Utajiri usioonekana kwa watu wengi Tukuyu Mbeya

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Kunavitu vinashangaza sana Tanzania wiki iliyopita nilipata fursa ya kutembelea maeneo ya wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya huko tukuyu nilifika Katumba nikaingia ndani huko kuna vitu vinaendelea naamini watanzania wengi hawajui.
Kijiji cha ISEBE kuna gase inayochimbwa kabisa na inasafirishwa kwajili ya matumizi ninahakika wengi hawajui na sijui ninani anachimba nilipotaka kupiga picha nilizuiwa na walinzi .

UFUAJI WA UMEME MTO SUMA
Wachina wametega mitambo yao kwenye mto suma na nguzo wamesha supply huko
Hayo ni maporomoko ya maji ambako wameweka mitambo yao huko.

LUTILI
Sehemu hii kuna gase sijajua ni gase gani inatoka ardhini ndege hawapiti juu ya eneo hilo wakipita wanakufa baada ya kuvuta hewa ya hapo hata binadamu ukivuta hewa hiyo kichwa kinauma sana wazungu naambiwa walifika wakapima na kuondoka

KANYELELE

Hi ni sehemu ambayo napo pana gase ni jilani na Mwakaleli huko wameshazungushia fance na ulinzi upo wanasubiri kuanza kuchimba

MASEBE MWAKALELI GASE
Sehemu hii wanachimba gase ya wanatoa Cabondioxide na Oxygen wana safirisha na magari sijui wanapeleka wapi hii Tanzania inamambo .picha imegoma kupanda wakuu.

Tena kunasehemu kuna udongo ule wa kutengenezea Sahani za udongo wachina wanafanya taratibu za kuanza kuuchimba ila ni kimya kimya

Ndizi nazo zipo za kumwaga nmekula sana na wale wapenzi wa Kitimoto aka mbuzi katoriki kilo ni 5000 unakula na ndizi hadi unasema basiii jamani hayo ndio niliyoyakuta nilipokuwa huko wiki iliyopita
IMG_20180316_140953.jpg
IMG_20180316_141001.jpg
IMG_20180316_132548.jpg
IMG_20180316_132557.jpg
IMG_20180316_132647.jpg
IMG_20180316_132824.jpg
IMG_20180316_141242.jpg
 
Tuko blessed sana mkuu..yaani tuna kila kitu,ila dah tunanuka umasikini..ukiwa mpenda adventure kama Mimi utagundua ninachomaanisha..wanasema tembea ujionee..
 
Karibu sana mkuu, huko ndo home sweet home. Japo kuna utajiri wote huo lakini wanainchi wanaishi maisha ya kawaida ya umasikini ingawa sura zao zina furaha muda wote.
 
Hizo gas kuanzia pale road ya kuelekea Tukuyu unapoanza kuteremka kwenye kona, upande wa kulia, kuna geti flani hivi ika ukipita nje unaona ndani ya uzio pamoja na tankers, wanasema mbona siku nyingi tu watu wanavuna!

Ile ndo njia ya mwakayembe, mwamyanga, mwamkusa, mwandiosasa, tula eksheni, n.k kuelekea makwao.

Nashindwa kushangaa kwakweli....
 
Daah umenikumbusha mkuu huko tukuyu kumebarikiwa Sanaa mwaka juzi nilikua kwenye trip bus likasimama Kijiji kimoja nikaagiza ndizi mbivu za buku yaani elfu moja
Nililetewa karibia nusu mkungu nilishaanga Sanaa...na hapo alitaka kuniongezea ..natamani kurudi huko ila hiyo chance sijapata.
 
Mkuu ulikuwa hujawahi kufika mitaa hiyo?hapo ndo tukuyu hongera kwa kufanya utalii wa ndani karibu tena ukajipatie mkungu wa ndizi sukari kwa jelo! Huku ukiendelea kushangaa rasilimali za nchi yetu yenye kila aina ya baraka!
 
Daah umenikumbusha mkuu huko tukuyu kumebarikiwa Sanaa mwaka juzi nilikua kwenye trip bus likasimama Kijiji kimoja nikaagiza ndizi mbivu za buku yaani elfu moja
Nililetewa karibia nusu mkungu nilishaanga Sanaa...na hapo alitaka kuniongezea ..natamani kurudi huko ila hiyo chance sijapata.
Karibu sana mkuu
 
Hizo gas kuanzia pale road ya kuelekea Tukuyu unapoanza kuteremka kwenye kona, upande wa kulia, kuna geti flani hivi ika ukipita nje unaona ndani ya uzio pamoja na tankers, wanasema mbona siku nyingi tu watu wanavuna!

Ile ndo njia ya mwakayembe, mwamyanga, mwamkusa, mwandiosasa, tula eksheni, n.k kuelekea makwao.

Nashindwa kushangaa kwakweli....
Tanzania yetu hii sijui tumelogwa wapi
 
Daah umenikumbusha mkuu huko tukuyu kumebarikiwa Sanaa mwaka juzi nilikua kwenye trip bus likasimama Kijiji kimoja nikaagiza ndizi mbivu za buku yaani elfu moja
Nililetewa karibia nusu mkungu nilishaanga Sanaa...na hapo alitaka kuniongezea ..natamani kurudi huko ila hiyo chance sijapata.
Mkuu nmekula ndizi huko balaa yani nazingine nmebeba
 
TOL ndiyo wanatoa cobon dioxide huko miaka mingi, kanyelele ndiyo ilianza, ni vituo viwili tu, umenyumbulisha, kwa mfano masebe ni njia ya kutokea huko kanyelele. Labda kama kuna vituo vipya sana!
Nani anamiliki mkuu
 
Kunavitu vinashangaza sana Tanzania wiki iliyopita nilipata fursa ya kutembelea maeneo ya wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya huko tukuyu nilifika Katumba nikaingia ndani huko kuna vitu vinaendelea naamini watanzania wengi hawajui.
Kijiji cha ISEBE kuna gase inayochimbwa kabisa na inasafirishwa kwajili ya matumizi ninahakika wengi hawajui na sijui ninani anachimba nilipotaka kupiga picha nilizuiwa na walinzi .

UFUAJI WA UMEME MTO SUMA
Wachina wametega mitambo yao kwenye mto suma na nguzo wamesha supply huko
Hayo ni maporomoko ya maji ambako wameweka mitambo yao huko.

LUTILI
Sehemu hii kuna gase sijajua ni gase gani inatoka ardhini ndege hawapiti juu ya eneo hilo wakipita wanakufa baada ya kuvuta hewa ya hapo hata binadamu ukivuta hewa hiyo kichwa kinauma sana wazungu naambiwa walifika wakapima na kuondoka

KANYELELE

Hi ni sehemu ambayo napo pana gase ni jilani na Mwakaleli huko wameshazungushia fance na ulinzi upo wanasubiri kuanza kuchimba

MASEBE MWAKALELI GASE
Sehemu hii wanachimba gase ya wanatoa Cabondioxide na Oxygen wana safirisha na magari sijui wanapeleka wapi hii Tanzania inamambo .picha imegoma kupanda wakuu.

Tena kunasehemu kuna udongo ule wa kutengenezea Sahani za udongo wachina wanafanya taratibu za kuanza kuuchimba ila ni kimya kimya

Ndizi nazo zipo za kumwaga nmekula sana na wale wapenzi wa Kitimoto aka mbuzi katoriki kilo ni 5000 unakula na ndizi hadi unasema basiii jamani hayo ndio niliyoyakuta nilipokuwa huko wiki iliyopitaView attachment 720426View attachment 720430View attachment 720431View attachment 720432View attachment 720439View attachment 720440View attachment 720441
ulizuiwa na walinzi kupiga picha,sasa hizi ulizoziweka hapa ni za wapi? au unapotosha
 
Malamba waterfalls.....napakumbuka hapo nishawahi kufika...mbeya hasa upande wa tukuyu kuna waterfalls za kutosha...usisahau kupanda mlima rungwe
 
Back
Top Bottom