapewa na kiti akae, halafu wewe unapewa MAMBO VP MSHIKAJI halafu unaambiwa WE BADO KIJANA MDOGO SIMAMA KIDOGO ULE TIZI UKOMAE . . .?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Nitajisikia vizuri mno. Nitawashukuru wazazi wangu kwa kunirithisha "genes" nzuri ambazo zinanifanya nionekane bado yanki kuliko umri wangu wa kweli.

  Nani anayetaka kuonekana kama ana miaka 50 wakati umri wake ni miaka 30? Si mimi...labda wengine.
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Sorry naona kama vile mnanitania... nitawapiga ban fasta
   
 4. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahahahah . . . una sura ndefu nini?
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Hua inatoke tu mpwa, si ndio maajabu ya mkuu wa wakuu?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kama una ego kubwa, na unahusudu ukubwa utakasirika.

  Kama unaelewa vitu kwa kina zaidi utacheka na kushukuru kwamba huonekani kuzeeka mapema.

  Wakati wengine wanatumia pesa nyingi sana ili waonekane vijana bado, wengine wanakasirika kwa sababu wanaonekana vijana bado.

  Ni vijimambo vya maisha tu.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Senkyuuuuu
   
 8. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikitokea mara moja unaweza kucheka, lakin ikiwa inatokea kila mara inakera bwana . . . mbali na kusema huonekani mzee lakin UNADHALILIKA MBELE YA WATU . . . ipo siku itakutokea mbele ya mkeo au mkweo . . . sijui napo utaona kawaida?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Huenda pia hili jambo ni la tofauti za kiutamaduni maana kwenye nchi magharibi watu wanajidunga botox kuondoa makunyanzi ambayo ni alama ya uzee.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Fikra kwamba unadhalilika mbele ya watu inatoka wapi? Au tunahalalisha kudhalilisha wadogo?

  Mimi ni kaka mkubwa kwenye familia, na sina tabia ya kutaka kuabudiwa kwa sababu ya ukubwa, naongea na wadogo vizuri tu na kuwaheshimu wote sawa tu.

  Tatizo kubwa linajionyesha hapa ni kwamba tunadharau wadogo. Nelewa kuhusu umuhimu wa kuthamini busara zinazokuja na umri, lakini je hili linamaanisha kwamba automatically udogo ni wa kubezwa?
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Shikamoo mwanangu!
   
 12. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nadhani umeenda mbali kidogo, udogo haubezwi ila unatakiwa upewe heshima stahiki, ukubwa nao upewe heshima stahiki. Udogo hauheshimiki kwa kuibia heshima ya wakubwa . . . udogo ukubali kuwa udogo tu
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Sasa kwa nini mtu ajisikie vibaya kuonwa mdogo ? Au ndiyo habari ya kupenda ukubwa niliyoitaja juu?

  Hata manabii wamesema anayejikuza hushushwa, anayejishusha hukuzwa. The rejected stone is now the cornerstone, sorta like the masterbuilder when I make my way home.

  You know my steez.
   
 14. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwani kuwa mkubwa ni kujikuza? Ukubwa wa umri sio cheo cha kazin kwamba unaweza kushushwa au kupunguzwa. Unaweza ukamdharau mkubwa lakin KAMWE huwezi punguza umri wake. Pia unatakiwa ufaham kuwa hapa sio kwamba mkubwa atamchukia mdogo kwa tukio walilofanya wengine, badala yake ni challenge kwa jamii kutotambua mtu kwa kuangalia sura . . . sijui unanielewa?
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kama unaelewa hili tatizo liko wapi?

  Jamii inaweza kuchukulia mkubwa ni mdogo na mdogo ni mkubwa kwa mujibu wa muonekano, ama sivyo itabidi tutembee na vitambulisho vyenye tarehe ya kuzaliwa na kuvionyesha kila tunapoenda ili watu wasituchanganye.

  Wewe tatizo lako hasa ni nini? Unaona kuambiwa mdogo ni kudharauliwa au vipi ?
   
 16. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona kama una JAZBA fulani hivi, au pengine una lako jambo hapa. Ulipoingiza maneno KUTEMBEA NA VITAMBULISHO VYENYE TAREHE ZA KUZALIWA ulinifanya nikufikirie mara mbili-mbili uwezo wako wa kuoanisha mambo? Na bado unaniuliza KUITWA MDOGO NI KUDHARAULIWA AU? Naona hatulingani uwezo wa kufikiria . . . iache tu mada ipite
   
 17. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  toka haraka hapo umeingia choo cha kike
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nitafurahi....
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Dec 18, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaaah!! Huyu ni mgeni!
   
 20. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  If you can YOU CANT convince ME . . . . umejitahidi kijana kwa uwezo wako wa kujibu hoja
   
Loading...