Utaifa wa Zanzibar ulizaliwa Kabla ya Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaifa wa Zanzibar ulizaliwa Kabla ya Tanganyika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHIBUU, Apr 6, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Nashangazwa sana kuona watanganyika wanakuwa na viburi sana,na kuwakashifu wazanzbari,na nchi ya zanzibar kwa ujumla,nakumbuka mara ya mwisho pinda kutamka kuwa zanzibar sio nchi sasa leo hii niwapa hii ramani kabla pinda hajazaliwa,wala taifa lake halijazaliwa,lazima tuwekeane heshima.

  Ni jambo la kusikitisha kuona Utaifa wa Zanzibar uko ukingoni kupotezwa katika Ramani ya Dunia. Nawaletea ramani kongwe ya Bara la Afrika ambayo inaonesha mipaka ya Zanzibar mpaka mwaka 1669. Angalia ukubwa wa Taifa la Zanzibar ulivokuwa wakati huo na ulinganishe na ile ilivyokuwa kabla ya 26 April 1964 .
  View attachment 26806

  Ramani hii inaonesha kuwepo kwa Zanzibar kabla ya kuzaliwa nchi za Afrika Mashariki, Zambia na Zimbabwe.

  Nadhani mutaweza kupata mwanga kiasi gani Utaifa wa Zanzibar umemegwa kidogo kidogo hadi kubakia visiwa vya Unguja na Pemba. Kwa kweli, hili ni jambo la kusikitisha sana. Historia inatufunza kwamba, kwa kiasi kikubwa umegaji huo wa Taifa la Zanzibar ulifanywa kwa kuwashirikisha Wanasiasa, Watawala wetu wa Zanzibar, vita pamoja na Wakoloni.
  Hivi karibuni tunakabiliwa na muswada wa kurekebisha Katiba ya Muungano ambayo itatoa dira ya Watanazania with respect to Zanzibar. Scenario yenye nguvu ni kuwa tayari Watanganyika wameshajua matokeo ya mchakato mzima, kwani vigezo vilivochongwa katika muswada huo ni vile vitavoimeza kabisa Zanzibar.
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ramani ya Africa ya karne ya 16 !!
  Ramani ya Zanzibar!!
  Lol! Zenj-bar map!!

  Haya, ngoja waandike wengine.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo unataka uturudishe miaka ya 1600'?
   
 5. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baada ya muungano znz ilikoma kuwa nnchi na ndio maana waliohukumiwa kwa uhaini mahakama iliwaachia huru.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hata himaya ya ethiopia ilikuwa inafika Afrika kusini. So what are you saying? Tuwarudishie mwambao wa pwani hadi Morogoro? Halafu kisha tumrejeshe Sultani?
   
 7. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Tanganyika 1815-1886
  Tanganyika kama taasisi ya kijiografia na kisiasa haikuchukua sura kuwapo katika ramani ya Afrika kabla ya wakati wa Ubeberu Mkuu (High Imperialism), jina lake limeanza kutumika baada ya kile kilichojulikana kama "Ujerumani ya Afrika ya Mashariki" kuhamishiwa kwa Uingereza chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa katika 1920. Hii ndio katika historia ya eneo ambalo litakuja kujulikana baadae kuwa ni Tanganyika.
  Katika 1698 na tena katika 1725 wa-Omani waliwang'oa Wareno kutoka bandari za biashara kwenye pwani ya Afrika Mashariki, hasa kutoka Kilwa na Zanzibar. Wakati wa karne ya 18, Zanzibar alikuwa ilijitokeza kama bandari kubwa ya kanda na pwani ya Afrika Mashariki. Biashara kwa ujumla ilikuwa na ikafanikiwa, mlolongo wa miji ya pwani biashara, kati yao TANGA na BAGAMOYO, alikuwa na kushamiri.
  Katika 1841, Sultani Sayyid Said kuhamishia makao makuu yake kutoka Muscat na kuleta Zanzibar; pamoja naye walikuja Waarabu wengi ambao waliukuza uchumi. Katika 1856, Usultani wa Zanzibar ulitengwa na Usultani wa Oman, na Zanzibar ikabaki na mamlaka yake ikiwa na kisiwa cha Pemba ikiwemo ardhi ya pwani ya Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na Kilwa. wafanyabiashara wa Kiarabu walimarisha njia na misafara katika maeneo ya ndani ya Afrika, ngamia ikiwa ndio vyombo vikuu vya usafiri.
  Bandari ya Zanzibar ilikuwa ikitembelewa na meli za Kiholanzi, Kiingereza na Ufaransa. British East India Company alikuwa mwakilishi wa Zanzibar, ambaye alifanya kazi kama mshauri wa Sultan.
  Mwaka 1848 Misionari wa Ujerumani Johannes REBMANN ‘aligundua' Mlima Kilimanjaro, nae Burton na Speke 1858 ‘aligundua' Ziwa Tanganyika.
  Katika 1877 mfululizo wa kwanza wa misafara ya Ubelgiji aliwasili Zanzibar. Katika mwenendo wa misafara hiyo, mwaka 1879 kituo cha kwanza kilianzishwa KAREMA ukingoni mwa mashariki ya Ziwa Tanganyika, na kufuatiwa na kituo cha MPALA ukingo wa pili yake magharibi ya ziwa hilo.
  Vituo vyote walikuwa vilianzishwa kwa jina la COMITE D'ETUDES DU HAUT CONGO, shirika lililoitangulia kile kilichoitwa Kongo Free State. Ukweli ni kwamba kituo hiki kilikuwa kimeimarishwa na kuhudumiwa na mahitaji yake yote (supplies) hutolewa kutoka na kuongozwa kutoka Zanzibar na Bagamoyo kilipelekea kuingizwa Afrika Mashariki katika eneo la Bonde la Kongo (CONVENTIONAL BASIN OF THE CONGO) katika Mkutano BERLIN wa 1885.
  Katika meza ya mkutano wa Berlin, kinyume na mtazamo mkubwa, Afrika haikuwa partitioned; badala yake sheria zilianzishwa na kuimarishwa miongoni mwa mamlaka za ukoloni na mamlaka ya kikoloni zilizotarajiwa jinsi ya kuendelea katika uanzishaji wa makoloni na Himaya (protectorates). Wakati maslahi ya Ubelgiji haraka kujilimbikizia kwenye Mto Kongo, Waingereza na Wajerumani wa Afrika Mashariki na katika 1886 partitioned bara Afrika Mashariki miongoni mwao wenyewe; Usultani wa Zanzibar, ukaporwa mamlaka na kubakizwa na visiwa vya Zanzibar na Pemba, na kubakia ‘nchi huru'.
  Kongo Free State hatimaye iliazimka kuondoa madai yake juu ya Karema (kituo kikongwe katika Afrika ya Kati) na katika wilaya yote ya mashariki ya Ziwa Tanganyika, na kuachia mamlaka kwa Ujerumani
  Nitawaletea Ramani nyengine kongwe kuliko hiyo ambayo inaonyesha Himaya ya Zanzibar ni kubwa zaidi kuliko hivyo ilivyo hapo, pia ramani ya eneno ambalo mpaka 1886 bado likijulikana kama German East Africa na mgao wa makabila yalokuwako wakati huo.
  Baadhi ya interesting things katika historia ya Tanganyika ni kuwa katika kipindi hicho Mkoa wa Kigoma ulikuwa chini hizo Congo Free States mapaka 1920 ndio ilikabidhiwa kwa Tanganyika chini ya Uingereza!
  Hamba ndipo hoja kubwa ni vipi Taifa lililozaliwa takriban miaka 1300 ilyopita linatak kfutwa na kutawaliwa na Nchi iliyoasisiwa miaka 1220 baadae yaani miaka 90 iliyopita! Huu ndio Ukoloni Mambo leo!
   
 8. K

  Kasesela Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, dunia nzima imebadirika sana tangu wakati huo; kama ulivyosema, vita, makubaliano ya kisiasa, kupeana ardhi kama zawadi (kumbuka mlima Kilimanajaro), wakubwa kuuza (kumbuka ukanda wa pwani wa Kenya) na uvamizi tu, na mwisho ukoloni. Nenda ulaya na asia mambo hivyo hivyo. Usisahau kwamba kabla ya vita ya kwanza hapakuwa na Rwanda na Burundi, Sudan ilikuwa ndani ya Egypt, Cameroon na Somalia zilikuwa nchi mbili mbili na kadharika.
   
 9. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huyu ni kama kakaa sehemu anakunywa viroba! Kufukua ramani mbalimbali za karne ya 14,15,16....nk ni kazi rahisi tu. Cha muhimu je una motive gani?. Duniaa wakati huo ilikuwa tofauti na tuionavyo leo. Ukiacha geographical baundaries,nyakati hizo tawala zilikuwa zikiongozwa na wafalme,machifu,watwa,watemi na ma sultan. Je kwa mfano tu unafahamu Wahehe walikuwa na tawala yao yenye nguvu na very respected chini ya Mtwa Mkwawa?. Na alikuwa na mipaka ya nchi yake inayotambulika na kuheshimiwa? Vivyo hivyo kwa Mangi Mareale,Chifu Isike,Mtemi Milambo,Chifu Kibasila,Chifu Mangungo,Chifu Mazengo...... nk. Je tuanze kulilia sasa hivi tawala zile zote na mipaka yao ya ki jiografia zirejeshwe?. Kwani nikirejea picha ya wakati huo,kulikuwa na wavulana shupavu,wasichana warembo watoto wenye furaha na wazee wenye busara waliokuwa wanajiheshimu na wakiendesha maisha yao vizuri kwa busara na kwa hekima,nchi zao zilikuwa na nafaka,mifugo,mbogamboga asali nk vya kusaza,na walikuwa tayari muda wowote kulinda mipaka ya himaya zao. Vyote vilibadilika kutokana na mabadiliko ya dunia ki siasa,kiuchumi,kijamii kisayansi nk. Mabadiliko hayo hakuna hata mwanadamu mmoja anayeweza kuyashikiria na kuyazuia. America kwa u asili wake ni ya wahindi wekundu(Red Indians) wako wapi leo?.Whats so special with Zanzbar?
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Afadhali umemjibu vizuri! Haya mambo yatazidi kubadilika maana miaka ijayo tutakuwa na Political Federation of East Africa, kwa hiyo hatutakuwa na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kama nchi huru!
   
Loading...