Utajiri huu: Si mimba zote za vichaa ni za wahuni

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Kisa cha jana kimenihuzunisha sana, yule mama kichaa aliyejifungua kichanga jana kisha akakinyonga halafu akawa anatembea nacho mitaani
Polisi wamem clear, ameachiwa huru na hana kesi ya kujibu
Huwa tukiwaona hawa watu wenye matatizo ya akili tunazani hawana hisia, na ikitokea wamepewa ujauzito huwa tunakimbilia kuwasingizia wahuni..... Kuwa muhuni Tanzania ni janga..!! Kila baya ni lako
Nyuma ya pazia, huko gizani na haya mambo ya utajiri heshima umaarufu na madaraka kuna mengi ya kutisha na kushangaza sana
Kuna matajiri wamezaaa na hawa vichaa kutokana na masharti ya waganga wa kienyeji.... Chizi kichaa ama mwendawazimu anaporopoka ama kupayuka kuwa huyu ni mtoto wa fulani sio bahati mbaya anaongea ukweli... ILA hawezi kuaminika kwa watu kutokana na hali yake
Hawa watu pia ni binadamu wana hisia Kama wanadamu wengine, wana maumivu.... Inapotokea wakaguswa kidogo wakaumizwa!!! kwa ajili ya matatizo yao wanakuwa wanakosa utashi wa kuamua kwa weledi
Trust me sio mimba zote za vichaa ni za wahuni... Na kila kichaa aliyezaa anafahamu kwa hakika baba wa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila inategemea na level ya ukichaa ya huyo mtu, kuna vichaa wametokana na hali ngumu ya maisha au kuna tukio tu likamchanganya akili, huyu sometimes antenna inadaka na muda mwingine inapotea. Ila kuna wale vichaa full yaani hawa sio mwezi mchanga bali mwezi uliokomaa kabisa, hawa hata wakipindwa nyuma ya nyumba gizani hata kwenye mwanga hawawezi mtambua mtu
Kazi kwa hao matajiri kubaini mwezi mchanga na ule uliokomaa kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IGcNhJx0kR2t8Bam5YHjCC17.png


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli mkuu na tabia kama hizi zipo kwa muda mrefu sana na zimeshaanza kuota mizizi kwa sababu ya imani zisizo na vichwa wala miguu.

Ila kiukweli ni kukosa utu, kwa sababu kama utajiri upo upo tu cha muhimu kuchakarika.
Hivi utajiri wa kuchakarika unapatikana kirahiso kama huo?

nafight with my weather
 
Back
Top Bottom