Utajiri wa mafisadi kikwazo kushitakiwa

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Utajiri wa mafisadi kikwazo kushitakiwa

* Waziri Mkuu asema uwezo wao kifedha unaiogopesha serikali

*Wahusika wa Richmond kuchukuliwa hatua za kinidhamu tu

*Asema kuna upungufu mkubwa ofisi ya Mwanyika

*Serikali yazikataa mvua za Lowassa

Na Michael Uledi, Dodoma


SERIKALI imesema utajiri wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni moja ya kikwazo cha kuwafikisha mahakamani kwa pupa.Kauli hiyo ya serikali inayoonyesha kuwa, watuhumiwa wa EPA ni vigogo na watu wenye mtandao mpana ndani na nje ya serikali, imetolewa mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari.


Awali, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, ambaye ni mjumbe wa Timu ya Rais (Task Force) ya kuchunguza kukamata na kuchukua hatua za kisheria, aliwafananisha mafisadi wa EPA sawa na magaidi ambao wakifuatwa kwa pupa wanaweza kuilipua nchi.


Hata hivyo, Pinda ambaye amezungumzia suala hilo kwa mara ya kwanza tangu awe Waziri Mkuu, alisema bado serikali inaweza kutumia ushahidi wa fedha zinazorudishwa na baadhi ya

makampuni yaliyochota fedha kutoka EPA, kama ushahidi wa kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafungulia kesi za jinai mahakamani.


Pinda ambaye aliamua kuitisha mkutano huo na waandishi na kuwapa fursa waandishi waulize maswali bila yeye kuzungumza, alisema watu waliohusika na uchukuaji zaidi ya Sh133 bilioni lazima watakuwa ni vigogo, hivyo iwapo watapelekwa mahakamani

bila umakini wanaweza kuitia hasara zaidi serikali kutokana na uwezekano mkubwa wa kuweza kushinda kesi na fedha zisirudi.


Alisema kutokana na hali hiyo njia inayotumika na Kamati inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ndiyo mwafaka katika kulishughulikia suala hilo ambalo kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa fedha zinarejeshwa na kisha ikilazimu zitumike kama ushahidi mahakamani.Pinda aliyekuwa akitimiza siku 60 tangu ateuliwe na kuthibitishwa kushika wadhifha huo, alisema kamati inayoongozwa na Mwanyika itaendelea kufanya uchunguzi juu ya ukiukwaji wa taratibu katika uchukuaji wa fedha za EPA na kwamba hakuna sababu

ya kamati hiyo kuingiliwa na watu wengine kwa sasa.


Katika kuhakikisha kunakuwa na mafanikio katika suala hilo ambalo limeifanya serikali kuanza kupoteza imani yake kwa wananchi, alisema ni kuhakikisha kuwa kila jambo linafanyika kwa uangalifu ambapo kamati husika inatakiwa kuwa na uwezo wa kuchunguza kwa umakini na kisha kupatikana ufumbuzi wa suala hilo.“Watu waliochukua fedha zaidi ya Sh46 bilioni ukiwapeleka mahakamani wanaweza kushinda kesi na hivyo hata fedha zisirudi, kwa maoni yangu naona njia inayotumika hivi sasa ni njia bora na inayowezesha kufanikisha mkakati huo wa kurudisha fedha hizo. Kama kuna umuhimu wa kwenda mahakamani fedha hizo zinaweza

kutumika kama ushahidi, ”alisema.


Hata hivyo, Pinda aliweka bayana awali kwamba hakuwa na uhakika kama majibu yake yangeweza kuwa mazuri kwa umma kutokana na unyeti wa suala lenyewe.


Alisema kamati ya Rais ina uwezo wa kueleza hatua kwa hatua juu ya hali ilivyo kuhusiana na suala hilo na amekemea kusijetokea viongozi wasiokuwa katika kamati hiyo, na kuanza kuingilia uchunguzi, jambo linaloweza kuharibu mustakabali wa kazi hiyo.


Juu ya kutaja wahusika wa wizi wa fedha hizo za walipakodi, Pinda alisema ni suala gumu kuwataja waliorudisha kwa kile alichodai kunaweza kuharibu uchunguzi


Alisema imani yake ni kuwa Watanzania wote akiwamo yeye, wana shauku ya kuwajua watu wote waliohusika katika wizi huo uliolitia hasara kubwa taifa, jambo ambalo likiunganishwa na misukosuko ya Kampuni ya kufua umeme ya Richmond lilishaanza kupunguza imani ya wananchi kwa serikali.


Waziri Mkuu, alisema uchunguzi utakapokamilika serikali itachukua hatua mbalimbali kwa watu waliohusika ikiwa ni pamoja na watumishi wa umma waliojihusisha na ufisadi huo katika maeneo yao ya kazi.


Kuhusu Richmond, alisema Tume ya Serikali ya kupitia mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu uchunguzi wa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond imemaliza kazi, lakini watumishi waliozembea hawatashitakiwa.


Kauli hiyo ya serikali imemaliza kile ambacho watu walikifikiri kwamba kungekuwa na uwezekano wa kuwafikisha mahakamani watumishi hao waliozembea hadi kutiwa saini mkataba huo.


Uamuzi huo wa serikali kuachana na mpango wa kushitaki watumishi wake, unatokana na ugumu wa ushahidi mahakamani kuthibitisha tuhuma hizo za uzembe wakati mchakato

ulifanyika katika vikao mbalimbali vya Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT).


Pinda ambaye anakabiliwa na mtihani mzito na wa kwanza katika mkutano huu wa 11 wa Bunge wa kuitetea na kutoa ufafanuzi wa mambo ya serikali bungeni, alisema Kamati yake ndogo (Task Force) ya wataalamu iliyopewa kazi ya kufanyia kazi

mapendekezo ya Kamati ya Mwakyembe (Dk Harrison-Mbunge wa Kyela), imekamilisha kazi.


Kwa mujibu wa Pinda, iwapo Spika atampa fursa katika mkutano huo atatoa taarifa kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na zile zitakazochukuliwa siku za usoni dhidi ya wahusika.


Waziri Mkuu alisema iwapo hakutakuwa na nafasi katika mkutano ni imani yake suala hilo linaweza kushughulikiwa katika mkutano wa Bunge ujao wa Juni.


Alionya kuwa, serikali haitakuwa na subira na wale wote watakaothibitika kuwa walisababisha hasara kwa taifa kwa namna moja au nyingine, na kuongeza kwamba serikali itawawajibisha kwa mujibu wa taratibu za kiutawala ili kuepuka uwezekano wa serikali kushitakiwa na kushindwa kesi.


Hata hivyo, alisema kuwa baada ya kamati yake kupitia mapendekezo ya hiyo Kamati Teule, imebainika kuwepo mapungufu ambayo ni pamoja na kuwapo uwezo mdogo wa kiutaalamu katika nyanja ya majadiliano ya mikataba kwa watumishi wa umma , hususan kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Alisema uwezo huo mdogo wa wataalamu umewafanya kushindwa kuzingatia maslahi ya Taifa na kuongeza kwamba, kasoro nyingine ni pamoja na matatizo ya usimamizi wa manunuzi

ambapo Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), bado haijawa huru kutokana na kufanya kazi zake chini ya Wizara ya Fedha tofauti na kama ilivyo Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Sanjari na hilo kasoro nyingine ambayo imebainika ni pamoja na kukosekana kwa taratibu bayana za uwajibishaji wa watumishi wa umma na viongozi wa kisiasa, na kuongeza sakata la Richmond limedhihirisha kuwa suala la maadili kwa watumishi na viongozi halijapewa kipaumbele katika masuala ya kitaifa.


Kuhusu mapendekezo ya wabunge wakati wa mkutano wa Bunge uliopita kutaka wahusika wa sakata la Richmond wafilisiwe, Waziri Mkuu, alisema hata kama ingebidi kufilisi mtu si jambo rahisi ni muhimu kwenda mahakamani.


Wakati huo; Waziri Mkuu amesema mradi wa mvua ya Thailand maarufu kama mvua ya Lowassa, umeshindikana kutokana na gharama kubwa.


Alisema utatifi kuhusiana na mvua hizo, ungeligharimu serikali zaidi ya Sh15bilioni, kiasi ambacho alisema ni kikubwa.


Taarifa za mvua hizo, zilikuja baada ya aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa kutembelea nchini humo na kukutana na wataalamu waliomuahidi kuja kutengeneza mvua hizo nchini, ili kukabiliana na ukame katika mabwawa yanayozalisha umeme, likiwamo la Mtera na Kidatu, ambayo yalikauka maji na kusababisha kuwapo kwa mgao wa umeme.

Source: Mwananchi newspaper
 

Now I know,

I amass wealth (irrespective of the means)so much of it and come to live in Tanzania, where the law has eyes and rewards the "moneyful" ones with an eternal impunity.
 
Kweli hii ni kasi mpya, hari mpya, nguvu mpya na usanii.

Ila kuna kitu kimoja huwa najiuliza wakati Benjamini anaingia madarakani alipo ambiwa kuwa kuna rushwa alikuwa hataki kuzungumza sana hila alikuwa anasema katika swala la rushwa hatakuwa na suluhu, kuwa halina mjanada atalimaliza.

Jk alipo ingia alisema anataka kujenga tanzania yenye neema ili watanzania wote wafaidi raslimali zao. Alitoa mifano mingi sana akazungumzia jinsi watanzania wanavyokula mlo mmoja kwa siku na kusema anataka kuwaondoa katika dimbwi la umasikini.

