Utajiri ni nini?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Ninaomba tujadili hii mada, maana halisi ya utajiri ni nini? Pesa na mali vinaweza kukupa furaha duniani? Kuna raha gani ya kuwa tajiri ilhali umezungukwa na masikini katika nchi, mji mtaa hata kijiji unachoishi?

Watafiti wa uchumi wanasema 5% ya wakazi wa dunia hii ndiyo wanaomiliki utajiri wa dunia hii. Utajiri huu ungegawanywa sawa kwa kila binadamu wote tungeweza kuondoa umasikini wa kutupwa (absolute poverty).

Duniani tunaishi na tunakufa, kuna faida gani ya kuua, kufanya makafara au kuiba ili uwe tajiri. Uwe tajiri ili iweje?

Kwa maoni yangu ninadhani kitu cha muhimu ni kupambana ili kupata mahitaji ya lazima. Nyumba, chakula, matibabu, elimu, dini, nguo na familia.

Watu wengi hawafahamu hili kuwa unaweza kuwa tajiri lakini kama huna familia utajiri wako hauna maana. Ni mara chache mno watoto wako kukuibia mpaka ufilisike. Hata hivyo, utakapo kosa mtu wa kuongea nae uzeeni utajiri wako utakuaaidia nini?
 
Pana watu mbalimbali wamepata kutoa tafsiri / falsafa ya utajiri:

1. Pastor mmoja, alipata kufundisha kuhusu "How to be Rich" , na akatoa tahadhari papo hapo, kwamba hazungumzii, "How to Get Rich kwa vile si mfundishaji wa "Prosperity Gospel". Mafunzo yake ni ni kuhusu, "How to behave as a rich man". Anasema kila mtu, hata ambaye wengine wanamuona tajiri, hujiona yeye siyo tajiri kwa vile huwaona wenye mali kuliko yeye kwamba ndio matajiri.

Tajiri ni mtu mwenye hela kuliko mimi. ~ Hii ndiyo definition ya utajiri ambayo matajiri (watu wenye kipato kikubwa kuliko dola mbili kwa siku) huitumia. Kwa mujibu wao, Utajiri ni pesa / mali nyingi kuliko ulizonazo.

2. "Pesa na mali ni vitu vya kupita. Lakini hakikisha vinapitia kwako" ~ a viral message. Hawa ni materialistic.

3. Kuhusu charity/usawa, Ayn Rand anasema matajiri waachiwe uhuru wa kuamua namna na kiasi cha kusaidia the underprivileged.
 
Kitu ninachojiuliza ni kwanini Yesu ambae amekua na jina kubwa duniani na kufanya miujiza mingi. Ni kwanini hakuzaliwa kwenye familia ya kitajiri na kuishi maisha ya fahari. Badala yake alizaliwa kwenye zizi la ng’ombe, baba mlishi alikua fundi seremala na yeye alifundishwa kazi hii tangu akiwa kijana mdogo.

Inawezekana aliona masikini ndiyo wengi duniani, hivyo akiwa katika hali ile itakua ni rahisi ujumbe wake kuwafikia wengi.

Au ni kutufunza kuwa mali ya duniani haina faida nyingi kwako, lilia utajiri wa Ufalme wa Mungu.

Funzo lingine ni kuwa binadamu unahitaji ujuzi utakao kupa rizki.
 
Mlenge ni tabu sana kuwa na pesa za ziada ilhali umezungukwa na masikini wa kutupa. Ninakumbuka miaka mingi kidogo mjomba wangu alistaafu na kuamua kurudi kijijini. Alijenga nyumba ya kawaida lakini kutokana na maisha aliyoishi nyumba ilikua na madirisha ya vioo. Sababu kubwa ya kuweka madirisha haya ilikua ni kujikinga na baridi.

Alifanikiwa kununua Land Rover 110 kutoka kwa Mzungu aliyemaliza mkataba wake wa kazi. Basi kijijini mjomba alionekana ni tajiri mkubwa.

Gari yake ilikua ndiyo ambulance ya kijiji. Usiku saa nane aliamshwa kuna mzazi amepata uchungu. Kuna wakati anaingia tu ndani mnamuwekea chakula analetewa habari kuna aliyeanguka juu ya mti anatakiwa kukimbizwa hospitali.
 
Mlenge ni tabu sana kuwa na pesa za ziada ilhali umezungukwa na masikini wa kutupa. Ninakumbuka miaka mingi kidogo mjomba wangu alistaafu na kuamua kurudi kijijini
Mtu mmoja alipata kutuambia duniani hakuna mtu maskini. Kama ukiangalia mipango na matamanio ya watu, wote wangependa kuwa katika maisha bora yasiyo ya umaskini. Shida ni kwamba mipango na matamanio yao hayatimii. Kwa hiyo, tajiri ni mtu ambaye mipango na matamanio yake yametimia.

Kama Mwenyezi Mungu amemkubalia mtu akapata utajiri (kwa maoni ya wanaomzunguka), ina maana Mungu amekubali mipango na matamanio ya mtu huyo yatimie. Lengo kuu la Mungu kumkubalia mtu huyo afanikiwe, ni kumuwezesha awasaidie watu fulani kwa wakati fulani, kwa namna aliyokusudia Mungu. Yaani mtu huyo anageuka kuwa kipitishio ( conduit ) ya kuwa msaada kwa watu wengi.

Baba yangu alipata kutuambia kwamba Mungu alikasimu madaraka ya vitu vyote kwa wanadamu na malaika, lakini jambo moja tu alibaki nalo Yeye Mwenyewe, ni kugawa riziki. Kwa hiyo, kwa mfano wa huyo mjomba aliye kijijini, Mungu anamtumia ili kazi yake Mungu ya kugawa rizki iwe fanisi kuwafikia wale aliowalenga.

Siku ambayo ataacha kuwatumikia wananchi, hata hilo Land Rover 110 litaanza kupata majanga yanayoyapata Malendrova mengine. Kwa sasa hilo Landrover linalindwa na Mungu kwa vile ndiye analitumia kwenye kazi zake za kugawa rizk, na linalindwa pia na wananchi ambao humkumbusha Mungu kupitia sala zao na shukran zao kwa mjomba wanapomuombea kheri kwa msaada anaowapatia.

Ni hivyo pia kwa cheo, madaraka, mamlaka, elimu, uwakilishi na namna zote zinazomuinua mtu mmoja ukilinganisha na wenziwe.
 
Mtu mmoja alipata kutuambia duniani hakuna mtu maskini. Kama ukiangalia mipango na matamanio ya watu, wote wangependa kuwa katika maisha bora yasiyo ya umaskini. Shida ni kwamba mipango na matamanio yao hayatimii. Kwa hiyo, tajiri ni mtu ambaye mipango na matamanio yake yametimia...
Mjomba alishatangulia mbele za haki akiwa na umri wa miaka 87. Tangu habari za msiba zinafika kijijini mpaka mwili unafika kutoka Muhimbili hatukugharamia chakula wala kuni za kupikia.

Chakula pekee familia iligharamia ilikua karamu ya mwisho baada ya misa na watu kuona sura ya mwisho. Hii pia ilipata mchango wa ng’ombe kutoka kijijini.

Tuliuona utukufu wa Mungu kupitia maisha yake RIP mjomba.
 
Mjomba alishatangulia mbele za haki akiwa na umri wa miaka 87. Tangu habari za msiba zinafika kijijini mpaka mwili unafika kutoka Muhimbili hatukugharamia chakula wala kuni za kupikia...
Poleni. Aliishi vizuri na watu. Na watu huwa si wajinga, hata ikiwa ni matajiri au wana umaskini wa kipato, huweza kujua mtu anayewathamini utu wao. Waliweza kufanya hayo yote si kwamba wanarudisha fadhila, bali ni sehemu ya kusema asante, na kumuaga mpendwa wao. Juzi tu nimetoka kusikia kisa cha mtu aliyeonekana tajiri kijijini, lakini alikaa vizuri na watu. Alipofariki, ndugu walitaka kumzika mahali pengine; wanakijiji wakasisitiza sana azikwe kijijini kwao, kwa kumuenzi kwa namna alivyokaa nao vema. Ikabidi ndugu wakubali.

Kusaidia kwa nia njema hakujifichi. Hali kadhalika kusaidia kwa masimango. Duniani ni mapito tu. Sote tu wasafiri kwenye chombo kimoja. Nobody gets out of this world alive. Over a long period of time, we are all dead. Tumche Mungu, na tutendeane mema kila mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom