Utajiri wa Gachuma, Airo watumika kushawishi wapiga kura Kirumba; Mrisho Ngassa atumika kwa kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Gachuma, Airo watumika kushawishi wapiga kura Kirumba; Mrisho Ngassa atumika kwa kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Deus Bugaywa
  [​IMG]


  Mrisho Ngassa atumika kushawishi kura
  Waahidi kutumia fedha binafsi kujenga barabara, kutatua kero ya madawati
  Henry Joseph, Jerry Tegete na Mrisho Ngassa watumika kushawishi kura


  VYAMA vya CCM na CHADEMA vimeendelea kukabana koo katika dakika za "lala salama" za kampeni ya kuwania kiti cha udiwani wa Kata ya Kirumba, ahadi, vijembe na hata vitisho vikiendelea kutawala kampeni hizo.

  Katika kushawishi wapiga kura kwa mgombea wake, CCM mwishoni mwa wiki kiliwapandisha jukwaani wanasiasa na wafanyabiashara marufu Jiji Mwanza, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC-Taifa) kutokea mkoani Mara, Christopher Gachuma na Mbunge wa Rorya, Lameck Airo, ambao kwa pamoja waliahidi kujenga barabara ya Kabuhoro kama mgombea wa chama chao atachaguliwa.

  Akizungumza katika kampeni hizo, Airo alisema yeye ni mwana Kirumba kwa kuwa amewekeza katika kata hiyo na kwa hiyo, yuko pamoja na watu wa kata hiyo katika kila hali. Airo ni mmiliki wa Hoteli ya La Kairo.


  Aliwaeleza kuwa ahadi zake ni za kweli na ushahidi ni jimboni kwake Rorya ambako aliahidi na kufikia Aprili, mwakani atakuwa amekamilisha ahadi zake.


  "Nina madawati kama 200 yako stoo tu, isingekuwa sheria za uchaguzi inakataza kutoa ningeyaleta hata leo, lakini hata hivyo baada ya tarehe 1, Aprili mkimchagua mgombea wetu, nitaita Mwalimu Mkuu mmoja baada ya mwingine kuwapatia," alisema.


  Akizumgumzia ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita tano inayopita katika Kilima cha Kabuhuro, alisema atasaidiana na Gachuma ili kujenga barabara hiyo kwa kuwa ana mitambo ya kujengea barabara.


  Akimnadi mgombea huyo, Gachuma aliungana na Airo akisema mgombea wao, Jackson Robert, ni kijana hodari na akipewa udiwani ataumudu kwa kuwa watamsaidia.


  "Nina magreda yamekaa ningeyatoa hata leo kama kufanya hivyo isingekuwa kinyume cha taratibu za uchaguzi, lakini niwahakikishie barabara hii ni kilomita tano tu wengi mnanifahamu ninawahakikishia yote yako ndani ya uwezo wetu, tutaimudu," aliahidi.


  Wakati makada hao wa CCM wakijinadi hivyo, CHADEMA wamebeza ahadi hizo kwa kusema CCM kimeishiwa sera na badala yake kinaleta porojo mpaka kwenye masuala ya msingi ya maisha ya watu.


  "Wenzetu hawa wamegeuza siasa kuwa sehemu ya ghiliba, hivi wamejua leo kwamba Kirumba kuna barabara mbaya? Hawa si wako hapa kila siku walikuwa wapi siku zote, hatuna nafasi tena ya kurudi nyuma, 2010 tuliamua kuanza safari ya ukombozi kwa kuwapiga chini CCM, hatuwezi kurudi nyuma, kura zote kwa Dani Kahungu," alisema Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, Wilson Mshumbushi.


  Alisema kuwa makada hao kama wangekuwa na dhamira ya dhati kwa wana Kirumba wasingesubiri wakati huu kwa kuwa chama chao kimeongoza kata hiyo kwa miaka 49 hiyo barabara na tatizo la madawati yalikuwepo na uwezo huo walikuwa nao, wangeweza kulifanya tatizo hilo historia lakini wanachofanya sasa ni ghiliba tu.


  "Miaka hamsini ya ‘uhuni' wa utawala wa CCM bado wana ujasiri wa kuzungumzia barabara na maji, marehemu diwani wetu Manoko ameongoza kata hii kwa miezi minane tu lakini amefanya mambo ambayo CCM haikuyafanya kwa miaka 48, msiwasikilize hawa," alisema.


  Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliwatahadharisha wakazi wa kata hiyo kuwa wasihadaike na CCM kwa kuwa chama hicho sasa kimekosa mwelekeo na kinahaha kujinusuru wakati tayari kimeshakata roho.


  Alisema mfumko wa bei chini ya Serikali ya CCM unakuwa kwa kasi kila siku kama mtoto anavyokuwa na kuongeza; "Inafika mahali mpaka mtu anaogopa kukua kwa kuhofia mfumko wa bei, hivi mnataka iweje ndiyo mjue CCM imechoka?"


  Henry Joseph, Jerry Tegete na Mrisho Ngassa watumika kushawishi kura

  Katika hatua nyingine, Diwani wa CCM Kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula, amewataka wana Kirumba kumchagua mgombea wa chama chake kwa kuwa atarejesha heshima na hadhi ya michezo kama ilivyokuwa awali kwa kuboresha viwanja ambavyo vitatengeneza vipaji.

  "Jack Atahakikisha viwanja vya michezo vya Magomeni na Kabuhoro vinatengenezwa ili kukuza vipaji, akina Henry Joseph, Jerry Tegete, Mrisho Ngasa wametoka hapa, lakini tangu ndugu zetu washike kata hii hatujazalisha vipaji tena, mchagueni Jack atarejesha heshima ya Kirumba" alisema.


  Bidhaa za Coca zatishiwa

  Mwenyekiti wa mtaa wa Kigoto, Kipara Bulemela kwa tiketi ya Chama cha Wanachi (CUF) akimnadi mgombea wa CHADEMA alisema wananchi wanachotaka si msaada wa wenye pesa, bali ni usimamizi mzuri wa mapato yao.

  "Halafu huyu Gachuma anakuja hapa kututishia pesa za soda, hizo Coca Cola si tunazinunua sisi, zinatokana na pesa zetu sisi walalahoi, sasa asipoangalia tutasusia hata soda zake tunywe pepsi peke yake," alisema.


  Kauli za wagombea

  Mgombea wa CHADEMA, Dani Kahungu ameahidi kuendesha harambee kubwa siku ya kuhitimisha kampeni, kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa elimu wa kata ili kuwasadia watoto wa wazazi masikini wasiojiweza katika kata hiyo.

  Amesema atasimamia upimaji maeneo ya milimani katika kata hiyo ili wananchi wamiliki halali wa maeneo yao na yawawezeshe hata kukopa kwa kuwa na dhamana ya ardhi.


  Kwa upande wake mgombea wa CCM, Jackson Robert, amewatahadharisha wafuasi wa CHADEMA kupuuza wito wa viongozi wao kukaa mita 100 kutoka kituo cha kupiga kura, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuzua vurugu zisizokuwa na sababu.


  Amesema endapo tafrani yoyote itaibuka katika uchaguzi huo wataokaoumia ni wazazi, mama na baba wa vijana wa Kirumba au hata ndugu na rafiki zao na hivyo akawasihi wasiwasikilize kwa kuwa wanaohamasisha hivyo familia zao ziko mbali.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Na bado wanashindwa Kirumba, Mwanza
   
 3. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  katika vita hata kama ni katoto kachanga, kama hujawapi kukapiga, tumia sila zako zote kukapiga. Unaweza ukaumbuliwa.

  Wache watumie silaha zao zote kama ni kwa uhalali.
   
 4. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Kwani Airo kawekeza leo hizo hotel zake za Lakairo??/ tangu nasoma Kitangiri sec mwaka 2000 hizo hotel zipo hapo kirumba iweje leo aseme atajenga ,,kwanini hakujenga enzi hizo,,,huyo gachuma haishi kirumba ,,hajazaliwa kirumba,,kwao Tarime hajajenga,,pale cocacola nje kuna barabara za karibu na kampuni yake lakini hajasaidia kujenga barabara ili malori yanayokuja kuchukua bidhaa zake zichukua vizuri bila usumbufu,,iweje aje kujenga kirumba,,,mmmmhhhhh ccm ndugu zangu tulikuwa tunawapenda sana ila uongo wenu unazidi kutukatisha tamaa,,tunawaomba mbadilike kidogo basi hata siku mojamoja muwe mnaongea ukweli,,
   
 5. e

  eddy JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,373
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hayo magreda yangeanza kazi kule igoma kwanza, baada ya uchaguzi ndo yaje kirumba ingekuwa sahihi sana.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Huyo Lakairo atawasabishia hao CCM kipigo cha Ziada, hizo Hotel alizojenga apo Kirumba zinatumika kudhalilisha mama zetu wanapokwenda kuoga, Lakairo Mwenyewe ni kinara wa kuwachungulia hata bibi vizee wakiwa bafuni hili linajurikana kirumba nzima sasa sielewi anapata wapi ujasiri wa kusema yeye ni muwekezaji.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jee, kuna uhusiano wowote na yule "mchumba" maarufu kuliko wote duniani ambae ni mke wa mtu?
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama watu wa kirumba watakubali uongo kama huu wa lakairo a.k.a rorya hawana mbunge na gachuma basi watakuwa wamepoteza heshima ya utu wao kwani ni ahadi ambazo hazitekelezeki.

  Kama wangekuwa wakweli hao magamba wangeshafanya hayo mambo kwani ccm ndio wamekuwa wakiiongoza hiyo kata miaka yote.

  Katika hili ccm wameishiwa na wamebanwa pumzi, tena bila aibu eti wanampeleka ngeleja kuwafanyia kampeni.
  Kabla hajaanza kuhutubia aulizwe kuhusu umeme na mafuta muone kama hajapoteza muelekeo na kukimbia jukwaa!
   
 9. H

  HOJA YANGU Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona CCM wanawakejeri wana kirumba? Grrrrrrrrrrrrrrrrr!
   
 10. bepari1

  bepari1 Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  ndiyo ndo baba yake na josephine mushumbusi kwani unatakaje mkuu? Kuna uhusiano gani kati ya comment yako na kinachojadiliwa kwenye hii thread? Lets discuss about issues and not people vinginevyo utaonekana shankupe!
   
 11. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nadhani watu tuliokaa mwanza tunaifahamu kirumba na sina hofu kuwa watu wa kirumba ni watu makini na walishasikia ahadi kibao za ccm na walishachoka kuwasikia na si ajabu wanaofika kwenye mikutano yao ni watu toka rorya kwa lakairo na sio wanakirumba. CCM has got no chance to stand against CHADEMA in mwanza. Kesho kitajulikana tu.
   
Loading...