Akaja na kasi mpya na hari mpya iliyokuwa imetoweka baada ya BENJA kusaini kuwageuka watanzania na kusaini mikataba ya rushwa akibadisha rushwa jina(akiweka tasifida)TAKRIMA.

Sasa hivi baada ya JK kuwa madarakani miaka miwili/mitatu tayari ameanza mbinu za kusaini mikataba na MAFISADI(kusalimu amri ) na kusahau wananchi kuwa hawawezi sasa hata kupata mlo mmoja. Maana kila kitu sasa ni juu mojawapo ya sababu ni UFISADI ambao mwingine umefanyika akiwa tayari madarakani.

Yeye sasa huyo anatalii, watanzania hoe hae.

Sasa suala ninalojiuliza hivi pale ikulu kulikoni panabadilisha watu kwa muda mfupi? Tunatakiwa kufanya tafiti kujua nini haswa kinawasibu viongozi wetu mara tu wapatapo madaraka. Inawezekana kuna vitisho pale ikulu.
 
Kweli hii ni kasi mpya, hari mpya, nguvu mpya na usanii.

Ila kuna kitu kimoja huwa najiuliza wakati Benjamini anaingia madarakani alipo ambiwa kuwa kuna rushwa alikuwa hataki kuzungumza sana hila alikuwa anasema katika swala la rushwa hatakuwa na suluhu, kuwa halina mjanada atalimaliza.

Jk alipo ingia alisema anataka kujenga tanzania yenye neema ili watanzania wote wafaidi raslimali zao. Alitoa mifano mingi sana akazungumzia jinsi watanzania wanavyokula mlo mmoja kwa siku na kusema anataka kuwaondoa katika dimbwi la umasikini.

Akaja na kasi mpya na hari mpya iliyokuwa imetoweka baada ya BENJA kusaini kuwageuka watanzania na kusaini mikataba ya rushwa akibadisha rushwa jina(akiweka tasifida)TAKRIMA.

Sasa hivi baada ya JK kuwa madarakani miaka miwili/mitatu tayari ameanza mbinu za kusaini mikataba na MAFISADI(kusalimu amri ) na kusahau wananchi kuwa hawawezi sasa hata kupata mlo mmoja. Maana kila kitu sasa ni juu mojawapo ya sababu ni UFISADI ambao mwingine umefanyika akiwa tayari madarakani.

Yeye sasa huyo anatalii, watanzania hoe hae.

Sasa suala ninalojiuliza hivi pale ikulu kulikoni panabadilisha watu kwa muda mfupi? Tunatakiwa kufanya tafiti kujua nini haswa kinawasibu viongozi wetu mara tu wapatapo madaraka. Inawezekana kuna vitisho pale ikulu.

Mafisadi wanakuwa matajiri kupitia mapesa wanayakupua toka kwa walipa kodi wa Tanzania. Halafu pesa hizi hizi walizokupua ndizo zinawapa kinga ili wasishtakiwe! :confused:
Hili tamko la pinda linaleta ujumbe mbaya sana kwa mafisadi kwamba they are untouchables!

Ama kweli tunaongozwa na wendawazimu na mafisadi ambao hawastahili nafasi yoyote ta uongozi katika nchi yetu.
 
Mimi nafikiri pinda amekosea kusema kuwa majambazi hawashikiki. Hapa ina maana ametoa ruhusa kwa kila mtu akiweza kukusanya pesa za kutosha automatically anakuwa juu ya sheria bila kuangalia kazipataje
 
kakindo master nakukubali kabsaaa....usemi wake huoo una mushkeri...
 
Hivyo ni visingizio visivyo na msingi wowote.Sasa hii inatuweka njia panda.Kwamba sasa rasilimali zetu ziendelee kuibiwa bila sisi kufanya lolote,jamani hii mpya.Hivi utajiri wa mtu unashindana na nguvu za kijeshi.Kwani Nyerere alifanyaje mpaka akawadhibiti.Mmm,haya maajabu.Nimesema wananchi hatuna wakutusaidia,shetani ameshachukua nchi,viongozi wa dini,na ninyi shetani amewadhibiti nini,mbona mko kimya amkeni mtetee wananchi hawa maskini wasio na mtetezi kabisa.
 
Tanzania hatuna sheria inayosema mtu akiwa tajiri mkubwa basi hata akitenda maovu hatashtakiwa kutokana na utajiri wake. Haya ni mawazo mufilisi yaliyojengwa na mafisadi waliokuwa madarakani akina Kikwete, Pinda, Mwanyika na Mkuu wa polisi. Mbona wahujumu uchumi walifikishwa mahakamani bila kujali walikuwa na utajiri mkubwa kiasi gani? Hiyo sheria imetungwa lini na Bunge la Tanzania? Wapumbavu tu hawa kazi imewashinda lakini bado wanaendelea kung'ang'ania madarakani.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom