Utajiri wa Wahubiri Nigeria balaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Wahubiri Nigeria balaa!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Jun 15, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,219
  Likes Received: 3,779
  Trophy Points: 280
  Bbc Swahili
  15 Juni 2011 13:00

  ?


  Wahubiri wa Nigeria wamefanikiwa katika miradi yao na kuwa na utajiri unaolinganishwa na matajiri wanaofanya biashara ya mafuta.

  Kwa mujibu wa muandishi wa blogu moja huko Nigeria aliyefanya utafiti wa wahubiri hawa wa neno la Mngu ameiambia BBC kuwa wana Biashara kabambe utadhani wana visima vya mafuta.

  Mfonobong Nsehe, mwandishi wa blogu ya jarida la kibiashara la Forbes anasema kuwa ma- pastor wanamiliki biashara kubwa kuanzia hoteli kubwa hadi biashara za chakula, mfano wa vyakula vya haraka kama vile 'nyama na kuku'' sawa na Kentucky' ambazo ni vivutio kwa familia na vijana.

  Mwandishi huyu anasema kuwa"Uhubiri ni biashara kubwa. Faida yake ni sawa na biashara ya mafuta ya petroli.

  Alitowa mfano wa utajiri wa Wahubiri watano ambao wana takriban dola milioni 200m.

  Kanisa za wahubiri wa aina hii zimeimarika nchini Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, ambapo maelfu kwa maelfu wameshiriki na kujiunga nazo.

  Bw.Nsehe anasema Mhubiri anayeongoza kwa utajiri, Bishop David Oyedepo wa Kanisa lijulikanalo kama Living Faith World Outreach Ministry, alikadiriwa kuwa na utajiri wa takriban dola milioni150.

  Bishop Oyedepo anamiliki kampuni ya kuchapisha, Chuo kikuu, shule moja ya msingi ya kifahari, ndege zake nne za binafsi za kifahari na nyumba kadhaa mjini London na Marekani.
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Lol! Ndo maana Lusekelo huwa anatoa povu kumbe anajua siri ya hiyo kitu na akaunti zote za kanisa zina jina lake. Duhu 'MS'
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama ni kuhubiri tu na wewe unaweza kwani ni kazi rahisi sana unaweza kujaribu ili uwe millionear
   
 4. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sio tu kuamka na kuanza kuhubiri, wenzetu wana nguvu ya ziada ya kuvuta watu pamoja na miujiza, Mungu wakweli hapo hakuna zaidi ya ushetani
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mapopo nuksi sana. Wauza unga
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kumbe Wahubiri ni MATAJIRI kuliko MASHEHE,

   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Usiende mbali na kuwasakama hao preachers wa kipopo. Jiulize mbona hapo bongo kuna mega churches na wahubiri wake wako vipi? Wanajificha tu lakini ukichimba sana nasikia ni matajiri kuliko hao popo. Anzia na hapo Mikocheni kwa mbunge wetu..........
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wivu wa wafuasi wa allah kiumbe. Ha ha ha ha ha ha

  Maislam subirini misaada kutoka umangani kwa allah wenu. Kanzu na Ndala na tasbihi, ha ha ha ha, Ooops MIKEKA, ha ha ha ha, deen ya allah inatia aibu kweli kweli

   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe umeona tatizo gani ?
   
 10. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  It's all about the truth. Mimi sio mkristo wala muislam. Usichume dhambi za buree kuwasakama muslims wakati naongelea ukweli hapa.I'm just a believer!!
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Dini ni biashara siku hizi!huoni mwingira anavyotangazia benki yake?
   
 12. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Bilieving what? Tell us pls. Au ndiwe freemason?
   
 13. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ulitaka atangaze tende na halua?
   
 14. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  I believe in God. Hayo ya kuwa Freemason may be wewe ndo wayajua.
   
 15. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mimi ni mfuasi wa Kristo, sikubaliani na uchokozi dhidi ya waislam,why unalete hoja au mada zisizokuwepo kwenye thread? Mods do the needful , I am sorry Muslims sio Wakristu tulivyo hao wana magamba
   
 16. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Weye ni pagani? Believer of what?
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  I believe in GOD
   
 18. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Where in the Bronx do you go and worship God? Soundview? South Bx, Pelham, pale Brackner close to KMart?
   
 19. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakweli nimekubali hawa ni matajiri! Vip mwingira nasikia nae nitajiri hebu mwenye data atumwagie hapa!!
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  utajiri wa mali na tamaa ya macho ndio silaha kali mikonono mwa shetani kuliko silaha nyingine yoyote ile. Alimpandisha Bwana Yesu mahali pa juu ambapo angeweza kuziona falme zote za dunia na kumuahidia kama atamsujudia angemkabithi hizo. Yesu alimwambia nenda zako shetani, kwani imeandikwa 'msujudie Bwana Mungu peke yake na umwabudu yeye'
  Sasa hawa wahubiri hybrid wa leo, hakuna asiefahamu kuwa wamesujudu kwa yule mungu wa dunia hii. Japokuwa wanalitaja jina la Yesu lakini ndio wale Bwana atakaowaambia ondokeni kwangu sikuwahi kuwatambua kamwe. Wana nguvu nyingi za kiroho lakini ukiwapima ktk kipimo cha neno, hawasimami kabisa. Hakuna jibu sahihi kwao ila 'mawakala wa shetani'. Waulize ni nani kiongozi billionea miongoni mwa wanafunzi wa Yesu kuanzia wakati alipokuwepo duniani na hata baada ya kuondoka? Yaani matendo ya mitume?. Watakimbilia kwenye kina sulemani Daudi, ibrahimu nk bila kutambua kuwa utajiri wa watu hawa ulitokana na kazi zao za kawaidi nje ya utumishi wa Mungu(sadaka). Watumishi matajiri tulio nao leo ni matajiri wa sadaka za waamini huku waamini wenyewe wakiwa masikini wa kutupwa.
  Mungu wa kweli sio mtesi kwamba aruhusu mtu kuwa tajiri wa kupindukia katikati ya masikini waliopindukia. Ndio maana kiongozi wa kiroho wa injili ya Yesu hawezi kuwa bilionea wa sadaka za masikini wasiojiweza. Lazima wajane wote, yatima wote na masikini wote katika kusanyiko lake watengamae kabla ya yeye kuanza kujilimbikizia katika mabenki ya ndani na nje. Watu hawa wanahubiri habari za ujio wa Yesu punde tu, huku wakiwa radhi kunyanganya hata cent za mjane na kwenda kuzichimbia Bank. Ingekuwa kweli wanaamini wanachokihubiri wangejilimbikizia hazina duniani tena kijinai?
  Ona katika kanisa la mitume hakukua na kitu cha mtu peke yake, bali walikuwa na kila kitu shirika. Jiulize yule Roho wa kiwango cha wakati wa mitume kimepotelea wapi? Ni mbwa mwitu wakali waliolivamia kundi wabinafsi kama shetani mwenyewe alivyo na kwa ubinafsi huo wa kutamani kila kitu kiwe chake, wamelirarua kundi.
  Chunguza roho ya ufisadi iliyolikumba taifa kwa sasa, kama hutakuta kwa asilimia kubwa zaidi imechangiwa na mafundisho potofu ya utajirisho kutoka kwa mawakala wa shetani.
  Sipingani na juhudi zozote za kujipatia kipato hata kidogo, napingana na utajiri haramu nyuma ya kivuli cha utumishi. Huu ni wizi unaopaswa kupingwa kwa nguvu zote. Ijulikane pia kuna mgawanyo katika kazi na huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja yaani Mungu na mali.
   
Loading...