Utajiri wa kizazi Cha kwanza (First Generation) Huwa mgumu sana

Changamoto nyingine ni Sibling rivary. Ndugu yako wa damu anakuletea upinzani akisikia unataka kubomoa nyumba ya zamani na kushusha apartments kwa mpunga uliopata kwenye harakati zako.

Anaona hapa hatakuwa na sauti anapinga kabisa ile ya sitaki upate.

Hii tabia imefelisha familia nyingi sana za watoto zaidi ya wawili kutaka kugawana mali ili kila mtu afe kivyake. Ila baada ya miaka kadhaa unawakuta wamefulia mali zote wamejifilisi.

Ubinafsi ni mbaya sana .
Kwa nini uruhusu ndugu yako akurudishe nyuma? Huo ni upunguani...
 
that is why wanyonge watabaki kuwa wanyonge milele,ukiinuka kidogo unakua nguzo ya ukoo mzima hupati ata nafasi ya kufanya maendeleo zaidi
Inabidi uwe tough kwa ndugu zako. Kwani wao ni nini kimewazuia wasifanikiwe kama wewe? Si wote mmezaliwa katika hali hio hio? Manake wao si wapambanaji kama ww. Mimi nawaambia wapambane tu na hali zao.
 
Hapo mnakosea sana. Mimi binafsi sikusaidiwa na ndugu yeyote tena wakati napambana mishe za kwenda ughaibuni ambako ndio kulinitoa, walikuwa wananiita mwenye ndoto za ramli, mvuta bangi, na aliyechanganyikiwa.
Ila baada ya mafanikio wote wanakuona Hero
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom