Utajiri wa kibegi unavyopukutisha vijana mikoa ya Kusini

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,094
2,835
Hii ni aina mpya ya uchawi na njia ya mkato ya kupata pesa bila kuzitolea jasho! Ni utajiri flani hivi ambao unapewa kibegi na mganga na popote unapoenda lazima ukibebe mgongoni. Ndani ya kibegi kuna kinyoka kidogo urefu wa nusu futi, kinakaa ndani ya begi maisha yake yote!

Kila unapokatiza na kibegi mitaani kinakusanya fedha, kikijaa unaenda kupeleka benki unaendelea na mizunguko yako! Kwa siku mtu unasanya hata m50. Ukienda baadhi ya maeneo kuna watu kila siku anakibegi na hakitoki begani, wanaviduka vya kuzugia tu ila ni watu hatari.

Yule nyoka anavyozidi kukua na utajiri unaongezeka, ila siku akianza kuugua na wewe unaugua na siku akifa na wewe unakufa! Nilipelekwa na marafiki zangu fulani ambao ni matajiri sana, ila nilivyoambiwa akifa na mimi nakufa nikastuka.

Kwa ushuhuda wangu vijana wanakufa ovyo kwa tamaa ya pesa. Naongea hivyo leo tumetoka kumzika mmojawapo aliyewahi kunishawishi sana, kweli alikuwa na pesa siyo mchezo. Benki anaenda mara tatu kwa siku, tutafuteni pesa halali, kama ipo ipo tu.
Screenshot_20230213-174730_1.jpg
 
Daahh ..subhana llaah maisha haya naogopa kuhukumu lakini shirki ni mbaya mnoo na Ndo maana inakatwazwa Sana ktk vitabu vya dini(Kwa wanaoamini)

Ila Sasa umaskini nao daahhhh ugaigai Sana Jamani kudharaulika plus kuonekana mpuuzi umefeli ndo maana watu wanajitosa huko huko japo wanakufa..mtihani Sana asikuambie mtu ndugu yangu,ingawa huo utajiri wa muda na furaha yake haidumu ni fupi tu ilabwenyewe wanainjoi baaasi Kwa Mimi siwezi Imani yangu hainiruhusu kufanya shirk ya aina yoyote ile na naogopa Sana hizo Mali za masharti Zina mitihani Sana i

Sasa huyo nyoka hang'ati na akijua Ina maana unawezaje kumbebelea duhhh!!!yaani akifa tu na we umedanja!si jinni Hilo Jamani
 
Hii ni aina mpya ya uchawi na njia ya mkato ya kupata pesa bila kuzitolea jasho! Ni utajiri flani hivi ambao unapewa kibegi na mganga na popote unapoenda lazima ukibebe mgongoni. Ndani ya kibegi kuna kinyoka kidogo urefu wa nusu futi, kinakaa ndani ya begi maisha yake yote! Kila unapokatiza na kibegi mitaani kinakusanya fedha ,kikijaa unaenda kupeleka benki unaendelea na mizunguko yako ! Kwa siku mtu unasanya hata m,50! ukienda baadhi ya maeneo kuna watu kila siku anakibegi na hakitoki begani! wana viduka vya kuzugia tu ila ni watu hatari. yule nyoka anavyozidi kukua na utajiri unaongezeka! ila siku akianza kuugua na wewe unaugua na siku akifa na wewe unakufa.nilipelekwa na marafiki zangu flani ambao ni matajiri sana,ila nilivyoambiwa akifa na mm nakufa nikastuka. kwa ushuhuda wangu vijana wanakufa ovyo kwa tamaa ya pesa! naongea hivyo leo tumetoka kumzika mmojawapo aliewahi kunishawishi sana! kweli alikuwa na pesa sio mchezo! benki anaenda mara tatu kwa siku tutafuteni pesa halali , kama ipo ipo tu
Unaweza kunipeleka mkuu?
 
Ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom