Utajiri huo wadau | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri huo wadau

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by babukijana, Aug 28, 2009.

 1. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  MSAADA WAKO UNAHITAJIKA!


  [​IMG] Nisingependa sema jina langu, ila nitatoa mawasiliano yangu na napatikana wakati wowote hata usiku, sasa jamani mimi ni mtanzania mwenye miaka 26, nimesumbuka na maisha sana mpaka hapa nilipo naweza sema mwingine anaweza kuzaliwa mpaka kufa bila kufika hata nusu ya mambo niliopitia, kila kukicha mimi naangalia ni namna gain nawezapiga hatua kwenda mbele kimaisha suala la umaskini mimi sipatani nalo kabisa.Bila kupoteza muda wa mhariri naomba kusema, Tanzania hii imejaa kila aina ya jambo na kila siku mapya yanatoka, sasa jamani mwenzenu nimepata mahali ninaweza kutoa umasikini kabisa lakini sasa binafsi nimeshindwa kutoa umaskini huo. Wakati wajerumani

  wanaondoka nchini, mkoa Fulani( nisingependa kuutaja jina mpaka pale nitakapo fanikiwa) walichimbia dhahabu, rupia na vifaa vingine chini. Babu aliefariki juzi ambae alikua miongoni mwa watu waliokua vibarua wa watumwa wa kijerumani ndio alikua miongoni mwa vibarua waliochimba shimo hilo na kufikia dhahabu hizo, na hapa namnukuu(-Mimi na wenzangu ndio tulichimba shimo hilo, na baada ya kumaliza na kulipwa ujira wangu niliondoka wenzangu walibaki kwa nia ya kuendelea lakini hawakuonekana tena) huo ni usemi wa babu mwenyewe.  Baada ya kufanya utafiti wa hapa na pale, na hatimae kusafiri mpaka kufika eneo husika niloshawishika kuanza kuchimba nakuona nini nitatoa, ila mambo hayakua kama nilivyotarajia, baada ya kuchima kama mita mbili, tukakuta kokoto, tukaendelea kuchimba tena kwenda chini kwa umbali mrefu hadi tukakuta maji mengi sana chini, sasa tuikua timu ya watu 10, binafsi mimi ni mkristu tena mkatoliki lakini ilinibidi kukubali ushauri wa wenzangu waliniambia bwana haya mambo hayaendi namna hii, hua hatutoi kwa misingi hii ni lazima twende kwa mganga, hakika mimi sikwenda lakini wenzangu wao walikwenda na kweli kupata ushauri manake mganga aliwaambia Aaah ninyi mmeacha mali juu mmechimba kwenda chini rudini mchimbe kwenda kushoto kweli walirudi na tukaanza kuchimba kwenda kushoto hapo sasa ndipo niliona maajabu ya dunia.  Baada ya kuchima umbali kidogo tuu nikaona zege imemiminwa, kwa elimu nilionayo yale mawe yaliotumika ni granite stone yale ni magumu sana, tukapasua nakukutana na udongo tena nakuendelea kuchima kisha tukakutana na sealed nyingine tena kama ile ya mwanzo tukapasua na kuendelea pia kwenye udongo wa kawaida ila pakawa na giza nene sana, tukaamua kununua tochi japo hazikusaidia manake it was reall amazing miracles yaani ukiingia na tochi batteries ni mpya kabisa ila zinaisha hapo hapo hapo haziwaki,tukasema ok tukawa tunatumia vibatari vile vyenye tambi kubwa kabisa kiasi ya kwamba hata pakawepo upepo wa namna gain hakiwezikuzimika lakini bwana pakawa panatoka ma inzi makubwa sana na yalikua kazi yake yanazima vibatari vile tuu.alafu vikishazimika pakawa giza unasikia watu wanaita kwa sauti zile za kihuni (psiiii psiii psiii) baaada ya hapo pakatokea kutoelewana kabisa kati yetu mpaka kazi ikaishia hapo.  Sasa mimi nataka kuchimba pale, nataka kutumia jasho pale maana sio ndoto za kusadikika pana mali chini ila hali ndo hio, sasa dhumuni haswa la kukuandikia waraka huu nikwamba kila kukicha kupitia magazeti nasikia waganga chungu nzima na vioja kibao, naomba nisaidie kutangaza tenda hii awe ni mganga mimi nitajitolea gharama zoote kwenda mpaka pale na kutafuta vijana wa kuchimba manake nina hakika gharama zao hazifiki hata milioni mbili lakini sasa nina hitaji mganga wa kweli sio wale matapeli yaani malipo ni baada ya kazi kuonekana! Ama kama kuna mtanzania mwingine mwenye utalaamu huo ama yupo tayari kushikana na mimi tuakaenda vitani kujitoa mhanga kinachotoka tunagawana nusu nusu nina hakika gazeti lako tukufu litanisaidia, na kwa lolote ama anaetaka kukutana na mimi kwa maongezi zaidi anaweza nipata kwa namba +255688433961 natanguliza shukrani zangu.
   
 2. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  haya nimewaletea hii wanajamii najua jamaa anaweza akapata company hapa kwenye jitihada zake.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mods.....I don't think you are able to allow JF to be this low!
   
 4. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yes i think hii hoja ina ualakini. Wakoloni walikuja kuvuna madini kama hizo dhahabu na usafiri walikuwa nao tena ni meli sasa iweje wazichimbe chini waziache. walikuwa wakidanganya mababu zetu kwa pipi na wao kupewa madini ni lini hawakujua thamani ya dhahabu?
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Msaada pekee anaouhitaji mdau ni kwenda shule kufuta ujinga!
   
 6. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  dhahabu waifukue chini then waifukie?huyo babu yake nae hamnazo kama kweli aliexist,wazungu wamekuwa wajanja miaka 1000 back leo hii 1990's wafukie dhahabu?tena kwa kuishindilia kwa gharama kubwa?ili nini?kwa mwenye akili ataelewa,otherwise huyu jamaa kadata.kuna watu mererani wanauchu miaka yote wangeshaichimba,
   
 7. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  babu si lazima uchangie,ukiona inakuzingua anza tu thread ziko kibao mzee
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hii inareflect weakness ya Mfumo wa elimu yetu. Mkuu tembea uone.
   
Loading...