Utajisikiaje ukijua umemletea mwenzio UKIMWI au Magonjwa ya zinaa hali yeye alikuwa ametulia? Kama ni mama yawezekana alikuwa ananyonyesha na mtoto alizaliwa mzima lakini baadaye kwa kuwa bado ananyonya na yeye anaathirika. Imemtokea jirani yangu ni mama alijifungua akiwa salama na mtoto alikuwa salama juzi kagundua mume amempa mimba mwanamke mwingine jirani ambaye inaesemekana ameathirika na UKIMWI. ikabidi mke akapime na mwanae ana mwaka mmja na nusu wote wamekutwa wameathirika.