Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,265
- 105,432
Inaelekea unadanganyika kirahisi sana.Namkubali sana Magufuli , kwanza ni kwa sababu naamini ni mdau wa siasa ya ujamaa na azimio la Arusha.
Naamini anatatizika viongozi wa Serikali wanapozipata mali bila kuwa na chanzo elekezi.
Hawa vijana mfano mzuri RC wa Dar na yule wa Manyara bwana Mnyeti wana siri gani.
Je, ukuu wa mkoa unalipa sana?
Mnyeti kanunua timu na kutengeneza uwanja mfano wa azam complex kwa kiasi kinachokaribia na Bil 1
Makonda naye anasema ametumia bil 2 kuwapa viwanja Yanga na TFF.
Ninachojiuliza hawa kama watumishi wa umma japo wapo kwenye siasa wanafanya biashara gani ya kuwawezesha kugawa billions of money na wakiulizwa wanatoa sababu rahisi sana.
Natatizika hapa.
Na hapo ndipo mwanzo wa tatizo.
Magufuli angekuwa mdau wa siasa za ujamaa na Azimio la Arusha asingeuza nyumba za serikali nje ya mchakato rasmi.
Umekosea kutoka mwanzo kufikiri Magufuli ni mdau wa Ujamaa na Azimio la Arusha mpaka kushangaa vijana wake wanavyopiga hela.