Utajiri wa mbuga za wanyama Tanzania ni kielelezo cha ardhi duni.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,872
2,000
Tanzania ni mojawapo wa nchi chache duniani zenye utajiri mkubwa wa wanyama wa mwituni na ndiyo maana maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Hifadhi za Taifa (National Parks); Mbuga za Wanyama (Game Reserve) na Hifadhi za Misitu nchini ni wastani wa theluthi (1/3) ya ukubwa Nchi nzima. Ikiwa na km za mraba 945,000 Tanzania ni ya 12 kwa ukubwa wa eneo na ya 5 kwa watu barani Afrika.
Ukitoa Mbuga ya Selous (1920), Hifadhi na Mbuga zote nchini zilianzishwa baada ya mwaka 1951 kwa kuanzia na Serengeti, Mkomazi na Rungwa (1951). Zoezi la kuanzisha ama kupandisha maeneo yaliyotengwa limeendelea hadi miaka ya 1990 na mpaka miaka ya 2000s (Hifadhi ya Saanane). Uanzishwaji wa mbuga hizo ukiacha maeneo machache haukuhusu kuhamisha watu Bali maeneo hayo hayakuwa yamekaliwa na watu.
Kumbuka kipindi cha kuelekea uhuru wakati Hifadhi zinaanza kuanzishwa, Tanganyika ili kuwa na wakazi wapatao milioni 8 lakini ukirudi nyuma kipindi cha wajerumani (1910s) idadi ya watanganyika ilkuwa ni milioni 5 pekee. Linganisha Idadi hiyo ndogo na nchi za Rwanda yenye km za mraba 26,000 (watu milioni 2) na Burundi km za mraba 24,000 (watu millions 1.5) kwa kipindi hicho.
Licha ya kwamba watu wameongezeka sana nchini na kuwa nchi ya 5 Afrika kutoka ya 9 miaka ya 1970s, hiyo inaonyesha kuwa eneo kubwa la nchi limekuwa na mvua chache ama magonjwa ya yellow fever na mbung'o kiasi cha kutokaliwa na watu wengi. Mfano mzuri ni Pori kubwa la Selous na la Mikoa ya Tabora na Katavi.
Hivyo tukijivunia Mbuga zeta za wanyama tukumbuke kuwa ni maeneo yaliyoachwa kwa kutofaa kwa makazi na shughuli za kilimo.
 

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,872
2,000
Mtu anapotaka kuanza kufuga ng'ombe wa maziwa, anatafuta ng'ombe wa kisasa (kizungu). Hata hivyo hata kwenye hao wa kizungu atatafuta mwenye asili ya Holland ama Frisian ambao hutoa maziwa mengi kulinganisha na ng'ombe wengine.
Vilevile mkulima akitaka kulima mpunga nchini, anatafuta zaidi mbegu zenye asili ya Kyela Mbeya. Hii inamaanisha kuwa viumbe ambavyo vimekuwa na Nasaba nzuri yaani kwa nenda rudi vimekuwa vikipata vyakula vyenye virutubisho vya kutosha vimekuwa bora kulinganisha na viumbe ambavyo kwa miaka nenda rudi vimekuwa havipati vyakula bora kutokana na mazingira magumu yakiwemo ukase na magonjwa kama malaria na homa ya manjano.
Kutokana na Hali hiyo, maeneo mengi nchini yalibaki bila kukaliwa na watu kwa kuwa hayakuwa na uwezo wa kuzalisha vyakula bora. Aidha, kutokana na kanuni hiyo, ni wazi maeneo ambayo yalikuwa na ukame wa muda merge nchini, Mazao yake hayakuwa na virutubisho bora kulinganisha na maeneo yaliyokuwa yakipata mvua nyingi. Mfano nyama ya ng'ombe ya Rungwe Mbeya ni tamu sana lakini nyama kutoka wilaya yoyote mkoani Iringa hakuna lad ha nzuri. Mchele wa Kyela una soko kubwa kuliko wa aina yoyote Tanzania kama siyo kwa Bara Ziwa la Afrika kwa kuwa una ladha tamu sana tofauti na Michele kutoka seems nyingine mfano Mbarali.
He tunaweza kutafasiri nini juu ya sisi binadamu kama viumbe hai vyote vinaitikia hiyo kanuni. Je sisi ni dhaifu Afrika Mashariki kuliko wenzetu kwenye ubora wa nasaba kutokana na makabila mengi kupatikana kwenye maeneo yasiyo na rutuba hata nchini. Je ukubwa wa mapori Tanzania haumaanishi hata sisi mababu zetu (nasaba zetu) wamekulia katika mazingira magumu kwa hiyo tuna nasaba duni?
Tusaidiane kujibu hizo changamoto hasa ya kwa nini Tz ndio tunaogopa kujiunga na vitu ambavyo majirani zenu Arika Mashariki wanataka, kwa nini wao hawaogopi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom