"Utajiri wa Chenge" Nani awajibike??

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,948
710
Habari ya baadhi ya utajiri wa Mh. Chenge ulioibuliwa na gazeti maarufu nchini Uingereza The Guardians imewashitua watu wengi wakiwemo cabinet members wenzake. Maneno mengi yataongewa sana lakini the bottom line huyu Chenge ndiye anajua ukweli kuhusu huo utajiri wake. Inabidi aje mbele ya wananchi na aeleze ni jinsi gani ameweza kujikusanyia hizo fedha.

Anyway nirudi kwenye mada. Ninaamini kuwa Kiongozi yeyote wa ngazi ya juu katika serikali kabla hajachukuwa madaraka huwa anafanyiwa uchunguzi kuona uadilifu wake. Utaratibu huu upo na unafanywa na Usalama wa Taifa, nina ushahidi kuwa utaratibu huu ulikuwepo kwa sababu niliwahi kufanya kazi katika ofisi ambayo ilikuwa inaomba ushauri kutoka Usalama wa Taifa ilipofikia wakati wa kuteua viongozi wa serikali kama vile mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara n.k
Usalama wa Taifa ulikuwa na jukumu la kuangalia uadilifu na rekodi za mtumishi ambaye alikuwa anatarajiwa kupata Presidential appointment. Baada ya kupata rekodi zake ndipo Rais ana decide either kumteua huyo mtumishi/mtu au la kulingana na rekodi yake.

Kitu ambacho kinanishangaza mimi ni kwamba Mh. Chenge amekuwa mtumishi wa serikali kwa muda mrefu. Na kila alipokuwa anapata Presidential appointment faili lake lilitakiwa lipitiwe na hawa jamaa wa Usalama wa Taifa ili kubaini kama kulikuwa na vitu ambayo vilikuwa ninakwenda kinyume na maadili ya mtumishi.Sasa within 3 years huyu jamaa kapata Presidential appointment mara 2 lakini still faili lake halikupata kuangaliwa kubaini kama kulikuwa na kasoro yoyote. Huenda liliangaliwa lakini wakaamua kuziba midomo yao.
Sasa watanzania tuelezwe ukweli kama ili faili lilichunguzwa na recommendation zikapelekwa kwa JK kuwa huyu jamaa anafaa kuchukuwa nafasi ya uwaziri. Kama walibaini hayo maburungutu huko Jersey je JK alishawishika vipi kumpa cabinet positions 2 times bila kuuliza maswali kuhusu hiyo account? Na kama alipewa maelezo kuhusu hiyo pesa aliridhika vipi kama hiyo pesa imepatikana kihalali?

Hivi karibu kuna swali liliulizwa bungeni na hilo swali lilielekezwa kwenye ofisi ya Rais kuhusu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Na hilo swali liliuliza ni watumishi wa Umma wangapi ambao wamewahi kutuhumiwa au kugundulika na hiyo Sekretarieti kujipatia mali isivyo halali. Na hilo swali lilijibiwa kuwa hakuna hata mmoja. Sasa sielewi hii Sekretarieti inakwenda how much deep kuwachunguza viongozi wa Umma kuhusu mali wanazotaja. Maana Mh. Waziri katika ofisi ya Rais ambaye yuko responsible na hiyo Sekretarieti hiyo alidai hakuna kiongozi aliyedanganya katika kutaja mali zake. Leo hii tena Waziri wa nchi (Utawala Mtamu) anaonyesha mshangao kuhusu hiyo account. Hapa kuna mashaka kidogo kwamba kuna mtu au taasisi haifanyi kazi yake ipasavyo. NI NANI WA KUWAJIBIKA HAPA????? Usalama wa Taifa hilo hamkuliona kabla JK hajamteua kwa mara ya kwanza kuwa Waziri, Sekretarieti hamkuweza kuchunguza kwa undani zaidi ndani na nje ya nchi kujua kama mtumishi yeyote wa umma na akiba kupita income yake. Kama mlikuwa hamjui ukweli basi MMEPIGWA BAO SI TU NA CHENGE BALI KUNA WENGINE ZAIDI.
Huyu ni mtu mmoja kawapiga bao kwa account moja tu, maana hatujui anazo ngapi huko nje. Kwa hiyo alikudanganyeni, na huyo ni Chenge tu sasa je wengine vipi kama akina Mgonja, Mramba, Mkapa, Yona na wengineo???? Na kama mlijua ukweli kwa nini mlinyamaza? Na kama hamkunyamaza, mlimshauri vipi Rais kuhusu huyu jamaa. Hapa lazima watu wawajibike. Mambo yanakwenda tu kiholela, nakumbuka FS kabla hajawa PM faili lake lilipitiwa na watu wa Usalama kama ilivyo desturi lakini kwenye term yake ya pili faili liliteleza tu wakati kuna upupu tayari alikuwa ameshaanza kufanya. UCHAFU UMEKITHIRI KUPITA KIAMA.

Sasa katika hili nani wa awajibike hata kabla ya AC kuondoka maana dhis taimu AC haz no choisi dhan tu liv bifo hi get kicked aut. Nani awajibike? Usalama wa Taifa, Sekretarieti ya Maadili au Rais mwenyewe. Mie nilikuwa nafikiria wote mnatakiwa kuwajibika, Rais pamoja na taasisi zake za kisanii ili tuanze upya.
 
sahauni kabisa hakuna lolote hiyo hela hamtoisikia hata sikumoja......
huyu ndie JK

Naamini Mh. JK atakuwa na wakati MTAMU wa kuwaeleza wananchi kama ana sifa za kuendelea kuwa Rais wa JAMU na MHURI ya WADANGANYIKA. Chaguo ni dogo tu chagua mafisadi au kutumikia wananchi. Rais wetu yeye anaongoza nchi kwa Reaction. Naamini atasuburi hadi ikaribie kipindi cha uchaguzi ndo aanze kuwahadaa wananchi kwa kuanza kuwaajibisha mafisadi. Lakini akumbuke Tanzania ya Leo si ya 1922.
 
Inasikitisha sana kudhihirika hivi kuwa umaskini wetu ni wakujitakia.

Hebu fikirieni kiasi cha pesa inayozungumzwa kuibwa na watumishi/wanasiasa au kupitia mikataba uozo....Kiwila Coal Mine >TSHs 250 bil kwa mwaka, Richmund >TSHs 130 bil kwa mwaka, EPA, Melemeta, etc.

Huyu AC amekuwa Mwanasheria Mkuu tangu enzi Rais Mwinyi hadi miaka yote 10 ya jambazi Mkapa, leo hii senior minister. Mikataba yote ya awamu ya tatu imepitia mkononi mwake. Ni mwizi mkubwa

Hivi wana JF hakuna mtu anayefahamiana vyema na Watanzania wenzetu walioko kwenye pressure groups mbalimbali (wale wenye uchungu na matatizo haya ya nchi) pamoja na kwenye vyama vya upinzani wabebee bango hii ajenda ya ufisadi kwa kuitisha maandamano ya wiki nzima hata kwa jiji la Dar tu tujaye mitaani tumlazimishe Kikwete awateme chini mafisadi wote na kuchukuwa mali zao zote na kuwafikisha mahakamani. Naamini hii inawezekana kwani mwamko wa watanzania kipindi hiki ni mkubwa sana. Naomba tu tujipe matumaini kuwa haya mambo yanawezekana wala tusikate tamaa haraka. Pia Wafanyakazi kupitia vyama mbalimbali waweze kupigwa shule ili tuandamane kwani wafanyakazi tunaumia sana kila siku tunaambiwa serikali haina pesa kumbe inaishia mifukoni mwao, achia mbali kodi kubwa ya PAYE na VAT.

Lazima wapatikana wachache wa kuwaunganisha wa TZ ili kupinga ufisadi huu. Chonde chonde kwa wale wanaoweza kuwafikia akina Dr. Slaa, Zito, Wangwe, Lipumba, Sharif, Mtikila, Tundu Lisu, n.k. basi watusaidie kuanzisha ajenda hii kwa kuitisha maandamano kwa wk moja jijini Dar wakiombwa wakaazi wote kulaani vitendo hivi na kutoa masharti nini kifanye ili kusitisha maandamamo. Hivi sasa ajenda iko wazi kwa kila Mtanzania wala ajenda hii si ya chama fulani bali kila Mtanzania anaathirika sana.

Ahsanteni,
 
Sijui ni nani aliwaambia kuwa ni Dola milioni moja! kiasi halisi ni paundi milioni 5! Mmesikia hapa:

thanks.
 
Sijui ni nani aliwaambia kuwa ni Dola milioni moja! kiasi halisi ni paundi milioni 5! Mmesikia hapa:

thanks.

April 12, 2008 Saturday

SECTION: GUARDIAN HOME PAGES; Pg. 8

LENGTH: 892 words

HEADLINE: BAE corruption investigation switches to Tanzania: Focus on £28m radar deal with East African state: SFO's new director due to take over this month

BYLINE: David Leigh and Rob Evans

BODY:


Following the uproar over its halted Saudi investigation, the Serious Fraud Office is expected to decide whether to bring fresh corruption charges against arms manufacturer BAE within six weeks, over a second arms deal, this time with Tanzania.

A minister from the east African state has denied that more than $1m (£507,500) in his offshore accounts came from BAE.
Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Tanzania's anti-corruption bureau, which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to multi-million pound secret commission payments made by BAE.

Chenge does not dispute the money in his Jersey accounts. But he told the Guardian: "The obvious inference (of the investigations) is that I have received for my benefit 'corrupt payments' from BAE. This is untrue."

He said he was only involved in minor aspects of the radar deal, which was promoted by other ministries and approved by the Tanzanian cabinet. His bank records, he said, would show investigators that "there is no connection to the BAE Tanzanian radar deal".

His US lawyer from Cleveland, Ohio, J Lewis Madorsky, added: "While the matters in question took place a number of years ago, we can state . . . that any and all allegations of illegality, impropriety, mis conduct and unethical behaviour made against our client are categorically and vigorously denied".

Investigators say Chenge could be a valuable witness. The target of their investigation is not him but BAE. The arms company made the commission payments to a local agent in Tanzania to promote the £28m radar sale, through an elaborate chain of offshore companies and a Swiss bank.

The agent has now left the country and is wanted by Interpol.

These developments come at a key moment in the BAE saga. A landmark high court ruling on Thursday said that the decision to drop the SFO's Saudi inquiry was wrong.

In a huge embarrassment for the British and Saudi governments, the court rejected the claims that the inquiry had to be closed down for reasons of national security and because lives would be at risk.

And it took the extraordinary step of naming Prince Bandar, the crown prince's son, as the man behind what it said could be characterised as an attempt to pervert the course of justice.

Former prime minister Tony Blair caused uproar by personally forcing a halt to investigations into the Saudi deal. The Guardian subsequently disclosed that £1bn had been paid into accounts controlled by Prince Bandar during the deal. Bandar says the payments were not improper.

Inspectors from the Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD) grilled British officials in London last week about their failure to get results from any of their BAE investigations. Britain signed up to an international treaty to outlaw bribery, but there have never been any prosecutions.

The Tanzania deal, although smaller in cash terms than the Saudi deals, is equally controversial: Tanzania is one of the world's poorest countries, and the UK government is paying more than £100m this year to help the heavily-indebted country's budget.

It was Blair again who forced the radar deal through the British cabinet, despite protests from the then international development secretary, Clare Short. She said the sale, for which Tanzania had to borrow yet more from a commercial bank, was corrupt and "stank".

A lengthy SFO investigation in the UK subsequently discovered that 31% of the deal's contract price had been diverted via Switzerland.

BAE transferred the money to a subsidiary, Red Diamond Trading, registered anonymously in the British Virgin Islands.

Red Diamond then moved the cash to a Swiss account in the name of a Panama company, Envers Trading Corporation. This entity had two Panamanian nominee directors. But it was secretly controlled by a Tanzanian middleman, Shailesh Vithlani, according to Dar es Salaam court papers.

Investigators are now checking whether Vithlani arranged to pass any money in turn to Tanzanian politicians and officials.

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Vithlani, who is of Indian extraction but holds a British passport, is listed as wanted by Interpol.

He has been charged by the Tanzanian anti-corruption bureau with lying to investigators, but has left the country. His whereabouts are unknown.

According to the charges, Vithlani falsely denied he was the owner of the Panama company, and falsely claimed he had only handled a separate commission of 1% on the deal.

The SFO's new director, Richard Alderman, former head of UK tax investigations, is due to take over this month. The SFO refused to comment yesterday.

BAE, which has previously denied wrongdoing, also declined to comment, or to explain its chain of offshore payments, other than to say "BAE Systems continues to fully co-operate with the SFO investigation".

The company has recently launched an extensive public relations campaign and last week unveiled a report commissioned from a commercial consultancy, Oxford Economics, which claimed BAE was of key value to the UK economy.

LOAD-DATE: April 12, 2008
 
utashangaa Kikwete atanyamaza tu na hili.

Mkuu heshima mbele...
Waafrika ndivyo tulivyo.... atakaa kimya na kusubiria tusahau...kama alivyofanya baada ya kumsimamisha kazi Balali!!!

You are dead right!
 
The million-dollar question: Where did Chenge's fortune come from?


-New questions about integrity even as he denies radar bribery

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THERE are new question-marks in the air about how the Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge, was able to stash away more than $1m (over 1.2bn/-) in offshore bank accounts from his meagre salary as a public official.

This follows a report in last Saturday's edition of the UK Guardian newspaper that more than $1m has been discovered in offshore bank accounts controlled by Chenge, fuelling allegations that some of the funds originated from the 2002 radar deal.

Investigators from Britain's Serious Fraud Office (SFO), which has been probing the �28m (approx. 70bn/-) radar system deal, identified the money in Jersey accounts personally controlled by the senior minister and former attorney general.

According to the UK newspaper report, Chenge has not disputed the money in his offshore bank accounts, but he has denied suggestions that he received corrupt payments from Britain's BAE Systems, manufacturers of the controversial radar sold to the Tanzanian government.

Chenge is quoted as saying he was only involved in minor aspects of the radar deal, which was promoted by other ministries and approved by the Tanzanian cabinet.

His bank records, he said, would show investigators that ''there is no connection to the BAE Tanzanian radar deal''.

It is understood that the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to $12m (approx. 15bn/-) in secret commission payments made by BAE in connection with the radar deal.

Chenge was not available for comment yesterday. His mobile phone went unanswered several times when THISDAY attempted to contact him.

However, the ready admission by the minister that he has a million-dollar-plus fortune stashed away in offshore accounts abroad does raise new questions about his integrity and where the money may have come from, given past and present government salary rates.

Chenge has worked for the government for over three decades as a state attorney, attorney general, and cabinet minister.

At least one fellow cabinet minister has described the reports of Chenge's previously-undeclared wealth as ''quite shocking.''

''The amount of money we are talking about here is simply astonishing...such amounts of money are usually owned by governments, not individuals (within governments),'' the minister conceded to THISDAY on condition of not being named.

Several members of parliament from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) told THISDAY that the reports of the discovery of the massive wealth in Chenge's personal bank accounts has dominated weekend discussions in Dodoma, where the National Assembly is currently in session.

''We are all quite shocked about all this...Chenge has always looked prosperous, but we never suspected he could be an actual millionaire,'' said one CCM lawmaker.

''The big question is, how did he manage to amass such huge wealth? And did he declare this wealth to the government as public officials are supposed to?'' the lawmaker added.

The often outspoken opposition legislator, Zitto Kabwe (Kigoma North-CHADEMA), described the allegations against Chenge as ''very serious.''

''The minister must weigh the allegations against him, and take appropriate action,''said Kabwe, adding: ''If he deliberately failed to declare all his wealth as an MP, the National Assembly should seriously look into this matter.''

Amongst those who fiercely opposed the Tanzanian radar deal from the outset was Britain's former international development secretary, Ms Clare Short, who public said the sale - for which the Tanzanian government had to borrow yet more from a commercial bank - was corrupt and ''stank''.

A long-running investigation by Britain's SFO discovered that a staggering 31 per cent of the deal's contract price had been diverted via Switzerland, with around $12m in illegal commissions being paid to a Swiss bank account secretly controlled by middleman Shailesh Vithlani.

Investigators suspect some of this money was paid as bribes to several senior officials in the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa, in order for them to approve the radar deal.

At the time, Chenge was serving as Attorney General - the government's chief legal advisor.
· SOURCE: GUARDIAN
 
MIMI NADHANI TUMELOGWA,YAANI MPAKA WANAWANAAMUA KUCHUKUWA FEDHA NYINGI KIASI HICHO?
KWANINI TUSITETE MASLAHI YETU NASISI KAMA WAO WAENDA MPKA KWENYE MEDIA KUJITETEA KWAINI NA SISI TUSIJITETEE???
 
MIMI NADHANI TUMELOGWA,YAANI MPAKA WANAWANAAMUA KUCHUKUWA FEDHA NYINGI KIASI HICHO?
KWANINI TUSITETE MASLAHI YETU NASISI KAMA WAO WAENDA MPKA KWENYE MEDIA KUJITETEA KWAINI NA SISI TUSIJITETEE???

MKANYA naamini hatujalogwa ila kuna WATANZANIA wachache hawajali MASLAHI ya nchi na hawastuki kabisa kwamba UFISADI ni SARATANI mbaya kwa maendeleo ya nchi. Wao ni KUCHUKUA CHAO MAPEMA kwa kwenda mbele. Kazi kweli kweli, au ndiyo kuitikia kauri mbiu za "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na KASI MPYA-ARI MPYA-NGUVU MPYA". Mapambano na mafisadi lazima tuyadizidishe, hasa kwa kila MZALENDO na kila mwana JF!!!
 
MKANYA naamini hatujalogwa ila kuna WATANZANIA wachache hawajali MASLAHI ya nchi na hawastuki kabisa kwamba UFISADI ni SARATANI mbaya kwa maendeleo ya nchi. Wao ni KUCHUKUA CHAO MAPEMA kwa kwenda mbele. Kazi kweli kweli, au ndiyo kuitikia kauri mbiu za "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na KASI MPYA-ARI MPYA-NGUVU MPYA". Mapambano na mafisadi lazima tuyadizidishe, hasa kwa kila MZALENDO na kila mwana JF!!!

Hii kasi mpya naona ni kwa reverse!!! we are going backwards at a very high speed!!!
mmh inatisha....sijui hizi slogan huyu jamaa alikozitoa ila they were well planned!!
 
Kwa kweli inauma sana na hasa ukijua ukweli.Nakupongeza Nsololi kwa hoja ya maandamano nadhani kuandika imetosha sasa iliyobaki vitendo.Hela tamu viongozi wetu hawajali hata kama tunajua.Jamani tuandamane kushinikiza usafishaji wa Tanzania, wanasema maneno matupu hayavunji mfupa,tutasema mchana usiku tutalala, safari hii hakuna kulala mpaka kieleweke,hatuitaki Kenya ya leo na lazima tuikatae kwa vitendo.Ukijua madeni serikali inayojiingiza bila sababu utasikitika sana, nobody cares,tukumbuke madeni hayo yatalipwa na wototo na wajukuu zetu wakati wajukuu zao wamehamia Marekani.Haya shime vijana kwa wazee tukatae ufisadi kwa vitendo. Na J.K usipowawajibisha iko siku tutashika madaraka na tutawawajibisha vibaya.
 
Aliyekwambia TZ kuna salama wa Taifa nani? hakuna kitu kama hicho,kilikuwepo enzi za Nyerere baada ya hapo usaniitu, kila mtu anajichukulia atakavyo.Dawa ni moja wananchi wenyewe tuwe usalama wa Taifa na tuwawajibishe
 
Back
Top Bottom