Utajiri ni Dhana Nyeti

Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,474
1,079
Habari ni wanagenzi, najua wengi mmechoka na purukushani za kutafutia tumbo mlo na watoto ada ya shule, bila kusahau kale kanakobakia kuendeleza msingi wa kibanda au kulipa kodi kwa wajanja waliowahi kufikiria kuna watu watahama kwao na kujitenga na wazazi wao na hivyo lazima watapanga. Suala ni hili Vijana wengi tumekuwa na uchu wa maendeleo kwa kuwa matajiri; lakini tujiulize matajiri walio wengi utajili wao ni kisayansi/kitaalamu au kishirikina? Na wewe kijana unapojitusu kwenye huo mchakato wa kuwa tajiri umekaa na kufikiria ni jinsi gani utafikia hayo malengo, tuache speed twende taratibu aisee, siyo unaona Mkude ana V8, BMW, Vogue, Murano, na Hutu tugari tudogotudogo wanatuita vitz au hii inaitwa IST(Inadumu Siku Tatu) na wewe macho yanakutokaaa; ahaha jamani tuache tamaa bora kidogo unachokula kwa furaha kuliko kingi unachokula kwa mateso!! Acha haraka; siku moja nilikaa na Mzee mmoja baa akaniambia kijana naona kila nikiagiza bia na wewe una agiza, je ukifikia umri wangu hizo pesa Si ungekuwa umefungua kampuni yako ya breweries!! Duh niliona aibu aisee, ila kilicho muhimu tupunguze SPEED ya kumiliki kila kitu;
 
kuwa na nidhamu ya pesa na kuwa na kiasi kwa kila kitu. ni sawa pia. Ila mwanagenzi tupiamo kapicha basi kuweka msisitizo
 
Back
Top Bottom