Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Mkuu uchawi usukumani ni kama secret society zinavyofanya kazi forbidden knowledge zote ndio zimepelekea secret society ndio maana unasikia vikongwe wanakatwa mapanga ukihusishwa na uchawi. Uchawi pia unavyeo/ranks wale first class/highest rank ndio wanajua mambo makubwa.
Kwa walio kulia usukumani I.e mwanza, geita, shinyanga, tabora wanaweza kuwa wameskia au kushuhudia mtu aliyekufa baadae akarejea mara nyingi wanolejea hawajakatwa ulimi ndio wanasimulia mambo ya huko japo sio wote hupelekwa huko.
Sehemu niliyo kulia ilikuwa kawaida kusikia milio ya treni ikihusishwa na gamboshi.
Gamboshi ni kama taifa kule utaambiwa kuna wanasiasa wakubwa e.g Nyerere, kuna wachumi wakubwa I.e lipumba, kuna wanasayansi, walimu, shule, hospitali nk.
Nikawaida usukumani mme kuishi na mwanamke mchawi lakini asijue, usiku analala na fisi mkewe anaenda vilingeni.
Uchawi una operate kama secret society kwa sababu ya kuwakat mapanga na mara nyingi hata familia yenye uchawi unakuta anayejua ni mama na binti yake kwa sababu ndiye atakaye mrithisha na hao wengine ni ngazi ya kupanda daraja atakapo watoa kafara.
Kuna baadhi ya vijiji huko usukumani hukuti mzee(above 60) ni wabibi tu na vijana.
Ukiwa hauna kipaji unaenda kufanya manual work ndio hao wanaokatwa ulimi.
Lastly Gamboshi kwa wachawi ni kama sehemu takatifu mostly wa wale wanaoenda huko ni wenye loyalty ya highest order kwa hiyo sio rahisi kukwambia habari za huko.
Kuna padre mmoja alikuwa paroko mwadui father Deo alikuwa anafanya research yake kuhusu hayo mambo ya uchawi usukumani nadhani aliandika kitabu sijajua kama alikiweka public.
Kama wazazi au mzazi ni mchawi mtoto huwezi jua kamwe, labda yule aliyeridhishwa vinginevyo wale wengine wataitwa wajinga hata kama huyo walimpa ndiye anaonekana mental lakini kumbe anawakengeza tu
 
Kuna jamaa yangu Mpemba mmoja hivi ana daladala(Nissan Civilian)zake kibao mjini, ana duka la simu pale Aggrey na pia ana Bakery maeneo ya Ilala Bungoni. Yeye tabia yake huwa analaza PESA chooni wiki moja kabla kwa ajili ya kuwalipa mshahara wafanyakazi wake.
Halafu utegemee hao watu hizo pesa zije kuwasidia wao? hawapokei kitu hapo dhamani ya pesa inakuwa tayari ishaondolewa
 
Naona kama uandishi wa Lwanda magere na Master Umughaka unaendana.

Ila Lwanda alijua kutaabika aisee
Akaenda Kigoma,akaenda Kongo
Mara akazama ziwani Tanganyika
Yaani heka heka kama zoote

Bado tego zake barabarani za kuangusha magari,.mara Mbeya,mara Mbozi,mara Tukuyu.

Hii stori ya Umughaka imenivutia na nimeweza kusoma.
Ni stori yangu ya pili kuifuatilia.
Ya kwanza ni ya huyo Magere.

Mimi si mzuri sana kwenye kusoma soma hadithi.
Hadi nimesoma basi waandishi wapo vizuri.

Salute kwako mwamba UMUGHAKA .

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba unitag hiyo story ya Magere sijui

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uelewa Wangu(Low thinking capacity)

Ally mpemba alikua anaitumia nyota ya UMUGHAKA kukamilisha mambo yake ya kujipatia utajiri, yaani kulikua na Connection kubwa sana kati ya pete aliyoivaa Master na ally mpemba mwenyewe.

Na ndio maana Master alikua akizingua tu Ally mpemba na yeye uku mambo hayaendi poa kiasi cha kumchukia kabisa Master.

Refer pia kuna Sehemu Ally alimlalamikia Master kwamba anataka kumfanya Maskini. Pale master alipovunja Mashart ya kutopakia mtu asiye wa ukoo wa Ally siti ya mbele

Master alikua amelibeba jini la Ally mpemba na ndo lilikua linampa Blindness ya kumpa pesa kidogo kusudi asishtukie mchongo mzima. Alikua akitumika kama chambo na pia kama Ndoano.

Utajiri una siri nyingi sana Wajameni na madubuwasha ya Ajabu. Usipo ya Face huwezi kuelewa kamwe.
Huo ndiyo ukweli kabisa.
 
