Utajiri wa kizazi Cha kwanza (First Generation) Huwa mgumu sana

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,273
7,362
Nawasalimu Kwa Jina la Jamhuri Kazi iendelee

Utajiri wa kizazi Cha kwanza Huwa mgumu mno kwakua ,muhusika anakuwa Hana rasilimali za kumuwezesha kufanikisha mambo yake hvyo bhac ...mtaji pekee alionao ni Akili yake

Tofauti na utajiri wa kurithi ambayo muhusika anakua na jukumu la kuendeleza vile alivovikuta au vile alivyo achiwa

Safari ya kuutafuta Utajiri ikiwa ww ndo rasilimali pekee , Maumivu yake n makali sana kwakua kila kitu unachokifanya lazima ukihangaikie Kwa nguvu nyingi sana ,nidhamu ya Hali ya juu ,kujituma sana ili kuweza kukamilisha ndoto zako

Utajiri wa kizazi Cha kwanza ..upo Kwa Wachache ,wengi wamekuta mali ..hvyo jukumu pekee walilonao n kuendeleza vile walivyovikuta

Jamii kama ya wahindi Wana Tamaduni za kurithishana mali mfano mtu kama Moe dewg , Richard wa Toyota , na wengine Hawa wamezaliwa kwenye utajiri so kuviendeleza walivovikuta n kazi ngumu lakini sio kama ya kuanzisha kitu kipya

Asilimia kubwa ya matajiri wa kizazi Cha kwanza (first generation) ..wamefanikiwa kutokana na Talents walizo nazo ...mfano wanamuziki , wacheza mpira, wavumbuzi wa vitu mbali mbali n.k

Big S/O Kwa matajiri wote wa kizazi Cha kwanza Juhudi zenu ndo zimezaa matunda ya mafanikio na maendeleo tuliyo nayo
 
Licha ya kurithishana mali, Wahindi huwekeza kwenye ndoa. Mfano ninataka kufungua tawi la Supermarket yangu Mombasa. Nitamtafuta mtu wa kushirikiana nae pale Mombasa, yeye ndiye atakua msimamizi wa kila siku na wote tutaweka pesa. Baadae watoto wetu wataoana na wataendeleza ile biashara.
 
bado sijaelewa umemlenga nani
Tulia usome kwa umakini utaelewa tu.

Anachosema mwandishi ni kwamba, ni kazi sana kutafuta mali ukatengeneza utajiri wa kudumu. Inahitaji akili ya ziada, vipaji na ugunduzi ili kupata utajiri.

Akaeleza matajiri wengi wamerithi, ni kazi kuuendeleza na kuukuza utajiri wa kurithi lakini ni kazi zaidi kuutafuta ukiwa hauna kitu.
 
Tulia usome kwa umakini utaelewa tu.

Anachosema mwandishi ni kwamba, ni kazi sana kutafuta mali ukatengeneza utajiri wa kudumu. Inahitaji akili ya ziada, vipaji na ugunduzi ili kupata utajiri.

Akaeleza matajiri wengi wamerithi, ni kazi kuuendeleza na kuukuza utajiri wa kurithi lakini ni kazi zaidi kuutafuta ukiwa hauna kitu.
Shukrani sana mkuu...kwa kuelewa point yangu
 
Daah acha tu.

Kuendeleza mali uliyoikuta unatumia nguvu ndogo sana.

Ukiwa na akili na nidhamu nguvu inazidi kupungua.

Balaa kuanza kutafuta uwe tajiri.

Changamoto zake unaweza kukata tamaa ukaishia njiani.
Yeah .na mazingira yetu ya kiafrica ..utapitia changamoto nyingi sana ..coz vikwazo ni vingi sana
 
Tumetoka familia maskin ambazo wazazi waliishi bila hata kumiliki baiskel tukawa tukiona magari ya watu mtaani tunaimba "gariii ya babaa" ili tujifariji
Lakin sisi inatakiwa tupambane zaid ili watoto wetu wasije kuimba kama tulivyoimba sisi waanziee kuyaona magari na nyumba nzuri kwao hata kama hatutakua matajiri wakubwa lakin sisi iwe ngazi ya wao kuufikia utajiri mkubwa
 
Licha ya kurithishana mali, Wahindi huwekeza kwenye ndoa. Mfano ninataka kufungua tawi la Supermarket yangu Mombasa. Nitamtafuta mtu wa kushirikiana nae pale Mombasa, yeye ndiye atakua msimamizi wa kila siku na wote tutaweka pesa. Baadae watoto wetu wataoana na wataendeleza ile biashara.
For sure wenzetu Hadi Kwa Mahusiano Wana nidhamu pia ...hivyo ni rahisi kukuza utajiri coz wanaishi Kwa kuheshimiana na pia kama ulivoeleza ..hapo wakitaka kufanua Wigo wa biashara ..wanawekeza pia kwenye ndoa ...
 
Waafrica huwa hatuwekezi kwenye mafunzo ya take over kwa watoto wetu ya kile tulichokifanya maishani, unafikia wakati huna nguvu watoto wako hata mkeo hajui undani wa chote kile ulichokifanya maishani - ukifa mali zinapotea, watoto wako wanamalizia na wajukuu wanakuta hamna kitu zaidi ya story kwamba Babu yenu alikuwa doni sana hapa mtaani....inasaidia nini.
 
Back
Top Bottom