Mkuu uchawi usukumani ni kama secret society zinavyofanya kazi forbidden knowledge zote ndio zimepelekea secret society ndio maana unasikia vikongwe wanakatwa mapanga ukihusishwa na uchawi. Uchawi pia unavyeo/ranks wale first class/highest rank ndio wanajua mambo makubwa.
Kwa walio kulia usukumani I.e mwanza, geita, shinyanga, tabora wanaweza kuwa wameskia au kushuhudia mtu aliyekufa baadae akarejea mara nyingi wanolejea hawajakatwa ulimi ndio wanasimulia mambo ya huko japo sio wote hupelekwa huko.
Sehemu niliyo kulia ilikuwa kawaida kusikia milio ya treni ikihusishwa na gamboshi.
Gamboshi ni kama taifa kule utaambiwa kuna wanasiasa wakubwa e.g Nyerere, kuna wachumi wakubwa I.e lipumba, kuna wanasayansi, walimu, shule, hospitali nk.
Nikawaida usukumani mme kuishi na mwanamke mchawi lakini asijue, usiku analala na fisi mkewe anaenda vilingeni.
Uchawi una operate kama secret society kwa sababu ya kuwakat mapanga na mara nyingi hata familia yenye uchawi unakuta anayejua ni mama na binti yake kwa sababu ndiye atakaye mrithisha na hao wengine ni ngazi ya kupanda daraja atakapo watoa kafara.
Kuna baadhi ya vijiji huko usukumani hukuti mzee(above 60) ni wabibi tu na vijana.
Ukiwa hauna kipaji unaenda kufanya manual work ndio hao wanaokatwa ulimi.
Lastly Gamboshi kwa wachawi ni kama sehemu takatifu mostly wa wale wanaoenda huko ni wenye loyalty ya highest order kwa hiyo sio rahisi kukwambia habari za huko.
Kuna padre mmoja alikuwa paroko mwadui father Deo alikuwa anafanya research yake kuhusu hayo mambo ya uchawi usukumani nadhani aliandika kitabu sijajua kama alikiweka public.
Hii comment ilinipitaje mazee?... mbna inatupeleka mbali na kuzua maswali zaidi.. em tiririka mkuu nna maswali yangu hapo
 
UMUGHAKA vipi kuhusu fedha za benk ulizoweka kama akiba?!

Vipi kuhusu mawasiliano na Ally Mpemba?

Fedha za kila mwisho wa mwezi kupitia pete ile, zilikuwa zinakifikiaje?! Mfukoni, benki au ndani unazikuta zimewekwa?!

Ufafanuzi tafadhari
 
Naona kama uandishi wa Lwanda magere na Master Umughaka unaendana.

Ila Lwanda alijua kutaabika aisee
Akaenda Kigoma,akaenda Kongo
Mara akazama ziwani Tanganyika
Yaani heka heka kama zoote

Bado tego zake barabarani za kuangusha magari,.mara Mbeya,mara Mbozi,mara Tukuyu.

Hii stori ya Umughaka imenivutia na nimeweza kusoma.
Ni stori yangu ya pili kuifuatilia.
Ya kwanza ni ya huyo Magere.

Mimi si mzuri sana kwenye kusoma soma hadithi.
Hadi nimesoma basi waandishi wapo vizuri.

Salute kwako mwamba UMUGHAKA .

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo uzi wa Magere upo hapa JamiiForums??
 
Duh imeniuma sana japo siwez sema ni hvyo ila nimenikumbusha mwaka jana mwezi wa sita (6) mdogo wangu wa kike nae alikuwa anafanya kazi kwenye mgahawa posta ..siku alirud nyumban kaingia bafuni kuoga ile anataka aanze kuoga akahis kizungu zungu akaghahir kuoga akawa anarud chumban kwanza apumzike ile kafika mlango wa chumban kaanguka pale pale
Tukambeba na kumuwahisha rabininsia hospital pale tegeta
Akalazwa siku nne gharama sana pale tukamwamishia muhimbil (Moi) - wakasema mishipa kichwan imetanuka akafanyiwa upasuaj ukamalizika ila
Dah ….rest in peace my young sister
 
Ali mpemba huyoo alifanya yake.... natania
 
Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 27.

Nilifanikiwa kufika Sumbawanga na ilikuwa ni Safari iliyochukua takribani siku siku mbili kwasababu nakumbuka tulipofika Mbeya tulilala pale halafu kesho yake tukaianza tena safari, nilipofika Sumbawanga sikutaka kupoteza muda nilitafuta gari zilizokuwa zinaelekea Namanyere nikawa nimekata tiketi,muda ulipowadia tuliondoka.

Nilifanikiwa kufika kwa yule mtaalamu niliyekuwa nimeelekezwa kwake,alinipokea na nikawa nimeambiwa nisubiri kwanza amalize kuwatibu watu kadhaa niliowakuta pale;Zamu yangu ilipofika aliiniita nikawa nimeingia ndani ambako alikuwa akifanyia shughuli zake za uaguzi.Sasa alinipatia kigoda nikawa nimekalia na akaniambia nitulie nisizungumue jambo lolote,alianza kuhesabu tudude fulani kama tumawe kisha akawa ananiambia.

Mganga "Hadi sasa uko hai inabidi ushukuru Mizimu kukulinda"

Aliendelea "Naangalia namna ulivyotupiwa jini linaloendelea kukutesa na inapaswa ufe,kuna sehemu ulienda ukatengenezwa ndiyo imesaidia"

Aliendelea "Mtu uliyemuamini ndiye kafanya yote haya"

Mganga "Huyu mtu ni nani kwako?"

Mimi "Ni rafiki yangu tu"

Mganga " Kwanini unaishi na rafiki ambaye anakufanyia mambo mabaya namna hii?"

Aliendelea " Huyu mtu ni hatari sana kwako"

Aliendelea "Huyu mtu anafuga jini ambalo ndilo limekuhangaisha na kwakuwa ulikuwa kwenye himaya yake alikuwa anakufanya anavyotaka!"

Aliendelea "Ndiyo maana nasema Uishukuru Mizimu yako kwasababu alikuwa amekutegeshea Jini hilo likuangamize kabisa"

Baada ya kuniambia maneno hayo ndipo sasa akaniambia nizingumze ninachokitaka.

Mimi "Nimekuja unisaidie maana hali yangu si nzuri "

Mganga "Nitakusaidia ondoa shaka ila inabidi kuna vitu ununue niweze kukutengeneza vizuri"

Basi akawa ameniambia nikanunue vitu kadhaa ambavyo vitahusika katika matibabu yangu,mimi nilitoa fedha na vitu hivyo vikaenda kununuliwa na mtu ambaye alimtuma yeye.Baada ya kununuliwa vitu hivyo nilianza matibabu na matibabu yenyewe nakumbuka kuna mengine yalifanyika makaburini akiwa ameniambia ni kuzika mikosi yote na uchawi wote ule wa Ki-Unguja(Chumbe).

Nilikaa kwa yule mtaalamu takribani wiki 2 na baada ya kuwa amekamilisha zoezi la matibabu,kuna dawa kadhaa alinipatia ambazo aliniambia nitazitumia nikapafika Dar es salaam.Niliondoka nikawa nimerudi Dar es salaam na sikutakiwa kabisa kumsogelea Ally Mpemba hata kidogo,nakumbuka maisha yalianza kuwa magumu sana tena kwa upande wangu,kwakuwa nilishazoea kupambana sikutaka kabisa kukaa,fedha ambayo nilikuwa nayo kwa kipindi hicho ndiyo ilinisaidia kwa kipindi chote ambacho sikuwa na kazi,pia ndiyo fedha niliyotumia kumlipia Ada na matumizi mpenzi wangu Rehema wakati wote akiwa chuo cha ualimu.

Kuna kipindi hali ilipokuwa mbaya kiuchumi nilikuwa naenda pale Gongo la mboto kwa washikaji kujipendekeza kwenye magari na hatimaye kuna gari ambalo nililipata nikawa konda mimi na mshikaji wangu mmoja,lile gari lilikuwa likifanya ruti za Gongo la mboto kwenda Mbagala,niliamua kuto mtazama mtu usoni ili niweze kupambana,sasa nakumbuka Steve alikuwa akinishangaa mimi kuwa konda wa daladala ilihali niliacha kazi ambayo angalau ilikuwa kidogo na heshima ya usajili wa line,jamaa yeye aliona ni heri kuwa msajili line kuliko kuwa konda kazi ambayo ilikuwa ikidharaulika na kila mtu!,mimi sikuona taabu yeyote kwasababu nilishaifanya na ambacho nikagundua ni kwamba wakati huo makonda walikuwa wakipiga sana hela,yaani kulaza kwa siku elfu 20 lilikuwa jambo la kawaida kabisa,hiyo elfu 20 ni hela ambayo unabaki nayo baada ya mambo mengine kama msosi n.k

Mimi sikutaka kumuangalia mtu ananipangia nifanye nini,niliangalia kitu ambacho kinanipatia hela nzuri na ambacho nakifanya kwa moyo mmoja,aibu haikuwaga na haipo hadi leo kwenye maisha yangu ya utafutaji!.Kwenye lile gari nakumbula makonda tulikuwa wawili kwasababu lilikuwa gari lililokuwa na milango miwili,hivyo tukawa tunafanya kazi kwa kushirikiana!.

Namshukuru Mungu hata Rehema wangu ni mwanamke ambaye alikuwa hajali wala hachukii kile nilichokuwa nakifanya,tena nakumbuka ni mwanamke ambaye alinitia sana moyo katika kupambana.Alipomaliza chuo akawa ameajiliwa mkoani Morogoro wilaya ya Ifakara ambako ndiko anafanyia kazi hadi leo,baada ya kuwa ameajiliwa na kupangiwa kituo cha kazi akawa ameondoka.
Mimi niliendelea kupambana sana kwenye kazi ya ukonda na nikawa najinyima kiasi kwamba nikapunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.Baada ya kutengeneza kama milioni 2 kwa miezi kadhaa ya kujinyima,nikawa nimenunua tena uwanja maeneo ya kibamba,nililipa hela nusu nikawa napambana kutafuta pesa nyingine ili angalau nilipe yote kile kiwanja nikimiliki,nilipambana sana na hatimaye nikawa nimemaliza kulipia kile kiwanja,sasa kumbe kiwanja chenyewe kilikuwa na mgogoro wa kifamilia.Kiukweli nilihangaika sana na kile kiwanja,ilifika sehemu mtu aliyeniuzia tulifikishana hadi mahakamani,jamaa aliahidi kuwa atakuwa ananipatia hela kidogo kidogo hadi hela niliyompatia itakapokwisha,sasa ulipaji wake ulikuwa wa kusua sua na ikabidi niachane nacho,alinilipaga pesa kama nusu ya kile nilichompatia ikabidi niachane nae.
Rehema aliniambia nitulie niachane nacho na kama ni uwanja tungenunua mwingine,huu mji kiukweli umenitesa sana ndugu zangu.

Namshukuru Mungu baada ya kupata tena fedha kiasi ambazo nilizikusanya kwenye kazi yangu ya ukonda kwa kudunduliza,Rehema akawa ameniongezea fedha nyingine nikawa nimenunua pikipiki yangu na nikaanza rasmi kazi ya bodaboda ambayo ndiyo inaniweka mjini hadi leo.

Rehema alinizalia mtoto wa kike mzuri kama yeye na mwaka huu ifikapo mwezi wa kumi anatimiza umri wa miaka 5.Rehema hadi sasa ni mwanamke wangu ingawa mi naishi Dar es salaam na yeye akiwa kituo cha kazi hapo Ifakara,huwa naenda na yeye pia huwa anakuja Dar es salaam.

Ally Mpemba hadi sasa ninavyoandika hapa yupo na naona jamaa amekuwa mtu mkubwa sana,lile duka la pale gerezani walilifunga na ile fremu sikuhizi naona ina mtu mwenye biashara nyingine,duka lile la Aggrey bado lipo na huwa jamaa anakuwepo pale mara moja moja,ule mgahawa hadi sasa upo na unayo sifa ileile ya kuua wafanyakazi wake.

Jamaa kwasasa sijajua atakuwa anabiashara gani nyingine lakini hizo nilizoziacha bado zinafanya kazi.

Mwaka jana nikiwa kwenye mitikasi yangu Kkoo nilipita pale Aggrey nikawa nimemuona ila yeye hakuniona.Jamaa bado anaendeleza libeneke na kupiga pesa.

Mimi niliamua nichague haya maisha yangu yasiyokuwa na msongo hata kidogo kwasababu naridhika na hichi kidogo nikipatacho.

Kuna uwanja mwaka jana nimenunua kwa kushirikiana na Rehema wangu upo maeneo ya Maili moja,na Mungu akisaidia mwaka huu tunaweza kuanza ujenzi mdogo mdogo.

Kituo changu cha kazi huwa ni Bunju ingawaje pia huwa niko bize wakati fulani,mimi napaki Bunju ila sikai Bunju ndugu zangu.

Maisha si lelemama kama mnavyodhani,kama una nafasi ya kufanya chochote ambacho ni halali wewe fanya ili ukimbilie ndoto zako,usiogope kufanya kwa kuhofia watu watasema nini,wewe kaza moyo fanya,hao wanakucheka leo yawezekana kesho wakaanza kusema weww ni freemason,hivyo wape kisogo na fanya chochote ilimradi kinakuingizia pesa.

Usimuangalie mtu wewe ziangalie fedha,huyo mtu anakucheka kwasababu huna fedha,ukizipata hata kuwa na muda wa kukucheka tena.

MWISHO.
Kazi nzuri sana na hongera sana Kwa mapambano, visa vyako vinatoa mafundisho mengi yanayotunga na kutupa moyo vijana wenzako. Asante sana UMUGHAKA . Ukipata muda shusha nyuzi nyingine sie wasomaji wako kindakindai.
 
Similar Discussions

122 Reactions
Reply
Back
Top Bottom